Tuesday 2 August 2016

Re: [wanabidii] Biashara ya kuku wa kienyeji inavyoweza kukuondolea umasikini.

Nyabenda
Inawezean kanza nakuku 20 wakafikia 10,00 bila kuwa na jogoo?
--------------------------------------------
On Mon, 8/1/16, 'Nyabenda Juma' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: Re: [wanabidii] Biashara ya kuku wa kienyeji inavyoweza kukuondolea umasikini.
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Monday, August 1, 2016, 4:27 PM


Kama
dhamira yako ni kufuga kuku wa kienyeji ili kuuza mayai(ya
kula) unafuga jogoo wa nini?, au wewe ni mmoja kati ya wale
wanaotaka kuiaminisha jamii kuwa kuku jike hawezi kutaga
mayai bila jogoo, au kwamba kuku wa mayai wasio na majogoo
hupewa dawa maalum ili kutaga mayai?Sent
from Yahoo Mail on Android

On Mon, Aug 1, 2016 at 2:55 PM, 'Charles
Nazi' via
Wanabidii<wanabidii@googlegroups.com>
wrote:
Watu
wengi wamekuwa wakifikiria kuhusu namna ya kujikwamua kutoka
kwenye
umasikini.Leo hii nitawaelezea kuhusu biashara ya kufuga
kuku wa
kienyeji ambavyo inaweza kukukwamua kutoka kwenye umasikini.
Lengo kuu
ni kuwawezesha watu kutengeneza ajira kwao binafsi na watu
wengine.
Takwimu za uzalishaji (kutaga,
kuangua na kukuza kuku)

Utafiti uliofanywa na Dr. John Bishop kwa msaada wa shirika
la kitaifa
la utafiti wa kilimo nchini Equador na Chuo kikuu cha
Florida nchini
Marekani, umeonyesha kuwa ; Kama kuku akitunzwa vizuri
kutokana na mbinu
bora za ufugaji, anaweza Kuongeza uwezo wa kutaga mayai
kutoka mayai 10
hadi mayai 12 kwa mwezi. Kwa mfano ukiwa na kuku 12 na
jogoo 1
waliolishwa kilo 1 ya nafaka kila siku unaweza kuuza dazani
10 za mayai
kila mwezi ambayo ni sawa na mayai 4 kila siku.
Jee unapenda kutajirika kwa kufuga na kuuza
kuku?

Angalia mchanganuo wa mahesabu mapato yako yatakuwa kama
ifuatavyo, Kwa
kipindi cha miaka 2. K wa mtaji wa Sh. 500,000/= kama una
eneo la eka 1
na mabanda ya kutosha kiasi cha kuku 10,000. Ukianza kwa
kufuga kuku 25
( kuku 20 na jogoo 5) ambao utawanunua kwa Sh. 250,000.00.
Hao kuku 20
wakianza kutaga vifaranga 10 kila mmoja wataangua vifaranga
200 watunze
vizuri katika vifaranga hao tuchukulie majike yanaweza kuwa
150 ambao
ndani ya miezi 6 au zaidi nao wataanza kutaga. Kipindi hicho
utakuwa na
kuku (200+ 25 =225.) Baada ya hiyo miezi 6 kuku watakaotaga
ni 170 kila
mmoja akipata vifaranga 10 mpaka mwisho wa mwaka utakuwa na
kuku
(1700+20+55=1775) ukiuza kuku 1,000 kwa bei ya Tshs. 10,000
utapata
Tshs. 10,000,000/=. Mwaka wa 2 majike 775 yakiangua
vifaranga 10 kila
mmoja utakuwa na kuku 7,550 mwisho wa mwaka ukiuza kuku
3,000 kwa bei ya
Tshs. 10,000 utapata Tshs. 30,000,000/= Hesabu hizi ni kwa
makadirio ya
chini sana kwani kama nilivyoelezea hapo juu kuku mmoja
kama atatunzwa
vizuri anaweza kuataga mayai kati ya 10 hadi 12 kwa
mwezi.
.Kuku wa
kienyeji wamekuwa wakifugwa kwa wingi vijijini kwa malengo
ya kupata
nyama na mayai kwa ajili ya familia husika na kwa ajili ya
kupata pesa
za kujikimu. Kuku na mayai ya kienyeji yana faida kubwa
kiafya
kutofautisha na kuku wakisasa ambao hukuzwa kwa kemikali.
Idadiya kuku
Tanzania inakadiriwa kuwa na jumla ya kuku Milioni 34
wanaofugwa na
takribani 60.5% ya kaya zinazojishughulisha na kilimo. Hata
hivyo
uzalishaji wake umebaki kuwa duni kutokana na changamoto za
wafugaji
zifuatazo; Utunzaji duni , Udhibiti mdogo wa magonjwa, lishe
duni,
makazi duni, Uzaliano wa karibu, Teknolojia duni, Kukosekana
kwa
mtazamo/mwamko wa kibiashara.
Faida ya
kufuga kuku wa kienyeji.

Ufugaji wa kuku wa kienyeji una manufaa mengi kwa mfano;
Kuku hutumia
eneo dogo kuliko wanyama wengine wa kufugwa, pia hutumia
chakula kidogo
hivyo ufugaji unaweza kuendeshwa bila kutumia mtaji mkubwa.
Kuku
wanaweza kupewa mabaki ya chakula pamoja na vyakula vya
kujitafutia kama
vile wadudu,mbegu na majani. Kazi za usimamizi wa kuku
zinaweza
kufanywa na mama na watoto. Kuku na mayai humpatia mfugaji
chakula bora
na kumuongezea mapato. Pia mfugaji ni kama mtu aliyewekeza
fedha zake
benki au kwenye kitegauchumi kingine ambapo kuku huweza
kuongezeka
kutokana na kuku kutaga na kuangua vifaranga kama faida
inavoongezeka
benki na kwenye vitegauchumi vingine. Mfugaji ni sawa na mtu
aliyeweka
akiba benki kwani akipata shida anaweza kuuza kuku na kulipa
ada, mahari
matibabu ya hospitali pamoja na shida zingine. Kuku wa
kienyeji
anasaidia kusafisha mazingira kwa kula wadudu na kuongeza
rutuba kwa
mbolea inayotokana na kinyesi cha kuku ambacho hakina
kemikali. Mbolea
hii ni nzuri sana na kama inazalishwa kwa wingi inaweza kuwa
chanzo
kingine cha mapato kwa mfugaji wa kuku. Kuna mjasiriamali
ninayemjua
anafuga kuku wengi anazo tani nyingi za mbolea hii na anauza
mbolea ya
mavi ya kuku kwa Sh. 600 kwa kiloba cha kilo 50. Kuku wa
kienyeji ana
uwezo mkubwa wa kuhimili magonjwa, hutaga mayai na kutunza
vifaranga
badala ya kutumia mashine. Kuku wa kienyeji anaweza kuishi
nchi yoyote
duniani bila kuathiriwa na hali ya hewa.

Aina za magonjwa ya kuku na jinsi ya kukinga magonjwa.

Wapatie chanjo kuku wako kwa afya bora. Wapatie kinga mara
kwamara kila
baada ya miezi 3. Magonjwa yafuatayo ndiyo huwa
yanawashambulia kuku.
New castle

Dalili za ugonjwa huu ni kuku kushindwa kupumua, kukohoa na
kutokwa na
mate,kuwa na kinyesi cha rangi ya kijani, ugonjwa huu hauna
dawa. Chanjo
hutolewa machoni kwa njia ya matone.

Minyoo.
Dalili za mionyoo
ni kuku kukosa hamu ya kula uzalishaji wa mayai kupungua.
Ukiona dalili
hizo waone wataalamu wa mifugo upate dawa.

Wadudu.
Utitiri
husumbua kuku, kwa kuwasababisha kukosa usingizi,ngozi
kuharibika,huathiri uzalishaji wa mayai. Ukiona dalili hizi
wasiliana na
wataalamu wa mifugo upate dawa.
Magonjwa
ya mapafu.
Huathiri
sehemu za kupitishia hewa na kuwa na sauti ya kukoroma. Hali
hii
hupunguza uzalishaji wa mayai na uzito wa kuku kupungua.
Ukiona dalili
hizi wasiliana na wataalamu wa mifugo upate dawa.
Mambo mengine unayopaswa kuyajua kama mfugaji
wa kuku

Inapokuja katika ufugaji wa kuku wa kienyeji ,mbinu
inayotumiwa
kijijini ile kuku huachwa azurure katika boma bila uchungaji
ama na
uchungaji mdogo.Kuna matatizo mengi ambayo kuku hukutana
nayo. Kuku
halishwi vyema kwani hula masalio ya.chakula na mabaki
mengine
wanayoyapata. Vifaranga wadogo huachwa washindanie chakula
na kuku
wakubwa na huwa nyama rahisi kwa wanyama wanaowinda na kula
nyama na
husambaza magonjwa. Kuku hawapati maji ya kutosha na hawana
mahali pa
kujisetiri dhidi ya upepo na mvua ama kuwaweka salama dhidi
ya wanyama
wanaowinda na kula nyama bila kusahau wezi. kuku hutaga
mayai ardhini na
yanaweza kuharibiwa kwa urahisi na kuliwa na wanyama
wengine. Sio
kawaida kuku kupewa chanjo na matibabu dhidi ya magonjwa na
vimelea.
Matokeo ni kuku wengi huwa wagonjwa na hukua pole
pole,hutaga mayai
machache na nyama kidogo.
Ili kuhakikisha
mapato mazuri kutoka kwa kuku wako,fanya yafuatayo:

Kuwapatia kuku mgao mzuri wa vyakula tofauti na maji
safi.Kutemeana na
kipindi cha mwaka,wataweza kujitafutia chakula kwa kukwaruza
ardhi
katika boma. Wapatie chakula cha ziada ili kuku waongeze
uzani na kuku
watage mayai mengi zaidi. Walishe vifaranga na chakula
kilicho na
protini kama mchwa ili wakue kwa haraka na wawe na afya.
Wajengee kuku
mahali penye giza na patulivu ambapo wanaweza kutaga mayai
yao.Kuku
huhitaji kujisikia wakiwa salama kutoka kwa wanyama
wanaowinda na kula
nyama na wapita njia. Kama kuku watasumbuliwa mara kwa mara
watakuwa
wakiviacha viota vyao na hii huathiri uanguaji wa mayai.
Ikiwa nia yako
ni utoaji wa mayai,ni vizuri kufuga kuku wa kike pekee.Jogoo
mmoja
anaweza kufugwa aangalie wanyama wanaowinda na kula nyama na
kuwahudumia
kuku.Wakati jogoo wa ziada wanapofikia umri wa
kuuzwa,wanafaa
kuuzwa,kuchinjwa ama kutolewa kama zawadi kuzuia jogoo kula
chakula
ambacho ni adimu na kupigana na kuwataabisha kuku. Ukubwa wa
kundi
unafaa kuafikiana na ukubwa wa nyumba au banda ,kiasi cha
chakula
unachoweza kununua na raslimali za chakula katika maeneo
yanayokuzunguka. Usinunue kuku kutoka katika vyanzo ambavyo
havijathibitiwa haswa vipindi milipuko ya magonjwa ni
kawaida kwa sababu
wanaweza kusambaza magonjwa kwa wengine. Toa chanjo mara
kwa mara
kulingana na ushauri wa watoaji chanjo na madaktari wa
wanyama wa
nyumbani. Vifaranga wachanga wanapaswa kuchanjwa dhidi ya
magonjwa ya
kawaida ya kuambukizana wakifika umri wa wiki 2-3.
Ikiwa kuku watataabika kutoka kwa ugonjwa sugu
unapaswa:
• Kuita daktari wa wanyama
• Kumwtenga kutoka kwa wengine
• kuku anafaa kuuliwa mara moja kwa
kutegemea jinsi ugonjwa ulivyo mzito na

Anafaa kuchomwa ama kuzikwa katika kina kirefu ili kuzuia
mbwa na wanyama wengine kuwachimba na kusambaza ugonjwa.
Angalia ni kuku gani wana dalili za kutaka
kuangua mara moja kwa mwezi na uwapatie matunzo ya ziada
CHARLES NAZI
Mwandishi wa
makala hii ni Mkurugenzi wa Kampuni yaCPM Business
Consultants kwa mawasiliano zaidi pigasimu namba
0755394701



--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.




--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment