Friday 14 October 2016

[wanabidii] Tumuenzi Nyerere kwa kukataa kusaini mkataba wa EPA na nchi za Ulaya

Leo ni siku ya kuadhimisha kukumbukumbu ya kifo ya mawasisi wa Taifa letu, Mwalimu Juliasi Kambarage Nyerere ambaye anajulikana Ulimwenguni kote kwa misisimamo yake ya haki na kutetea utu na maendeleo kwa binadamu wote, na katika hayo ya Mwalimu Nyerere ndio leo hii Tanzania tuko salama pamoja na misukosuko iliyoipata dunia ikiwemo vita baridi na kadhalika

Tumekuwa salama kwa kuwa tupo katika nchi zisizofungamana na uande wowote ule pamoja na nchi zinazojali utu na haki za binadamu, Mwalimu Nyerere alikataa biashara na nchi yeyote duniani yenye masharti ya kutunyonya kwa njia yeyote iwe biashara au misaada.

Leo hii nchi zetu za Afrika ya Mashariki na kati zipo katika mtihani mzito wa kusaini mkataba mwingine ambao kwa maoni yangu siutofautishi na mikataKwa mujibu wa mkata wa EPA, nchi za umoja wa Ulaya (EU) zinatakiwa ziruhusiwe bidhaa zao ziingie nchini mwetu bila kutoza ushuru, Aidha EPA ingewezesha bidhaa za Afrika Mashariki kuuzwa ndani za (EU) bila ya ushuru.

Tangu mwaka 2002 nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda zimekuwa zikijadiliana, lakini tatizo linatokea pale EAC inapogawanyika baada ya baadhi ya nchi kutaka kusaini na zingine zikisita kusaini mkataba huo wakati huo huo.

Tatizo kuwa kwa mujibu wa wa shirika la biashara ya kimataifa (world Trade Ogreanazation-WTO, nchi za EAC haziwezi kusaini mojamoja ni lazima zisaini zote kwa pamoja.

Kenya kwa upande wake inahamu kubwa ya kusaini mkataba huu wa EPA kwa vile ndio inayoongoza katika EAC kwa katika biashara na EU.

Tatizo la Kenya ikiwa nchi za EAC hazitasaini mkataba huo italazimika kulipa kodi kati ya asilimia 8 hadi 12 kwa uzwaji wa bidhaa zake katika masoko ya EU. Wakati huo huo Kenya inapata zaidi ya shilingi (K) Trilioni 3 kwa mwaka kutokana na bidhaa zake katika masoko ya (EU)

Baya zaidi ni kuwa Kenya itaondolewa katika kundi la nchi zenye upendeleo (Generalised Scheme of Preference-GSP) amabao unahusu bidhaa zake za maua zinazopelekwa Ulaya na hivyo kutakiwa kulipa kodi zaidi.

Labda tuangalie sababu sisi Tanzania hasara tutakazozipata tutakaojiunga na EPA, kukubali Epa kwa nchi yetu maana yake ni kuukaribisha na kumiminika kwa bidhaa toka Ulaya, aidha sharti la kuondoa ushuru kutoka nchi za Ulaya ni jambo la hasara kwetu kwa kuwa kuingizwa kwa bidhaa za ulaya bila ushuru nchi yetu itakosa mapato, na ushuru ni muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi na ndio maana nchi za ulaya zilitumia ushuru katika kujiletea maendeleo.Pia ni vyema tukafahamu kuwa kuna tofauti baina ya nchi za ulaya na nchi za Afrika ya mashariki na Afrika kwa ujumla wake.

Serikali za Ulaya zinatoa ruzuku kwa wakulima wao ili kuhudumia bidhaa zao vyema ili bidhaa zao zisindane vyema katika masoko ya dunia. Hivyo kumshindanisha mkulima wetu na mkulima wa Ulaya ni sawa na kumshindanisha Daudi na Goliathi.

Katika EPA pia kuna kipengele kinachosema nchi inaposaini mkataba huo inatakiwa kuruhusu asilimia 80 la soko lake kupokea bidhaa kutoka Ulaya, pamoja na sekta ya kilimo ambapo nchi yetu itarazimika kuruhusu asilimia 80 la soko lake kupokea bidhaa kutoka Ulaya.

Endapo tutasaini EPA tutalazimika pia kupooteza uhuru wa kibiashara na kiuchumi. Ni pamoja na kuzuia makubaliano mapya ya ushirikiano na nchi zingine. Mfano mkataba wa AGOA na Marekani ambao umemalizika 2015.

Hasara nyingine kwetu kama taifa kwa kiusaini EPA, hatutakuwa na ushuru wa nafaka tutakazozisafirisha kwenda Ulaya na wakati huo huo hatutakuwa na ushuru wa bidhaa zitakazoingia kutoka Ulaya. Hivyo serikali kukosa mapato kwa ushuru wa bidhaa zinazoingia na kutoka, mbaya zaidio tutakuwa na kazi ya kuzalisha bidhaa ghafi kwa viwanda vya ulaya badala ya kuanzisha viwanda vyetu.

Suala la msingi la kujiuliza je sisi tutauza nini huko Ulaya chini ya mkataba wa EPA? Je uchumi na uzalishaji wetu unalingana na wanchi za Ulaya? Kwa mfano serikali Ulaya zinalipa ruzuku kwa wakulima wao kwa kuzalisha maziwa. Matokeo yake Ulaya inazalisha maziwa mengi mpaka hawana pa kuyahifadhi na kuyaeleka yanabwagwa kila siku, Hivyo EPA ikiruhusiwa ina maana maziwa bwerere yataingia kutoka Ulaya.

Katika hali hiyo maziwa yetu ya Tanga, Mara na Iringa yataweza kushindana na maziwa kutoka ulaya? Au ndio tutakuja kuua viwanda vyetu na wakulima na wafugaji waouza maziwa hapa nchi ndio utakuwa wamefikia mwisho na kuwa hasara kwa taifa.

Kiukweli chini ya EPA, Afrika mashariki na Afrika kwa ujumla hazitaweza tena kuunda misingi ya viwanda katika uchumi wake, na Badala yake tutakula kuku, mayai, nyama na maziwa kutoka ulaya.

Kwa mkataba wa Epa ni vigumu kwa kampuni za kiafrika kushinda zabuni za nchi nla Ulaya lakini ni rahisi kwsa makapuni ya Ulaya kushinda zabuni katika za Afrika za Afrika kutokana na kukomaa kwa teknologia na mbinu za kibiashra kwa nchi zao, hivyo basi jambo hilo litachangia kuua kampuni za nchi za kiafrika.

Tukiachana na hilo takwimu zinaonyesha kuwa kwa mwaka 2013 pekee nchi za ulaya ziliagiza bidhaa Afrika ya mashariki zenye thamani ya euro bilioni 2.3 kwa kununua vitu kam mbogamboga, maua, samaki, chai, tumbaku na kahawa. Wakati afrika mashariki ilinunua bidhaa za thamani ya euro 3.5 kutoka ulaya kwa kiununua mitambo, magari, madawa na kadhalika.

Kwa maana nyingine tunaambiwa tuzalishe bidhaa ghafi na kuuza Ulaya kisha na kuzinunua kutoka ulaya bidhaa za viwandani, hilo ndio eti soko huria linalokusudiwa chini ya EPA.

Tukiwa tunaadhimisha siku ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa TaifA, Mwalimu Julias Kamabarage Nyerere, basi tumuenzi kwa kukataa kusaini mkata wa EPA, ambao kiuhalisia una lengo la kutufanya kuwa soko la bidhaa za Ulaya na sisi kuwa wazalishaji wa malighafi pamoja na kuendeleza ukoloni mambo leo

0 comments:

Post a Comment