Friday 14 October 2016

Re: [wanabidii] JANGA LIKIJA JUU YA JANGA: NANI ATASIMAMA KUELEZA?

A goodcomprehensive plan that may not even be considered. Watu hawataki kujishughulisha vichwani sina uhakika kama mpango mzuri kama huu unaweza hata kujadiliwa. Ninajua kuwa hakuna anayeweza kuuza vifaa vya ujenzi kwa sasa kwa sababu watu wamebanana. Lakini kunahitajika kitu kufanyika. Aha habari za tetemeko kurudiwa, Mvua za upepo haiwezekani zisipite. Nyumba zilizopasuka lazima zimwagike. Hapo ndipo ilipolala kashehse
--------------------------------------------
On Fri, 10/14/16, 'Hildegarda Kiwasila' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: Re: [wanabidii] JANGA LIKIJA JUU YA JANGA: NANI ATASIMAMA KUELEZA?
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Friday, October 14, 2016, 10:18 AM

Muhimu cha kufanya Elisa ni kwanza:
i) Kutumia wataalamu wa Ecology na wa masuala ya matetemeko
ya ardhi kuangalia kama hilo eneo wanakoishi ni hatarishi
kwa matetemeko na mafuriko.

2) Ikiwa ni hatarishi ni wazilikitokea tena litabomoa nyumba
na kuingiza jamii ktk hasara. Hivyo budi watafute eneo la
kuwajengea nyumba kwa kutumia NHC kwa kujenga nyumba ambazo
hela zitatosha na kulingana na wingi wa watu katika familia
kwa standard space kwani building regulation zipo. Kusiwe na
mbanano. Hivyo itabidi kutafuta eneo na kufanya
participatory land use planninh na kuwapa hati miliki ya
makapo. Budi watoe fidia kwa ardhi ya kufaa watakayochukua
kama sio ya serikali.

3) Afanyavyo kiongozi kuwajengea nyumba ni muhimu ila
anajenga wapi panapofaa kuishi ukiangalia mazingira yasiyo
hatarishi. Ukiwapa pesa hao baadhi wataanza kunywa Lubisi na
baadhi ya walezi au watoto makanjanja wataanza kutaka
kuzitumia vibaya. Ukiwapa vifaa baadhi watauza na kusepa
mjini na kuacha vizee vikiteseka. Vibaka wapo pia ktk
familia na ndiko kunakotoka akina scorpion, panya road na
fisi na wengineo.

4) Mahali ambako palitokea tetemeko watakuwa wana mashamba
yao wapewe Hati Miliki ya Kimila. Kule wanakopimiwa wapewe
Hati Miliki ya Serikali na ipigwe muhuri-Haihamishiki bila
ya kibali cha Waziri wa Ardhi. Hii itakomesha uuzaji wa
ardhi hovyo kwa matajiri na wageni. Hati miliki itakomesha
wavamizi wa ardhi na uuzaji hovyo ufanywao na familia na
viongozi wa kijiji/Mtaa. Watu wa Kagera wana ardhi ambayo
ina nyumba na mashamba ya midizi na miti ya matumizi ya
familia. Kila mmoja anakata ,miti yake kwa kuni au mkaa.
Hivyo mashamba yao waachiwe waendelee kulima ila pale
watakapopimiwa serikali iangalie kuwa kila mmoja anayepewa
ardhi ajenge kama sheria ya ardhi inavyosema yaani 60% ya
plot na kubakiza 40% kwa mahitaji mengine ya choo, jiko,
mabanda ya uwani na bustani sio kujenga 100% halafu hata pa
kulima mbogambona  mtu hana kisha anabananisha feeder
road anaweka kiosk cha biashara. Moto ukiwaka hakuna pa gari
kupita au watu kupita kuuzima. Umefika hata vijijini
kulazimishe ustaarabu uwepo hasa katika mipango miji na
vijiji. Tuwache kuwa na majengo bananishi na squatters
vijijini. Tuwe wastaarabu. Inapofika shule-kila shule iwe na
space kubwa pamoja na mashamba kama ilivyokuwa wakati wa JK
Nyerere. Mashamba ya waanfunzi kujifunza kilimo, kupanda
miti kuzunguka shule na viwanja vya michezo sio Kiosk za
biashara kila kona ya shule na mabada ya mambo mengi
yanayoathiri elimu na mazingira ya shule.

5) Kamati ya kuhusisha wataalamu wa ardhi, mazingira,
majengo na kuangalia ramani nzima na matumizi ya pesa muhimu
sana kupunguza ufisadi ili kieleweke. Baada ay upimaji ardhi
na ujenzi evaluation ifanyike kuona kipi kilipangwa na
kimefanyika kipi at what cost na auditing muhimu.
Zinazobakia kama ni hela au vifaa vitumike vipi. Pia kujenga
makao ya wazee na vilema wasio na ndugu huko kijijini
walelewe naUstawi wa Jamii.

6)Kama ni hela za kuwapa taslimu-kuepuka matumizi mabaya
budi kupeleka NBC, NMB, CRDB kuwafungulia accounta hapo hapo
kijijini na kuziingiza ktk account. Tumia vitambulisho vya
Raia, Mpiga kura na vya vyama na kadi za kuzaliwa kwa
walionavyo uonfdoe urasimu wa wao kwenda bank mbali kufungua
account. Mpe kadi yake hapo hapo kijijini. Hufanyika hivyo
katika Valuation and Resettlement Tanzania. Ukimpa hela
taslimu-utata lipa kwa cheque na weka mashine za kuchukua
hela ofisi mojawapo ya Kata na Tarafa ili banks hizo ziwe
karibu. Ulizi wa mashine hizo muhimu viobaka wengi. Ukiwapa
cash-watavamiwa na majambazi mpaka wageni wahamiaji ambao
nao wameanza kupokea pesa za TASAF. Tujifunze kutokana na
makosa yatokeayo maeneo mengine.

Kama Kawa
--------------------------------------------
On Thu, 13/10/16, 'ELISA MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
wrote:

Subject: [wanabidii] JANGA LIKIJA JUU YA JANGA: NANI
ATASIMAMA KUELEZA?
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Thursday, 13 October, 2016, 22:22

Mwezi mmoja uliopita tarehe 10
September kulitokea tetemeko la ardhi na kuleta maafa
katika
Mkoa wa Kagera. Watu wasiozidi 19 walikufa, nyumba kadhaa
zikaanguka na nyingine nyingi zikapata nyufa. Nyufa
nyingine
ni hatarishi kiasi nyumba hizo ni hatari kuzitumia na
nyufa
nyingine si hatarishi. Katika dharura hiyo miyndombinuu
kadhaa iliharibika. Mfano ni shule kadhaa zilianguka,
barabara zilipasuka, makanisa yalianguka na kadhalika.
Nchi, serikali, balozi za nchi za nje, vyama vya siasa;
mashirika mbalimbali na watu binafsi waliitikia kwa kutoa
michango mbalimbali kwa lengo la kusaidia waathirika wa
tetemeko hilo

Niliwahi kufanya hesabu wakati huo nyumba zikiwa elfu sita
zilizoathirika nikahesabu kama sh. Million 10 zingetumika
kwa kila nyumba basi zingehitajika bilioni 60. Hazipo.
Kati ya waathirika wapo waliokwisha maliza kurekebisha au
kujenga upya nyumba zao kiasi athari za tetemeko kwao si
hoja. Hii ni nafuu kwa kamati ya maafa.
Wapo ambao wamejaribu na kukwama kwa sababu uwezo wao wa
kujenga ni mdogo. Wapo ambao ni haki yao kukaa kimya na
kusubiri msaada maaqna hawawezi kuzijenga.
Misaada ambayo imetolewa hadi sasa si ile ya kurejesha
majengo ya kuishi.
Ninapopita maeneo yaliyoathirika nayaona yote
ninayoyaeleza.
Ninaona pia watu wanaoishi kwenye nyumba ambazo ni hatari
kutokana na nyufa zilizotokea.
Ninaamini halitakuwa jambo la kushangaza kama mvua
zitakuja
na upepo mkali mkoani Kagera. Lakini najiuliza mvua hiyo
ikinyesha na kuzipiga na kuziangusha nyumba zilizopasuliwa
na tetemeko na watu zaidi ya waliokufa kwa tetemeko
wakafa;
ni kiongozi gani atasimama kutoa maelezo? Rais, makamu
wake,
Waziri Mkuu au Mkuu wa Mkoa? Atawalaumu watu kwa kutumia
nyumba hizo kwa sababu serikali ilishazitangaza kuwa
mipasuko iliyotokea ni hatarishi? Jambo hili si la kucheza
nalo. Kuna miundo mbinu inayowezesha kufika walipo
waathirika. Nani ataelewa kuwa serikali ilitangulia
kutengeneza miundo mbinu? Misaada iliyotolewa ilikuwa
inatangazwa kuwa ni kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa
Tetemeko. Ni sawa, Na shule kujengwa ni kuwasaidia
waathirika. Lakini kweli baada ya wanafunzi kusambazwa
shule
nyingine inaeleweka kuwa watu waendelee kuishi kwenye
mahema
au nyumba mbovu kwa sababu kwanza tunajenga shule? Nani
ataelewa? Nani ataelewesha? Serikali ilipotangaza kutoa
sementi na mabati waathitika waliandaa mazingira kuanza
kujenga. Nani kasema kila aliyevunjikiwa nyumba ana uwezo
wa
kujenga? Ninafikiri hili jambo si la kuchezea. Mvua
inakuja
na ipo itakayonyesha kwa vurugu. Ni kawaida. Lazima
itazivuruga nyumba ninazozipitia kila mara. Kati ya wote
wanaowajibika na kadhia iwezayo kutokea, Mkuu wa mkoa
namuona akiwa hatarini. Ndiye aliye karibu. Kama wote
wakibanwa watasema hatukujua. Yeye atasemaje. Lakini pia
ni
garama ndogo yeye kuwajibika/kuwajibishwa. Nyumba
zikianguka
na kuua watu mia rais atatangaza tu kuwa 'amemtumbua'
kwa uzembe maana hakuweza kutumia misaada vizuri. Ndiye
mwenyekiti wa kamati ya maafa. Baada ya hapo atachaguliwa
mwingine mambo kwisha. Si kama kumuwajibisha waziri Mkuu
ambaye baraza lote litafumuliwa. Lakini heri Mkuu wa Mkoa
kutumbuliwa kwa sababu aliamua kutumia misaada kuwajengea
nyumba badala ya kuacha wao kujijengea kuliko kutumbuliwa
kwa sababu watu walifia kwenye nyumba zilizobomolewa na
tetemeko huku akiwa na misaada chini yake. Ataeleweka kwa
dhamira yake na kwa umma, Tusipuuze tahadhali kama hizi.
Elisa Muhingo


 
  --
 
  Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
   
 
  Kujiondoa Tuma Email kwenda
 
  wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
Utapata Email ya
  kudhibitisha ukishatuma
 
   
 
  Disclaimer:
 
  Everyone posting to this Forum bears the sole
responsibility
  for any legal consequences of his or her postings,
and
hence
  statements and facts must be presented responsibly.
Your
  continued membership signifies that you agree to
this
  disclaimer and pledge to abide by our Rules and
  Guidelines.
 
  ---
 
  You received this message because you are subscribed
to
the
  Google Groups "Wanabidii" group.
 
  To unsubscribe from this group and stop receiving
emails
  from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
 
  For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.
 
 
 
   
 
  --
 
  Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
   
 
  Kujiondoa Tuma Email kwenda
 
  wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
Utapata Email ya
  kudhibitisha ukishatuma
 
   
 
  Disclaimer:
 
  Everyone posting to this Forum bears the sole
responsibility
  for any legal consequences of his or her postings,
and
hence
  statements and facts must be presented responsibly.
Your
  continued membership signifies that you agree to
this
  disclaimer and pledge to abide by our Rules and
  Guidelines.
 
  ---
 
  You received this message because you are subscribed
to
the
  Google Groups "Wanabidii" group.
 
  To unsubscribe from this group and stop receiving
emails
  from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
 
  For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.
 

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole
responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and
hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to
the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment