Bundi ashutumiwa kwa kukwapua soksi na viatu vya jirani,
Askari wa kulinda wanyama wamtetea Bundi ! Kamanda adai Bundi wake aliokota viatu sio mdokozi !
Ughaibuni,
Wiki endi haikuwa nzuri katika makao ya mkuu wa FFU Ughaibuni kamanda Ras Makunja,
baada ya mmoja ya majirani kulalamika kuwa ndege aina ya Bundi anayefugwa katika
jengo (Anunnaki Empire) analoishi mwanamuziki kamanda Ras Makunja kiongozi wa Ngoma Africa band kule ujerumani,
Bundi huyo sasa amekuwa na tabia za ukwapuzi, jumamosi
iliyopita alishutumiwa kuiba viatu na jozi ya soksi za jirani , jirani anadai kuwa Bundi huyo
aliruka hadi kwenye bustani ya jiarani na kukuta viatu vya kuchezea mpira vilikuwa vimesauliwa nje na kuruka navyo ! kitu amabcho si cha kawaida jiarani alidai ndani ya viatu pia kulikuwa na soksi vyote hivyo vilikutwa juu ya paa la Bundi huyo baada ya Askari wa kikosi maalumu cha kuangalia wanyama kumfatilia Bundi huyo aliyepewa jina la Udi Udi.
Jirani alillamikia kuwa huyu Bundi siku hizi ni mkwapuzi kwa nini ? asihamishwe arudishwe Zoo, Cha kushangaza shutuma za jirani zilitupiliwa mbali na maaskari hao na badala yake jirani kapewa Onyo kwa kuambiwa asijaribu kumrushia hata jiwe Bundi huyo,askari wamesema Bundi wa kamanda anarusiwa kuwa huru majira ya jioni kwa ajili ya kuruka kupunguza uzito na kupata hewa mwanana.
Jirani huyo alibaki mdomo wazi na kushikwa na mshangao kwa kuambiwa kuwa Bundi hakuiba
viatu Bali aliokota,na akamua kuvipereka juu ya banda lake,kwa kuwa mmiliki wa Bundi huyo ni
jirani mwema lazima viatu angevurudishwa kwa mwenyewe au kuvupereka ofisi maalumu ya vitu vya kuokota (Fondbureu).
Jirani haelewi pale wanausalaa hao wa wanyama walipomwabia ole wake kama Bundi huyo akikutwa na jeraha.
Mmliki wa dege hilo la kutisha baba mtukutu kamanda mkuu Ras Makunja wa FFU,hakuwa a mengi ya kusema
Bali alimuomba msamaha jirani huyo kwa kumwambia ondoa shaka huyu
Bundi sio mkorofi bali ni rafiki wa kila mmoja, jirani aliambiwa na kamanda kuwa ajaribu
kuomba kibali cha kufuga mwewe au kunguru kwani ni ndege wazuri tuu kamanda aliongeza ndogo kwa jirani huyo.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment