JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
TAARIFA KWA UMMA
TAARIFA YA KUSITISHWA KWA AJIRA ZA KONSTEBO NA KOPLO WA UHAMIAJI ILIYOTOLEWA JANA NA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI HAIHUSIANI NA AJIRA 70 ZILIZOTOLEWA KWA NAFASI YA MKAGUZI MSAIDIZI WA UHAMIAJI
Baadhi ya Vyombo vya Habari leo tarehe 29 Julai, 2014 vimeandika kwa makosa kuwa ajira za Uhamiaji zilizositishwa jana zinahusiana na 70 zilizopatikana baada ya usaili uliofanyika katika Uwanja wa Taifa.
Ukweli ni kuwa usaili wa nafasi ya Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji ambao awali ulianzia Uwanja wa Taifa ulienda vizuri hadi wakapatikana wasailiwa wa kujaza nafasi 70 za Mkaguzi Msaidizi wa
Uhamiaji. Zoezi hilo halikuwa na matatizo yoyote, na waliochaguliwa walitakiwa kuripoti kazini tarehe 29 Julai lakini kwa sababu ya Sikukuu sasa wataripoti baada ya sikukuu.
Hivyo tunapenda kufafanua kuwa wasailiwa waliochaguliwa kujaza nafasi 70 za Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji hawahusiki na usitishwaji uliotangazwa jana na wanatakiwa kuendelea na mipango ya kuripoti kazini kama ilivyotangazwa hapo awali.
Wasailiwa wanaohusika na kusitishwa kwa ajira zao ni wale waliokuwa wameshiriki katika zoezi la kuajiri Konstebo na Koplo wa Uhamiaji ambao idadi yao ni 200, ambao walitakiwa kuripoti tarehe 06 Agosti, 2014 lakini kwa sasa hawa ndio wanaelekezwa wasubiri hadi hapo watakapopewa maelekezo mengine.
Sgn
Isaac J. Nantanga
MSEMAJI WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
29 JULAI, 2014
Taarifa ya jana ilisomeka hivi:
KUSITISHWA KWA AJIRA ZA KONSTEBO NA KOPLO WA UHAMIAJI
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Mbarak Abdulwakil amesitisha zoezi la ajira za Konstebo na Koplo wa Uhamiaji zilizotangazwa katika vyombo mbalimbali vya habari hivi karibuni na Idara ya Uhamiaji.
Hatua hiyo imechukuliwa kutokana na tuhuma zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya Kijamii kuwa kulikuwa na upendeleo kwa ndugu na jamaa za watumishi wa Idara hiyo.
Kufuatia hatua hiyo, Bwana Abdulwakil ameunda Kamati Ndogo ya Uchunguzi itakayochunguza kuhusu tuhuma hizo.
Kutokana na kusitishwa kwa zoezi hili waombaji wote walioitwa na kutakiwa kuripoti Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji tarehe 06 Agosti, 2014 sasa wanatakiwa kusubiri hadi hapo watakapotangaziwa tena baada ya uchunguzi huu kukamilika na maamuzi kufanyika.
Imetolewa na:
Sgn
Isaac J. Nantanga
MSEMAJI WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
28 Julai, 2014
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment