Tuesday, 4 February 2014

[wanabidii] WIZARA YA FEDHA YAKANA KUIDHIBISHA KIINUA MGONGO CHA MIL 160 KWA WABUNGE

WIZARA YA FEDHA TANGAZO KWA UMMA

Katika siku za hivi karibuni, baadhi ya magazeti yamekuwa yakitoa taarifa za upotoshaji juu ya suala la kuongezeka kwa malipo ya pensheni kwa Waheshimiwa Wabunge.

Magazeti hayo yanadai kwamba Mheshimiwa Waziri wa Fedha amethibitisha ongezeko hili. Taarifa hizo ziliendelea kudai kwamba Waheshimiwa Wabunge watakapostaafu watastahili kulipwa shilingi 160 milioni kila mmoja.

Kwa kupitia tangazo hili, tunaeleza kwamba, Mheshimiwa Waziri wa Fedha hajawahi kuongea na Mwandishi wa Habari yeyote kuhusu suala la nyongeza ya pensheni ya Waheshimiwa Wabunge na maelezo kwamba Mheshimiwa Waziri alithibitisha taarifa za ongezeko hilo sio kweli bali ni maelezo binafsi ya Waandishi wa Habari hizo na suala hilo halipo Serikalini wala Bungeni.

Aidha, tunapenda kuwaasa Waandishi wa Habari kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya taaluma yao na kuacha kuwachonganisha Wabunge na Wananchi wanaowaongoza kwa kuwapotosha kwa masuala ambayo hayana ukweli na uthibitisho wowote.

KATIBU MKUU – WIZARA YA FEDHA
5 FEBRUARI, 2014

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment