Thursday, 31 July 2014

[wanabidii] Re: URAIS 2015-MATATIZO YA BERNARD K. MEMBE

Nimeleta topic hii ili kwa pamoja pia tujadili matatizo ya mtu mwingine anayetajwa sana kuwa anaweza kuibuka kidedea katika kinyanganyiro cha urais CCM. Kwa mtazamo wangu Membe kwa haya yafuatayo sioni kama anafaa kuwa raisi wa Tz:

(a) Kwanza haaminiki: Ili mtu aweze kuaminika na jamii kubwa ya watazania ni lazima ajulikane undani wake na ikibidi madhaifu yake na strengths zake.Lakini Membe anaonekana yupo yupo tu na huku kwa nguvu zote akijitahidi kujificha asili yake, na hiki watu makini hatuwezi kumuamini haswa kwa dhamana ya nafasi kubwa kama uraisi. Binafsi siamini hata kidogo kama Membe anaweza kukemea chochote na kufanya chochote kwa maslahi ya nchi na haswa kitu kinachohusu kuwa na maamuzi magumu na yenye tija.

(b) Sio safi. Watu wengi wanadhani Membe ni mtu safi. Lakini, ukweli ni kuwa Membe si safi hata kidogo. Ni huyuhuyu ndiye aliyesema Tanzania inaweza kupokea hela kutoka kokote na kwa masharti yeyote hata kama anayetupatia fedha hizo ni shetani. Uraisi ni suala la values na misimamo. Kama mcha Mungu wa kweli ni lazima kuna mambo fulani mtu utakuwa nayo au basi kukupa hofu kiasi fulani. Sipendezwi na mtu ambaye anaweza fanya chochote ali mradi tu, afanikiwe katika mambo yake.Kwa lugha nyingine Raisi ajae hapaswi kuwa msani msanii kama Membe.

(c) Hana maamuzi magumu: Nchi kwa jinsi ilivyo na inavyoenda kwa sasa inatakiwa mtu mwenye uwezo wa kuleta displine katika system. Eti Tanzania nayo ina ugaidi wa ndani, huu ni udhaifu wa kimfumo kutokana viongozi wakuu kufumbia macho baadhi ya mambo kwa maslahi binafsi. Kwa tunakotaka kwenda Membe ni dhaifu sana na hawezi kukemea chochote na haswa akijua kundi fulani litampa kura,basi kundi hilo laweza fanya chochote na asifanye kitu. Hebu angalieni watu wanaompigia debe Membe, RidhiOne, Kigangwala,nk, wote ni wasanii sanii tu ambao bado hawajatoshea katika kusimika misngi ya kiinchi labda huko baadae.

(d) Hana historia. Kiukweli kabisa mpaka hapa tulipo nchi imepitia mambo mengi. Binafsi huwa sipendi mtu kuibukia kona fulani na kutangaza nia ya kuutaka uraisi kwa kisingizio unakerwa na kero za watanzania,lkn hata wakati mmoja hujawahi kuwa suluhisho la kero hizo na ni kiongozi. Membe hapo alipo ni kudra tu za familia ya JK na ndio hao wanataka kuendelea kutuongoza tena kwa mgongo wa Membe,nafikiri watanzania tunayo haki ya kuchagua mwingine tunayedhani ana uwezo wa kutusaidia. na mengine mengiiiiiiii...NGUPULA.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment