Friday 28 February 2014

Re: [wanabidii] HAKI ZA BINADAMU KWA JAMII NDOGO KAMA MASHOGA

we unayetetea haki za mashoga kaungane nao wewe mfanye ushoga, usituletee mambo ya kipuuzi katika katiba mpya.
Bob Leo.


On Tuesday, February 25, 2014 4:08 PM, Yona Maro <oldmoshi@gmail.com> wrote:
HAKI ZA BINADAMU KWA JAMII NDOGO KAMA MASHOGA

Ndugu zangu ,

Nimeona nisikae kimya , nisiwe mnafiki na nisimamie kile ninachosimamia siku zote , suala la haki za binadamu kwa raia wote bila kujali mapungufu au matatizo yoyote aliyokuwa nayo .

Kabla sijaanza kuandika ujumbe huu nimesikitishwa na kiongozi mmoja akiandika kwenye ukurasa wa kijamii kufurahia kitendo cha Rais wa Uganda Kusaini GAY BILL kwa kufuata mkumbo tu bila kujua hawa ni miongoni mwa wapiga kura wake .

Tukirudi kwenye suala la jamii za watu wenye jinsia moja yaani mashoga kwa upande wa wanaume na wasagaji kwa wanawake , kuna mambo kadhaa inabidi jamii ijue nitaweza wazi kwa ufupi .

Katika katiba mpya haki zao zitakuwa kwenye kipengele cha jamii ndogo ndogo .

1 – Ndani ya jamii hizi kumekuwa na magonjwa mbalimbali , kutokana na hawa watu kutokujulikana waziwazi wamekuwa wanajificha ndani hata mahospitali hawaendi hata watoa huduma hawawafikii matokeo yake ni kuathirika zaidi na kupoteza watu wengi zaidi .

2 – kuna wale washauri nasaha na wengine watoaji wa huduma za afya haswa zinazohusiana na ugonjwa wa ukimwi , wamekuwa wanapata tabu kumaliza gonjwa hili na mengine yanayohusiana na hili kutokana na kutokuwa wazi .

3 – Kuna ushahidi wa wazi wa vitendo vya mahusiano ya jinsia moja haswa katika nyumba za ibada au kwenye huduma za ibada na taasisi za kidini haswa kwa watu wazima na watoto wadogo wanaopelekwa kujifunza na matokeo yake ni kuificha jamii hii ambayo imelelewa na kufichwa kwenye nyumba za ibada .

4 – Kwenye katiba mpya inayokuja kinachopiganiwa ni haki ya jamii ndogo ndogo kama hizi za Mashoga , wasagaji , Hadzabe na nyingine nyingi zilizopo nchini ambazo rais ameapa kuzilinda na kuzitetea bila ubaguzi wowote .

5 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mhe Jakaya Mrisho Kikwete alichaguliwa na watu mbalimbali na aliapa kulinda watu wote na kuongoza nchi hii wakiwemo hawa ambao sasa hivi wanatengwa na kuonekana si mali kitu na si chochote  .

Kwa kumalizia napenda kusema na kusisitiza tena , Kwamba hii ni  nchi yetu wote , basi haki za wote ziheshimiwe bila kuingilia mambo ya faragha ya watu wengine , sasa tuko kwenye mchakato wa katiba mpya hili suala liangaliwe na tunakaribia uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 natumai viongozi wetu watatumia hekima katika kuangalia na kusimamia haki za jamii ndogo ndogo .


--

Yona Fares Maro

Institut d'études de sécurité - SA


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.


0 comments:

Post a Comment