Tuesday, 29 October 2013

[wanabidii] Table manner

Somo la namna ya kukaa mezani na kula ni ni somo muhimu sana, lakini halifundishwi mashuleni. Pengine watu wanategemea kufundishwa majumbani mwao. Lakini ni familia ngapi wanapokula hukaa mezani? Familia nyingi chakula huwekwa chini na watu hukaa mduara na kula kwa mikoni. Hii ni jadi ya makabila mengi. Ni tendo jema tena la umoja.

Lakini dunia ya leo ni lazima kujifunza zaidi ya hapo. Hasa wanaobahatika kwenda nje ya nchi. Utamaduni huu haupo kabisa. Kwa kawaida chuoni, meza huandaliwa. Huwekwa sahani mbalimbali. Labda ya supu, chakula chenyewe, salad na mlo baada ya mlo. Zaidi ya hayo, huwekwa kijiko cha supu, umma na kisu, na vijiko vya saizi mbalimbali. Pia huwekwa glass. Kuna glass ya wine nyekundu au nyeupe, glass ya maji nk.

Nimeona wanafunzi wetu hasa wanaomaliza high schools na ambao hawajawahi kukaa mezani na kula, wakienda ngambo huwa vituko. Naona kama ilivyo umuhimu wa kufundisha katiba ya nchi na mambo ya ukimwi kwa watoto wetu, pia namna ya kukaa mezani na kula ni vyema somo hili liwepo pia. Ni ustaarabu wa siku hizi. Si vyema kudharau kila kitu. 
kessy

0 comments:

Post a Comment