Thursday, 31 October 2013

Re: [wanabidii] CCM ILIIMARIKA ZAIDI KWA NYERERE KUNGATUKA

Watu wengine bwana? Nani ameenda Chadema akanyimwa taarifa za kalenda/ratiba ya uchaguzi? Ni mwanachama yupi hajui kinachoendelea ndani ya chama hicho? Kama Mbowe akitaka kuendelea kugombea anazuiwa na nani?  Je, ni hoja ipi ya maana na ya msingi gani wanaopiga chapuo Mbowe asigombee? Je, amefeli kama Mwenyekiti wa Chadema, Je, wanachama wamemchoka? ni nini tatizo?
Kuna hoja rojo kweli humu jukwaani, eti woga ni wa nini akiondoka Mbowe Chadema itakufa? Kwa nini wanahoji swali la kizushi? Kwani kama akiendelea kubaki Chadema itakufa? kama wanaohoji hili wana uchungu basi ukweli ni huo kuondoka na kubaki kupi kuna faida? mwenye jibu aseme. 
Nani alikuwa anaizungumzia Chadema kabla ya 2005; kilionekana kama chama kisichokuwa na madhara kisiasa kwa watawala, sasa kimekuwa, ndiyo maana hata fikra za kutaka kuwapangia viongozi wa kukiongoza zinaanza kuibuliwa. Hamkumbuki kilichotokea Bavicha? Wamekataa kuuziwa tena mbuzi ndani ya gunia!

Mwisho nikumbushe kuwa CCM hakujawahi kuwa na uchaguzi, kuna utaratibu wa hitifaki. kura kwa mujibu wa cheo. Rejea uchaguzi wa 2002. Kura za hitifaki. Kura nyingi zaidi ni kulingana na cheo ndani ya serikali. Mwenye kutaka kubishia hili amuulize mkuu wa kaya walipigwa zengwe gani wakati huo. Kina Sumaye waling'aa vibaya mno, Kina Mangula wa sasa akiwa Katibu Mkuu, kina makamu wa rais, hizi zilikuwa zama za mzee wa ukweli na uwazi. Mmesahau mara hii kuwa kura zinapangwa na ile idara nyeti. Mnataka kuleta za kuleta kuhusu kuachia uongozi wa chama hivi hivi bila mikakati, bila kujiandaa?

Ukisikia adui yako mkuu akikushauri jambo huku akionyesha ni kwa nia njema na huruma, kimbia, tena kimbia sana maana anakuwinda. Rejeeni maandiko matakatifu ya Biblia juu ya Samson na Delila
.

2013/10/29 Yona Maro <oldmoshi@gmail.com>
Ukimwona nyerere na uzuri wake wote aliacha nafasi ya mwenyekiti wa CCM , Mwinyi pia aliacha nafasi hiyo , Karume kule zanzibar aliacha , kikwete nae muda wake unayoyoma na ndio maana ya uongozi - sasa wengine wakiulizwa kuhusu kuacha vijiti wenzao wanakuwa mbogo , tukubali kwamba mabadiliko yanaanzia ndani mwetu haswa ndani ya vyama .

Kwa miaka zaidi ya 20 toka kuanzishwa kwa vyama vingi tumeona ndani ya CCM vikao vikifanyika watu wanabadilishana uongozi wanatoka hawa wanaingia hawa kwanini hili linashindikana ndani ya vyama vya upinzani ambavyo vina mpango wa kuchukuwa madaraka ya kuongoza taifa ?

Mwalimu nyerere alingatuka toka CCM akafuatia mwinyi nae akamwachia mkapa kwenye uchaguzi wa vyama vingi lakini chama hakijawahi kufa na hakijawahi kuogopa kufanya mabadiliko ndani ya chama 

--
Find Jobs in Africa Jobs in Africa
International Job Opportunities International Job Opportunities
Jobs in Kenya Jobs in Kenya

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment