Friday, 23 August 2013

Re: [wanabidii] RWANDA NA UGANDA ZAJITOA BANDARI YA DAR ZAHAMIA BANDARI YA MOMBASA

Mkutano uliofanyika kati ya nchi tatu Kenya,Uganda na Rwanda umelenga kuzibagua Tanzania na Burundi kwani nchi hizo zinaonekana kuwa kikwazo katika kuharakisha mtangamano wa kina zaidi (deep integration) hata kufikia Political Federation ambayo ni ngazi ya juu zaidi ktk mtangamano. Hata hivyo kikwazo kikubwa cha mtangamano kinaonekana kuwa Tanzania kwakuwa Burundi si nchi yenye rasilimali na fursa nyingi za kibiashara hivyo imekuwa tu ikikubaliana na Tanzania katika midahalo ya EAC kwa sababu mbalimbali zikiwemo za kihistoria. Hata hivyo muungano wa nchi hizo tatu (tri-lateral) umesemekana kuivuta Burundi kwa karibu na hivi karibuni itaungana nao nakuicha Tanzania peke yake.Hata hivyo nikinyume cha mkataba wa Jumuhia ya Africa Mashari (East Africa Treaty) kwa nchi wanachama kubagua baadhi ya washirika na kujianzishia utaratibu wao.

Ukichunguza mkutano wanchi hizo tatu uliofanyika majuma kadhaa yakiyopita,waligawana majukumu katika kutekeleza mkakati wakuongeza kina cha mtangamano baina yao, Kagame alipewa kusimamia swala la kuandaa vitambulisho vya pamoja ikiwa ni pamoja na swala la visa za watalii, Museveni alipewa jukumu lakusimamia uharakishaji wa Sarafu ya pamoja ( Common Currency/ Monetary Union) na baadae umoja wa kisiasa yaani Political federation wakati Kenyatta alipewa jukumu lakusimamia Reli yakutoka Mombasa hadi Kigali.Mambo haya yamekwisha anza kushughulikiwa kulingana na mgao huo wa majukumu. Kenya wameanzisha tozo ya asilimia 1.5 (1.5%) kwaajili ya ujenzi wa reli, tozo hiyo inaitwa Railway development Levy ambayo inatozwa kwakila bidhaa inayo ingizwa Kenya (every import to Kenya).

Uanzishwaji wa tozo hiyo una madhara mbalimbali kwa Tanzania yakiwemo yafuatayo;

1. Kupunguza ushindani wa bidhaa za Tanzania kwenye soko la Kenya hususani kwa bidhaa zili zinazo zalishwa Tanzania na pia kwenye viwanda vya Kenya m.f cement empty bags. Bidhaa inayotoka Tanzania kwenda Kenya itakuwa ghali zaidi kwa asilimia 1.5% nahivyo kukosa uwezo wakushindana kibei. Tayari Kampuni kama A to Z imeanza kuadhiriki vibaya.

2. Kutumia fedha za wananchi wa Tanzania kujenga reli ya Kenya itaiongezea bandari ya Mombasa Ushindani nakupunguza biashara inayopita bandari ya Dar es salaam kwa kiasi kikubwa kwakuwa wasafirishaji wa mizigo wa Uganda, Rwanda, Burundi na Kongo wataona unfuhu mkubwa kutumia reli kusafirishia mizigo yao badala ya barabara.

3. Nikinyume cha EAC Customs Union Protocal kuanzisha levy inayo-apply kwa bidhaa zote kwani hii itakuwa sawasawa na kuweka ushuru (tariff) baina ya nchi wanachama wakati chini ya Customs Union ushuru baina ya nchi kwa bidhaa zenye uasili katika nchi hizo inapaswa kuwa 0% na Common External Tariff ni 25%. Kitendo hiki cha Kenya kuanzisha tozo hii ktk bajeti yao ya mwaka huu kitakiuka makubaliano ya Umoja wa Forodha kwakuwa itafanya Common External Tariff (CET) kufikia 26.5%badala ya 25% na internal tariff kuwa 1.5% badala ya 0%.

Kuhusu suala la Rwanda na Burundi kutaka kuhamia bandari ya Mombasa nijambo ambalo bado kibinafsi nalitazama kuwa na chembe za siasa ya tri-latteral-the three Ks. Ukweli ni kwamba nchi hizi zimekuwa zikitumia bandari ya Dar es salaam kwakipindi kirefu sana hata kabla ya maboresho yasasa yaliyopo katika bandari ya Dar es salaam na miundombinu ya barabara kwenye Central Corridor. Central Corridor ni barabara inayo anzia bandari ya Dar es salaam kupitia Dodoma mpaka Kigali,Bujumbura Kampala, Goma na Kisangani DRC.Kuna juhudi mbalimbali zimefanyika zakuboresha bandari ya Dar katika miezi kadhaa iliyopita ikiwa ni pamoja na kupunguza vitendo vya wizi nakubadilisha management ya TPA nauanzishwaji wa ICDs (In-land Container Depots) ambazo zimesaidia kupunguza msongamano. Sisemi kwamba mambo bandari ya Dar ni shwari sana ila nakubali na kuamini kuwa yamefanyka mabadiliko makubwa ambayo yamewapunguzia watumiaji wa bandari ya Dar gharama. Wachambuzi wa mambo ya biasharara za kikanda wanasema kwa miezi mitatu iliyopita bandari ya Dar iliipiku ya Mombasa katika ukuaji wa biashara (trade volume growth rate).

Maboresho mengine yaliyofanyika katika Central Corridor ni pamoja na upunguzaji wa vizuizi vya polisi ( Police road blocks) ambavyo mwaka 2012 vilikuwa 52 kutoka Dar Port to Rusumo mpaka kati ya Tz na Rwanda na kwasasa viko vizuizi rasmi 15 tu.Vilevile Customs Stops au vizuizi vya mamlaka ya mapato vilivyo kuwepo kwenye njia hii (corridor) vimeondolewa baada ya uanzishwaji wa Electronic Cargo Tracking System mfumo ambao unayafuatilia malori ya transit electronically. Vizuizi hivi vilikuwa vinaongeza gharama ya biashara kwa maana ya muda uliokuwa unatumika kusubiri kukaguliwa na kuongezeka kwa mazingira ya rushwa.

Vilevile kikwazo kilichokuwepo cha waagizaji wa mafuta wa Burundi kulazimishwa kuingizwa kwenye mfumo wa Bulk Procurement kimeondoshwa na sasa Burundi wanaweza kuagiza mafuta moja kwa moja kwa mawakala wa nchi zingine.

Juhudi zingine ni pamoja na uanzishwaji wa mfumo wa utoaji taarifa za vikwazo vya biashara Non Tariff barriers (NTBs) SMS and Online reporting and Monitoring System unaotekelezwa chini ya Tanzania Chamber of Commerce Industry and Agriculture kwa ufadhili wa Trade Mark East Africa (TMEA). Kwakutumia mfumo huu wafanyabiashara wanaweza kutuma ujumbe mfupi wa simu wawapo njiani kusafirisha mizigo na kukutana na kikwazo chcochote na tatizo hilo kufanyiwa kazi mara moja kwa kushirikiana na taasisi husika.

Suala la mizani ya barabarani limebaki kuwa changamoto ambapo kutoka bandari ya Dar es salaam mpaka Rusumo kuna mizani 7.Suala hili limekuwa na mvutano mkubwa kati ya sekta binafsi na Serikali. Sekta binafsi inaamini uwepo wa mizani miwili au mitatu unatosha wakati serikali inaamini mizani 7 si mingi kutokana na uharibifu wa barabara unaofanyika kwa malori kuzidisha mizigo. Hata hivyo management katika mizani hizi bado nitatizo, kumekuwepo na vitendo vya rushwa na hivyo baadhi ya mizigo kuruhusiwa kupita ikiwa imezidisha mizigo jambo ambalo limeendelea kuharibu barabara zetu.

Kwa wale waliopita barabara ya Dar Dododoma kwa siku za karibu watakuwa wameona upande wa kushoto wa barabara ulivyo didimia. Inawezekana pia barabara hizi zilijengwa chini ya kiwango?. Wizara ya Ujenzi inaeleza kuwa kuna mkakati wa kununua mizani ya kupima uzito wa malori bila malori kusimama (weigh in motion) na kwamba kutoka Dar Port kufikia mpaka wa Rusumo itakuwepo mizani 8 mmoja ukiongezeka kutoka 7 ya sasa. Mzani huu wa wa 8 unatarajiwa kuwekwa katika bandari ya Dar es salaam. Hata hivyo jambo la msingi zaidi kakuzingatia siyo sana inadadi ya mizani hii bali ninamna inavyosimamiwa. Uongezekaji wa mzani wa 8 hata kama ni "weigh in motion" hasa kwa eneo la bandarini utaongeza uwezekano wakuwepo kwa msongamano zaidi.Kwa upande wa Kenya wana mizani 3 tu ambazo ni "weigh in motion" ukitokea nandari ya Mombasa kufikia mpaka wa Kenya na Uganda.Kwa Uganda wana mizani miwili tu na Rwanda hawana mzania hata mmoja. Hata hivyo kunauwezekano mkubwa kuwa idadi ya mizani inategemea pia na ukubwa wa nchi na ndio maana nikasema kuwa jambo la msingi ni namna mizani hii inavyo simamiwa pamoja na miundo mbinu iliyopo ktk mizani hii.

Juhudi zingine zimelenga kuhakikisha mipaka yetu inapitika kirahisi na kuondoa kero kwa wafanya biashara wanaopitisha mizigo yao kwenda nchi jirani. Kwa sasa kuna ujenzi unaoendelea wa One Stop Border Posts (OSBP) ambapo kwa mipaka kama ya Mutukula (Tz na Uganda), Kabanga (Tanzania na Burundi) ujenzi wa vituo hivi unatarajiwa kukamilika mapema mwakani.

Ukizungumzia gharama za usafirishaji kwa Central Corridor na Nothern Corridor (Mombasa to Kigali) hakuna tofauti kubwa sana kwani kwa container la 20ft au 40ft kusafirishwa kupitia Central corridor unakisiwa kugharimi 4000$ na kwa upande wa Nothern Corridor gharama ni around kiwango hicho hicho. Ila sasa inakuwepo na tofauti ya muda kwa mfano wakusafirisha mzigo kutoka Mombasa mpaka Kigali na kutoka Dar port mpaka Kigali kutokana na tofauti za umbali. Kwa hali ya Corrridor hizi mbili kwa sasa hakuna utofauti mkubwa sana ambaounaweza kusababisha nchi i.e Rwanda na Uganda kufanya uamuzi wakuacha kuitimia bandari ya dar es salaam moja kwa moja. lazima kuna sababu nyingi zaidi ya hali tunayo iona. Labda sasa tuzungumzie kuhusu mikakati iliyopo ya maboresho hiyo huenda ikatoa mwanga kwamba ni bandari gani au corridor gani miezi ijayo itakuwa na ufanisi zaidi ya nyingine. Rais wa Kenya aliagiza mamlaka za bandari ya Kenya hivi karibuni kuhakikisha kuwa bandari ya Mombasa inaongeza ufanisi nakufukisha siku 5 ( 5 days dwell time) tu kupitisha mizigo katika bandari hiyo. Juhudi za makusudi zinafanyika na serikali ya Kenya kuhakikisha reli inajengwa na endapo reli hiyo itajengwa basi itakuwa ningumi chungu kwa bandari ya Dar es salaam.Utumiaji wa barabara kusafirisha mizigo ni gharama sana na kwa nchi zinazofanya vizuri katika "logistic industry" hutumia reli badala ya barabara.Je! ni mikakati gani iliyopo Tanzania kuhakikisha kuwa reli zinafufuliwa na zingine kujengwa. Jambo lingine litakalo adhiri sana biashara katika nandari ya Dar es salaam ni uamuzi wa hivi karibuni wakuzuuia baadhi ya meli hasa zenye uzito mkubwa kufika bandarini. Meli hizi sasa zitaelekezwa bandari ya Mombasa nakuchukua biashara kubwa.

Bandari  ni raslimali muhimu katika uchumi wa nchi na kimsingi kama ikifanya kazi kwa ufanisi hatutahitaji hata pesa za gas wala madini na raslimali nyingine. Bandari hii inauwezo wakulisha vizazi na vizazi. mambo ya msingi yafanyike kuhakikisha tunapunguza muda wa kukaa kwa mizigo bandarini, gharama za bandari (port charges), tunaondoa kabisa vikwazo vingine hasa police road blocks, weigh bridges, prolonged border crossing procedures na kukomesha vitendo vya rushwa kwenye barabara zetu. Gharama ya lori moja kusubiri mpakani kwa siku moja inakadiriwa kuwa kati ya $200 na 400$ hivyo tukiharakisha upitishaji wa mizigo kwenye mipaka basi tutaokoa gharama kubwa nakufanya bandari yetu kuwa competitive. Pia watendaji wasio waaminifu na wasio na uwezo wakufanya kazi kwa ufanisi katika mizani, mipaka na bandarini waondolewe ilikuboresha mazingira ya biashara.

Kwaujumla nikwamba Tanzania inafanya biasharakubwa zaidi Kusini mwa Africa Southern Africa Development Community (SADC) kuliko EAC. Hata mizigo mingi inayopita bandari ya Dar es salaam inaelekea SADC. SADC ina nchi 15 ikimaanisha Tanzania ina nchi 14 yakufanya nazo biashara ukilinganisha na nchi 5 za EAC.Hivyo basi soko la SADC ni pana zaidi na lina South Africa ambayo nikati ya nchi nguli katika ufanyaji wa biashara za kimataifa ikiwa ni mojawapo ya nchi zinazo fanya kundi la  BRICS likipambana vikali na nchi zilizo endelea kama U.S.A na EU.Hata hivyo sababu hizi hazitoshi kusema kwamba Tanzania sasa ijiondoe EAC, bado kuna umuhimu mkubwa wakubaki katika jumuhia ya Africa Mashariki. EAC tayari iko kwenye hatua ya juu ya mtangamano yaani Common Market ikilinganishwa na SADC iliyoko katika hatua ya Free Trade Area (FTA).Huwezi jua nini kitatokea wakati SADC ikihamua kwenda katika hatua inayofuata ya Customs Union kwani tayari kuna upinzani wa taasisi kongwe ya Sourth African Customs Union (SACU).

 

Tayari tunajua nini kilichopo kwenye EAC Customs Union na Common Market. jambo la msingi nikuendelea kushikilia msimamo wetu wa gradual integration yaania mtangamano wa taratibu bila kukimbilia hatua za Monetary Union na Political Federation ambazo zina commitmnet kubwa zaidi. Ikiwa Kenya, Uganda na Rwanda wanahitaji kuharakisha mtangamno zaidi, tanzania haina sababu yakuwazuia isipokuwa taratibu ni muhimu zifuatwe kwa maana ya kuheshimu EAC Treaty. wakati dunia inazungumza kuungana zaidi hatuwezi kutafuta kuvunja miungano iliyopo bali tunaweza kuweka mikakati kuhakikisha tunafaidika zaidi nakuwa makini katika kuingia kwenye commitments ambazo zitatuadhiri. Jambo la muhimu zaidi nchi zetu zinatakiwa zijue kuwa unapokubali kuingia kwenye muungano wa aina yoyote ile ni lazima unapoteza a certain level of sovereignty. Nchi haiwezi kubakia na mamlaka yake kamili kimaamuzi inapokuwa imeungana na nchi nyingine katika jambo Fulani. Ni muhimu sana kwa wataalam wetu wanaowakilisha nchi yetu katika majadiliano mbalimbali ya kikanda wawe na weledi na uzalendo katika kila maamuzi wanayofanya. Tanzania ina nafasi nzuri zaidi yakufanya vizuri katika mitangamano hii ikiwa tutakuwa makini katika kila hatua.

 Elibariki Shammy,

NTBs Project Coordinator,

Tanzania Chamber of Commerce Industry and Agriculture (TCCIA) 

Mobile 0784477205.

 

 



2013/8/22 Juma Mzuri <jumamzuri@gmail.com>
Na Raymond Kaminyoge, 

Dar es Salaam. Chama cha Wasafirishaji wa Mafuta Tanzania (Tatoa), kimesema Rwanda na Uganda zitajitoa kutumia Bandari ya Dar es Salaam kuanzia Septemba Mosi, mwaka huu.

Katibu Mtendaji wa Tatoa, Zacharia Hanspope aliwaambia waandishi wa habari jana baada ya kukutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuwa nchi hizo zinajitoa kutokana na matatizo mbalimbali ambayo kwa muda mrefu zimekuwa zikiyalalamikia lakini Serikali haikuchukua hatua.

Hanspope alisema ushuru wa barabara na ushuru wa forodha ni baadhi ya vikwazo ambavyo vimekuwa vikilalamikiwa kwa muda mrefu na wafanyabiashara mbalimbali wa nchi hizo.

"Serikali ipunguze gharama za ushuru wa barabara na ushuru wa forodha ili kuwa na ushindani sawa na bandari nyingine na hivyo kuzivutia kutumia Bandari ya Dar es Salaam," alisema Hanspope.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Omary Chambo alikataa kuzungumzia lolote kuhusu suala hilo akisema halina mantiki yoyote kwake.... "Hivi hilo jambo unaloniuliza lina sense (mantiki) yoyote? Mie siwezi kujibu lolote nenda ukamuulize mwenyewe (Hanspope) maana wakati akisema mimi sikuwepo."

Alisema kujitoa kwa Rwanda na Uganda kuitumia Bandari ya Dar es Salaam hakutakiathiri chama hicho tu, bali uchumi wa taifa kwa ujumla.

Hayo yanatokea wakati Rwanda ikiendeleza vita yake ya maneno na Tanzania na mfululizo wa matukio ya kuitenga Tanzania kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki. Viongozi wa Kenya, Rwanda na Uganda walikutana Juni 25, mwaka huu mjini Entebbe, Uganda na kukubaliana kuongeza uhusiano wa kibiashara baina yao.

Kamati ya Bajeti

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Andrew Chenge alisema katika kikao kijacho cha Bunge, kamati hiyo itaibana Serikali kuhusu mikakati inayofanywa kukabiliana na ushindani wa kibiashara katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Alisema sababu ya Rwanda na Uganda kujitoa kutumia Bandari ya Dar es Salaam ni vikwazo katika barabara ikiwamo mizani mingi ya kupimia mizigo.

"Mizani ni mingi pia kuna usumbufu katika kupima mizigo yao na kwamba hali hiyo inawaletea usumbufu wafanyabiashara wengi," alisema.

Alisema vitendo vya askari wa usalama barabarani kudai rushwa pia ni miongoni mwa vikwazo pamoja na urasimu mkubwa katika utoaji wa mizigo bandarini ikilinganishwa na bandari nyingine.

"Ni lazima tujifunze kwa majirani zetu Msumbiji, upanuzi wa haraka wa Bandari ya Beira umekuwa kikwazo kwetu, kampuni nyingi zimeanza kuitumia bandari hiyo," alisema.

Chenge alikitaka chama hicho kuiandikia kamati hiyo mapendekezo yake ikiwa ni hatua ya kunusuru uchumi wa nchi ili waweze kuijadili bungeni.

Umoja wa nchi tatu

Marais Uhuru Kenyatta wa Kenya, Paul Kagame wa Rwanda na mwenyeji wao Yoweri Museveni walikutana mjini Kampala, Uganda na kuamua kuitumia Bandari ya Mombasa kwa shughuli zao.

Waliahidi kuimarisha ufanisi katika huduma za Bandari ya Mombasa ili kuhakikisha bidhaa zinafika mapema Uganda na Rwanda.

Pia walikubaliana kujenga reli mpya ili kurahisisha usafirishaji wa bidhaa kutoka Mombasa kwenda Kenya na Uganda.

Viongozi hao walikubaliana pia kushirikiana katika sekta ya nishati hasa ikizingatiwa kuwa Uganda imegundua mafuta.

Nchi hizo tatu ambazo zimeruhusu kwa raia wao kusafiri kwa vitambulisho pale wanapotembelea nchi tatu miongoni mwao, zitakutana tena Kenya mwezi huu.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment