Thursday, 14 April 2016

Re: [wanabidii] Rais Magufuli Wabadilishe Watanzania - Umaskini ni Hulka

Kwani kuna shortage ya malofa wa mawazo duniani! Hapana wapo wengi tu. Yaani mtu anasema serikali ifanye hivi kwanza ndipo ije kwa wananchi, je maisha ya hao watu yanasubiri kuanza mahitaji pale serikali itakapokamilisha mambo yake? Lini kazi hiyo itakamilika. Leo hii ni zaidi ya miaka 55 tangu Tanhganyika ipate uhuru, na kila siku serikali imekuwa ikidai au kujitahidi kutatua matatizo ili kuboresha maisha ya wananchi, je shughuli hiyo imekalika, au bando mbichi, mbichi kabisa.
Serikali huwa haina darasa la kuwaweka wananchi darasani na kuanza kuwaelimisha, hufundisha kwa njia ya sheria na hupanga sheria hiyo lini ianze kutumika huku viongozi wa ngazi mbli mbali wakiwasiliana na wananchi kuwaelimisha juu ya suala fulani linalotakiwa kufanywa, bahati mbaya sisi Afrika hata huwa hakuna muda wa kukusanya maoni ya wananchi ili sheria jambo fulani lifanyike kama linavyopendekezwa, viongozi wetu siku zote wana final say.


On Wednesday, 13 April 2016, 22:12, De kleinson kim <dekleinson@gmail.com> wrote:


Ipyana,
Inabidi tufurahi, nimesikia Magufuli akihimiza;
1. watanzania wafanye kazi kwa bidii.
2. Akikusanya kodi kwa umakini haswa biashara kubwa.
3. Akihamasisha viongozi kuwa makini na kutengua pale inapotakikana.
4. Ni mfuatiliaji wa kila jambo.
5. n.k. n.k.
Nimeona ameanza na kuimarisha ukusanyaji kodi, ikiwa na maana kubwa sana;
1. Utakapokuja kumwezesha mwananchi, tayari anakuwa anaelewa kila kinachoendelea kuhusu kodi na mambo mengine ya kiserikali.
2. Lazima asafishe huduma za kiserikali ndio arudi kwa wananchi watakaopewa huduma zenyewe.
3. Serikali ndio huongoza watu, sio watu kuiongoza serikali. Tutakapoona matumizi yamebanwa, serikali inajali wananchi, sheria inaheshimiwa na viongozi na watawala, itarahisisha mwananchi kuheshimu na kuisikiliza serikali yake!!  Unaanzaje kumwelimisha mwananchi unaemwibia kuhusu ulipaji kodi??? Ila anapoona hatua zinachukuliwa kama anavyofanya Magufuli, lazima alipe kodi!!! Logic applied.
Naamini miezi 4+ bado ni kipindi kifupi tukimhukumu kwa kila kitu. Ameanza vizur. Kama uongozi wa ngazi za juu unafanya kazi kw kasi ya Rais, na hawa wa chini watafuata nyayo!!!
Utasikia DC amepishana na hao ma-afisa kilimo, ujenzi, e.t.c. e.t.c. tulikuwa tunatafuta kichwa, na kimepatikana!!!!
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


0 comments:

Post a Comment