Vuguvugu la uchaguzi wa serikali za mitaa limepamba moto huku vyama vikubwa viwili ambavyo ni mahasimu wa kisiasa(CCM + CDM) wakipambana vilivyo.Kila chama kinajaribu kusimamia utamaduni wake katika kujijenga na kuziba nyufa ambazo zinaonekana kama kikwazo kwa nyumba hizo.
Tabia na mienendo ya wanachama wa vyama hivi kidogo zinaendana kutokana ama na sifa ambazo wamezipata ndani ya chama na kitaifa(wananchi) na kuwafanya wakati mwingine wabweteke au ulimbukeni wa kukubalika kw wananchi.
Changamoto kubwa ndani ya vyama hivi ni aina ya uendeshaji demokrasia katika kusimamia misingi imara ya utawala bora ndani ya vyama vyao.Pamoja na kutofautiana kimtazamo ,kiitikadi na mirengo ya vyama hivi,vyama hivi vimekuwa vikilea mamluki wa kisiasa ambao wanakosa sifa ya kuwa wanachama wa vyama vyao.
CCM kina umri mrefu sana kuliko vyama vingine na ni miongoni mwa vyama vikongwe duniani.Kinakumbana na changamoto nyingi na kubwa ambazo wakati mwingine hazistahili kuvumiliwa kwa mustakabali wa chama na serikali yake.Ndicho chama kilichoshika dola ambacho kina vyanzo vingi vya taarifa juu ya tabia na mienendo ya wanachama wake,lakini pia ni chama ambacho kwa makusudi kimeamua kuacha itikadi yake ya kijamaa na kuimba kibepari kiasi cha kuharibu ladha nzima ya mfumo wake iliouendesha tangu kuasisiwa kwa chama hiki.Changamoto kubwa ambayo inakisakama chama hiki ni kukosa uthubutu wa kufanya maamuzi magumu hata kama mambo hayo yanayotakiwa kufanyiwa uamuzi yanatishia uhai wa chama,matokeo ya udhaifu huo yamepelekea kuibua wimbi kubwa la ufisadi ambalo linaonekana kuwa ndiyo sera ya chama,huku vyombo vya maamuzi ya kichama vikipiga chenga na kutofautiana misimamo toka sehemu moja hadi nyingine.
Hali hii inakigharimu sana chama hiki kiasi cha kutokuaminika kwa wananchi na kuchukuliwa kuwa samaki mmoja kwenye tenga akioza hakuna hata mmoja atakayesalimika,wote watakuwa wameoza.Hali hii ndani ya CCM inatafsiriwa kama siasa za kuvumiliana ilihali kwenye mashina wanachama wanyonge ndiyo wanaowajibishwa.
CDM ni chama kikuu cha upinzani nchini chenye umri wa miaka 22 toka kuasisiwa kwake,mfumo wa itikadi yake ni cha cha mrengo wa kati,kuna changamoto ambazo zinakikumba chama hiki ambacho kimeonekana kama pambazuko jipya kwa wananchi.
Yaliyokikumba CCM ndani ya chama chao ni sawa na matatizo ya CDM katika uendeshaji wa siasa za uwazi na ukweli.Wanacho tofautiana ni mtazamo na uthubutu wa kufanya maamuzi ambayo wakati mwingine lazima uwe jasiri kweli.CDM wameweza zaidi ya mara nne pamoja na kuwa hakina umri mrefu kama wa CCM,waliweza kumvua umakamu mwenyekiti marehemu Chacha Wangwe,waliweza kumfukuza Dr. Amani Warid Kabouru ambaye kwasasa ni M/Kiti wa CCM mkoa wa Kigoma,waliweza kuwafukuza uanachama mdiwani watano wa Arusha na madiwani wa tatu wa Mwanza na kumsimamisha naibu katibu mkuu na kuwafukuza wenzake wawili,Mwigamba na Dr. Mkumbo kutokana na utovu wa nidhamu na mipango yao ya kukivuruga chama.
Kutokana na uwazi na uchambuzi mdogo wa nilioufanya kuna changamoto nyingi ambazo vyama hivi vinatakiwa kuzifanyia kazi japokuwa kiutendaji CCM ndiyo yenye kukusanya kodi na kutekeleza kile walichohiahidi lakini CDM wanabidi kubadilika na kuwaonyesha njia wananchi kwa kuzindua shughuli za uchumi shirikishi ambazo kwa njia moja ama nyingine zinaweza kunyanyua hali za wanyonge wa nchi hii.
Vyama hivi vijilikite kwenye mikakati ya kutoa elimu itakayowawezesha wananchi wajue wataifanyia nini Tanzania kabla Tanzania haijawafanyia,maana haki siku zote huendana na wajibu.Pia uwazi na ukweli uwe chachu ya uwajibikaji katika kufikia malengo kusudiwa ili kujenga taifa lenye nidhamu na maadili kwa watu wake.
-- Tabia na mienendo ya wanachama wa vyama hivi kidogo zinaendana kutokana ama na sifa ambazo wamezipata ndani ya chama na kitaifa(wananchi) na kuwafanya wakati mwingine wabweteke au ulimbukeni wa kukubalika kw wananchi.

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment