Wanajitesa wenyewe, ni kama unataka kwenda Dodoma toka Dar unaamua kupitia Iringa, badala ya shortcut, inakuwa longcut!
From: ezekiel kunyaranyara <ekunyaranyara@yahoo.co.uk>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Friday, August 23, 2013 6:33 AM
Subject: Re: [wanabidii] RWANDA NA UGANDA ZAJITOA BANDARI YA DAR ZAHAMIA BANDARI YA MOMBASA
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Friday, August 23, 2013 6:33 AM
Subject: Re: [wanabidii] RWANDA NA UGANDA ZAJITOA BANDARI YA DAR ZAHAMIA BANDARI YA MOMBASA
Nafikiri hapa ndipo kuna changamoto kubwa ya kufanyia kazi. Sent from Yahoo! Mail on Android |
From: Mike Zunzu <mikezunzu@yahoo.co.uk>; To: wanabidii@googlegroups.com <wanabidii@googlegroups.com>; Subject: Re: [wanabidii] RWANDA NA UGANDA ZAJITOA BANDARI YA DAR ZAHAMIA BANDARI YA MOMBASA Sent: Thu, Aug 22, 2013 7:26:25 PM
"Tukitazama upande wa pili viongozi hawa K3 ni watuhumiwa wote , Kagame na Museveni ni watuhumiwa wakubwa wa vita inayoendelea mashariki ya kongo wakati kenyatta anatuhumiwa na ICC ,Kagame na Museveni wameingia madarakani kwa njia ya mtutu na wameendelea kukaa hapo kubinya uhuru wa kujieleza na wanatuhumiwa kupoteza wapinzani wao kadhaa" Huo ni mtizamo wako, je viongozi wa Tanzania wanawaza hivyo pia? Mara ngapi kumependekezwa kuboresha huduma za bandari za Tanzania ili kuvutia wateja wa nchi jirani zisizo na bandari. Viongozi wetu wako busy na maandalizi ya urais wa 2015, wanacho kifanya, miradi ya maendeleo inafanywa kama ni mali ya mtu, mradi Fulani unaotakiwa uanze kutekelezwa leo unaweza kusimamishwa makusudi mazima ili kungonjea karibu na kampeni za kuwania urais kuanza ndipo mradi huo pia ukamliwa sasa unawewza ukaanza kutekelezwa, au harakati za kuanza, na kasha tu baada ya shughuli hiyo kwisha mradi huo unashia hapo, mingine hata hushia njiana na kusahaulika au mingine hufufuliwa kila shughuli hizo zinapoanza. Tanzania tu wasemaji wazuri, hasa watu tusiokuwa na hata na nafasi ya ya kusema hiki kifanyike, utaona nchi za wenzetu wanafanya miradi hiyo ya pamoja, kama wataitekeleza kama inavyodhani kuwa watakuwa wamesonga hatua kadhaa mbele, mambo ya kusema nani mtuhumiwa, nani aliingia madarakani kivipi haina maana, kama hao walioingia madarakani kwa kuchakachua au kihalali lakini wakawa hawafanyi chochote cha manufaa kwa nchi, haina maana yoyote. From: Yona Maro <oldmoshi@gmail.com> To: wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> Sent: Thursday, 22 August 2013, 18:03 Subject: Re: [wanabidii] RWANDA NA UGANDA ZAJITOA BANDARI YA DAR ZAHAMIA BANDARI YA MOMBASA Mwezi huu au ujao wanatarajia kusaini mkataba wa kujenga reli kutoka Mombasa kisumu kwenda uganda na kuunganisha kilometa 500 mpaka kigali , pia kuna mradi wa bomba la mafuta toka mombasa kampala , kigali na juba sudani ya kusini pengine hizi ndizo fursa wanazokimbilia , miradi yote hiyo ilibuniwa na K3 yaani Kagame , Kaguta na Kenyatta sijui kama inahusiana na jumuiya ya afrika mashariki au ni mipango binafsi kati ya mataifa hayo matatu . Tukitazama upande wa pili viongozi hawa K3 ni watuhumiwa wote , Kagame na Museveni ni watuhumiwa wakubwa wa vita inayoendelea mashariki ya kongo wakati kenyatta anatuhumiwa na ICC ,Kagame na Museveni wameingia madarakani kwa njia ya mtutu na wameendelea kukaa hapo kubinya uhuru wa kujieleza na wanatuhumiwa kupoteza wapinzani wao kadhaa . Upande wa Tatu ni jinsi Uganda inavyotamani Bandari ya Tanga ambapo kuliwahi kuwa na mradi wa reli kati ya tanga kwenda mara mpaka huko uganda , tukumbuke pia IDDI AMIN alipovamia sehemu ya tanzania huko kagera maslahi yake mengi zaidi yalikuwa ni kwenye ukanda huu wa bandari ya tanga - Mara - Kampala . Tusitishike na hawa , tunaweza kuendeleza TAZARA kupitia zambia tutaweza kuunganisha mpaka mji mkuu wa kongo na miji mingine mpaka goma na kivu lakini mpaka waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Uganda na Rwanda waondoshwe pawe salama zaidi kwa biashara na hilo linawezekana . Mwisho kitu kisichosemwa sana kuhusu hawa K3 ni biashara Haramu ya madini ambayo imenyanyua uchumi wa Rwanda , Uganda na Kenya , Tanzania tunaibiwa sana madini yanayouzwa kwenye soko la kenya kwa njia haramu , kongo inaibiwa sana madini yenye soko bandia uganda , rwanda na Kiongozi wao Kenya . 2013/8/22 John George <georgejn2000@gmail.com> Helo all, suala hapa hatuzungumzii east africa Community tunazungumzia Find Jobs in Africa Jobs in Africa International Job Opportunities International Job Opportunities Jobs in Kenya Jobs in Kenya |
0 comments:
Post a Comment