Friday, 23 August 2013

[wanabidii] Vyombo vya habari Tanzania vyashindwa kukabili propaganda za Malawi na Rwanda

Wanyarwanda wamekuwa wazuri katika siku za hivi karibuni kwenye anga la habari za kipropaganda na kuwazidi ndugu zetu Wakenya ambao kwa mda mrefu wamekuwa wakiongoza wa ukanda huu wa Afrika ya Mashariki.

Kwanza ifahamike kuwa PROPAGANDA za aina yoyote ile ni msingi wa taifa linalokuwa nakujitambua.

Tulipoingia kwenye vita vya Kagera kati yetu na Uganda, vyombo vya habari wakati huo vilikuwa vichache sana, tulikuwa na "Radio Tanzania" na magazeti machache ya serikali na chama tu.

Lakini ufanisi wavyo katika propaganda ile ya kivita hakika vilitawala nyoyo za Watanzania nakutufanya sote tujione tupo katika jando la taifa huru.

Leo hii tupo kwenye mgogoro wa kidiplomasia na nchi mbili yani Malawi na Rwanda, vyombo vyetu vya habari vimejiweka kando kabisa na masuala haya ukilinganisha na propaganda za wenzetu.

Mfano, nchini Malawi gazeti la NyasaTimes na mtandao wa intaneti wa gazeti hilo limekuwa ni chombo
muhimu kwa Wamalawi na dunia kwa ujumla kuuelezea kwa ufasaha mgogoro wa Ziwa Nyasa na kuhanikiza kuwa ziwa lote ni lao.

Vivyo hivyo tulipoingia kwenye mgogoro wa kidiplomasia na nchi ya Rwanda vyombo vyao vya habari kama gazeti lao maarufu la NewTimes Rwanda na mitandao maarufu ya intaneti kama www.umuvugizi.com nk vimekuwa vyombo muhimu vya propaganda kwa Rwanda dhidi ya Tanzania.

Mfano wa kwanza ni agizo la Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania la kuwaondoa wahamia HARAMU nchini, vyombo hivyo vya Rwanda vimegeuza kauli na kusema rais alitoa amri Wanyarwanda wote WAFUKUZWE jambo ambolo sio kweli.

Pili ni taarifa za vyombo hivyo vya Rwanda kusema Mke wa Rais Mama Salma ni Mhutu.

Taarifa hii imelistua taifa na kuilazimu serikali kujibu tena kwa utulivu wa hali ya juu.

Binafsi nimesikitishwa sana kuona serikali inaamua kujibu taarifa hii ambayo kimsingi ilistahili kujibiwa kiplopaganda hivyohivyo na vyombo vyetu vya habari kwakuwa taarifa hii sio "ngeni" kabisa.

Kwa wale wasiojua nikuwa asili ya habari hii ya "Uhutu" wa mke wa rais wa Tanzania ni siasa za majita za 2005.

Mtandao wa kijasu wa Wikileaks uliitoa habari hii tangu 2005 wakati wa harakati za uchaguzi wa Urais nchini Tanzania, ni Wanachama wa Chama cha Mapinduzi ndio waliopeleka habari hii huko Wikileaks kupitia kambi zao za Uraia hasa kambi iliyokuwa ikiongozwa na Mwandosya.

Sasa vyombo vetu kwakuwa vimezoea propaganda za ndani yani za CHADEMA na CCM hivyo viliona kama habari ile ni mpya na yakustua sana havikujua hata cha kujibu.

Unaweza kujiuliza sana, hivi uimara wa vyombo vyetu katika anga za kimataifa upo wapi?

Je, Taifa leo likiingia vitani ipi nafasi ya vyombo vyetu katika anga za kimataifa?

Katika propaganda za kiuchumi kimataifa huko ndio kabisaaaa hatuhitaji hata kuhoji kwakuwa vipo gizani kabisa.


Source: http://www.wavuti.com/4/post/2013/08/yericko-nyerere-vyombo-vya-habari-tanzania-vyashindwa-kukabili-propaganda-za-rwanda-malawi.html#ixzz2coFziUKL

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment