Thursday, 6 October 2016

[wanabidii] Sijawahi kuona kiongozi strategic kama Rais Magufuli!

Raisi Magufuli kwa kweli nimemvulia kofia, huyu jamaa anaielewa hii Dunia, watu kaliba ya
Pombe Magufuli (PhD) ndiyo watu ambao hufanikiwa maishani kwa kila wakifanyacho!

Ukiangalia Uraisi wake tangu ameingia, anafanya mambo muhimu tu, au ana uwezo mkubwa wa kutengenisha vitu muhimu na vile visivyo muhimu, angalia ziara zake alikwenda Rwanda na Uganda huko kote ni kwa sababu alikuwa anapigania SGR project baadaye tukasikia Rwanda wamewatosa Kenya na kujiunga na SGR ya kwetu, na Uganda ni kwa sababu ya Bomba la mafuta baadaye tukasikia Uganda wamewatosa Kenya na kuamua kutumia Bandari yetu ya Tanga, huko kwingine koote mara commonwealth, au AU mara sijui Japan na viongozi wa Kiafrika ni talk shop tu na tunawakilishwa na aidha Balozi, W/Mkuu au Makamu wa rais!

Sasa leo hii rais wa Kongo (DRC) ametua nchini na yaliyoongewa na kuafikiwa sina haja ya kuyarudia, tusisahau pia soko la Air Tanzania yetu nchini Kongo limegusiwa, kwamba Air Tanzania itakuwa inaruka kwenda Kongo, hakika sijawahi kuona ktk maisha yangu Raisi strategic na asiyeyumbishwa kama Pombe Magufuli!

0 comments:

Post a Comment