Wednesday, 26 February 2014

Re: [wanabidii] Re: [Mabadiliko] Bunge La Katiba; Kila Mbunge Ana Dakika Moja Na Nusu Tu Ya Kuongea Katika Siku 90..!

Kuna uwezekano kuwa bunge hili ni mock. baada ya uchaguzi 2015 mchakato sahihi ambamo bunge la katiba litachaguliwa rasmi utaanza. natarajia kuwa wakati huo wabunge waliopo hawataruhusiwa kugombea ubunge wa bunge la katiba. hata wakiruhusiwa wataangushwa. huenda hii ikawa agenda wakati wa uchaguzi 2015. Naanza kuishiwa na imani kuwa watanzania tutapata katiba mpya. Huenda wanasiasa wakapata lakini si watanzania.



On Wednesday, February 26, 2014 6:28 PM, lesian mollel <aramakurias@yahoo.com> wrote:
laki 3 for one minute input kweli daaah....si bora wasingepeleka...sana sana kina mtikila ndio wataongea na kuvunja mike.......daaah


On Wednesday, February 26, 2014 1:48 AM, Abdul Dello <abduldello@gmail.com> wrote:
Zinawatosha hizo kwa kusimama, kushukuru raisi kwa kumteua, na kuunga mkono hoja


2014-02-26 12:36 GMT+03:00 Maggid Mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com>:


Ndugu zangu,

Kwa Wabunge wetu wateule Bunge la Katiba kuendelea kupoteza muda kujadili posho na kanuni ambazo hazijakaa sawa mpaka sasa ni kuzidi kupoteza muda kwa kazi ambayo wananchi tulitarajia waende wakaifanye kule Dodoma; kujadili na kupitisha rasimu ya pili ya Katiba yenye kutokana na mawazo ya Wananchi.

Sijui kama kuna Wabunge wengi wateule wenye kujua, kuwa hata kama watakaa Dodoma kwa siku 90, bado, kwa hesabu za Kisayansi, hiyo ina maana ya dakika 54,000. Ukizigawa hizo kwa wajumbe 600 tu, unapata wastani wa dakika moja na nusu kwa siku ya kuongea kwa kila mjumbe. Ni kwa siku 90 na kwa kuchukulia kuwa watafanya kazi kwa saa kumi kwa siku, kuanzia Jumatatu mpaka Jumapili.

Hivyo, kwa hesabu hizo, nauona ukweli, kuwa hata hizo siku 90 hazitawatosha wajumbe wa Baraza la Katiba, endapo, sura ya hali itakavyokuwa Bungeni itakuwa kama inavyoonekana sasa. Hali ya mivutano na hasa kama Bunge hilo litaamua kufanya kazi ya kubadili vifungu vya rasimu hiyo na hata kuweka vipya.

Maana, kutahitajika mjadala mrefu. Na mjadala huo utatoka hata nje ya Bunge, kwa maana, wananchi nao watakuwa wakijadili kupitia vyombo vya habari na kuathiri upepo wa majadiliano ndani ya Bunge. Hivyo basi, kutakuwa na hali ya kuahirishwa vikao mara kwa mara na siku pia kuongezeka.

Nahofia pia, kuwa Wabunge wazoefu kwenye kuzungumza ndio watakaozungumza, na hivyo basi, watakuwa wamekula muda wa wenzao. Na matokeo yake, ni ukweli kuwa, kuna wabunge walioko Dodoma sasa, watakaozimaliza siku 90 kwa kuishia kupiga kura tu, na si kujadili Katiba wakasikika na kuonekana na waliowatuma kwenda Dodoma.

Naam, tutayaepusha haya, ambayo kimsingi ni aibu kwa taifa, kama tutatanguliza hekima na busara na zaidi kwa kutanguliza maslahi ya umma, na si ya binafsi, makundi au vyama vya siasa.
Maggid Mjengwa,
Iringa.
0754 678 252
http://mjengwablog.com
--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
MUHIMU KWA WANACHAMA WOTE: Jukwaa hili litafungwa hivi karibuni hivyo hii ni taarifa ya Mwisho kwako kuhakikisha unajisajili www.mabadiliko.com
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.


0 comments:

Post a Comment