Tuesday, 1 September 2015

Re: [wanabidii] WANANCHI WAFANYE NINI WASHINDE UCHAGUZI 2O15

Huyu ni aliyekuwa mtetezi wa haki z a wanawake na watoto na kugeuka mtetezi fanatic wa mafisadi

On Sep 1, 2015 5:52 PM, "'mokili juma' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Sawa dadangu Nkya. Nimeisoma makala yako ndefu kuhusu "Wananchi wafanye nini washinde Uchaguzi 2015". Lakini ajabu ukiingia ndani unaongelea haja ya Wananchi kuiondoa CCM kwa Kupiga Kura mwaka 2025!!!!!
Nakushauri tena, Tulia dadangu......... Acha jazba!!!  Unapoandika makala jaribu kumpa mtu mwingine mmoja ama hata ikiwezekana, wawili ili waisome na kufanya masahihisho kabla ya "kuipost" kwa wasomaji. Badilika Anna!



On Tuesday, September 1, 2015 5:26 PM, 'ananilea nkya' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:


WANANCHI WAFANYE NINI  WASHINDE UCHAGUZI 2015?
Na Ananilea  Nkya

Mmoja wa  watu waliosoma  makala yangu Raymond Mauki, makala  niliyoandika  kwamba CCM ilimtoa  Edward Lowassa kafara  kwa kumpakazia ufisadi  wa Richmond  ili chama hicho  kidanganye wananchi kwamba fisadi ni Lowassa  na CCM ni chama safi, amenishukuru kwa mchango wangu kwa taifa  kupitia ile makala. Baada ya kuisoma ameniomba nijubu  maswali mawili.

Kwenye malaka hiyo iiliandika  kwa serikali ya CCM ndiyo fisadi wa  fedha za umma na hivyo chanzo cha wananchi wengi hapa nchini kuwa maskini.  Nilitoa mfano wa serikali ya CCM kuwa fisadi  kusimamia  wizi wa fedha za umma kwenye  akaunti ya Tegeta Escrow shilingi bilioni 306 mwaka jana 2014. Nilitoa pia mfano wa ufisadi wa Richmond kwamba ni serikali ya CCM yenyewe  ilihusika lakini walidanganya umma kwamba muhusika ni Edward Lowassa.

Uthibitisho ni kwamba kama Lowassa ndiye alikuwa  fisadi wa Richmond leo hii angekuwa yuko jela kama Mramba na Yona.  Nilisema pia kwamba hivi sasa  nchi imejaa ufisadi unaofanywa na  watawala wa serikali ya CCM kwa hiyo hata mgombea wa CCM wa sasa John Pombe Magufuli  wanayejidai  ni mtu msafi akichaguliwa  yerikali yake italazimika kufanya ufisadi penda asipende.  Na yeye mwenyewe  Magufuli amekaririwa akisema  kwamba ataika mfano marais waliomtangulia.
 
Kwa hiyo nikawashauri wananchi wapiga kura wakiwepo wanaCCM  kwamba kama wanataka nchi yetu iondokane na ufisadi wa fedha za umma na jeuri ya watawala wa CCM kujitajirisha huku wananchi wengi wakiwa ni maskini wa kutupa, na tena  watawala hadi kufikia kuwatukana wananchi masikini kwamba ni  malofa na wapumbavu ni lazima  wananchi wafanye mabadiliko—waiondoe CCM madarakani mwaka huu 2025  kwa kutumia sanduku huru la kura  hapo tarehe 25 Oktoba .

Maswali mawili ambayo msomaji wangu alitaka niyajibu  ni haya  ifuatavyo:
Swali la kwanza: Nini mchango wa wanawake kwenye harakati hizi za  leo,unadhani wameamka kiasi cha kutosha?

Mchango wa wanawake katika kuleta mabadiliko katika maisha yao kupitia  uchaguzi wa mwaka huu 2015  ni mkubwa na muhimu sana. Wanawake kwa wingi wao  wakijitokeza kusikiliza kampeni za uchaguzi kisha wakijitokeza kupiga  kura na wakaipigia kura UKAWA  wataleta mabadiliko.  Hivyo kila mwanamke aliyejiandikisha kupiga kura, namshauri atunze kitambulisho chake  cha kupiga kura(kichinjio). 

Afanye hivyo kwa  kutokukubali kumuonyesha mtu yeyote kitambulisho chake. Kitambulisho chako ni siri yako  (ni silaha yako) ya itunze kama mboni ya jicho hakuna mtu mwingine yeyote hata kama ni kiongozi, hata kama ni polisi au mgambo  hapaswi kukiona kitambulisho (kichinjio)n chako.  Zaidi hata kama huyo mtu atakuwa amekuletea zawadi ya kanga, kitende, fulana, sukari, fedha au chochote kile mwanamke USIDANGANYIKE.

Mimi sina chama chochote cha siasa nimefungamana nacho lakini nasisitiza wanawake waipigie kura  UKAWA  kwa  sababu  ilani ya UKAWA ina agenda kuu mbili muhimu zinazogusa maisha ya wanawake moja kwa moja.

Kwanza UKAWA wana  agenda ya kutoa elimu bure hadi Chuo Kikuu. Hili ni muhimu kwa  sababu elimu ndiyo msingi wa maendeleo yote kwa mtu binafsi wakiwopo watoto wa kike, familia na taifa zima. 

Pili  UKAWA wana agenda ya  kuandika Katiba  Mpya inayotokana na  maoni ya wananchi.  Moja ya jambo muhimu katika Katiba  ya wananchi ni  kuweka uhusiano mpya kati ya viongozi na wananchi. Katiba Mpya itazuia viongozi kujitajirisha  kwa mali za umma huku mamilioni ya wananchi wakiwepo wanawake wakitaabika kwa umaskini.

Fedha za  nchi  zinazotafunwa na watawala wachache zitatumika  kwa mfano  kuboresha  elimu, huduma za afya,maji, umeme,  kujenga viwanda kuwapatia maelefu ya watu  ajira.  Pili Katiba mpya itaweka misingi imara ya kuhakikisha  uwakilishi wa wanawake  kwenye vyombo vya maamuzi unafikiwa asilimia 50/50.

Kashalika Katiba  Mpya italeta usawa wa kweli wa kijinsia nchini na usawa huo utaanza kuonekana dhahiri  uchaguzi wa 2020  kwa kutoa  idadi sawa  wanawake na wanaume  madiwani kwenye kata  na  idadi sawa ya wabunge wanawake na wanaume majimboni. Kadhalika kwenye vijiji na mitaa mwanamke akiwa mwenyekiti mwanaume atakuwa Makamu mwenyekiti.
 
Utaratibu wa viti maaluma utatumika  kwa watu  wenye ulemavu peke yake. Kila aina ya ulemavu itakuwa  mbunge mwanamke na mwanaume.  Hayo ndiyo mabadiliko kamili nay a kweli kuhusu usawa wa kijinsia  unaotakiwa Tanania ili nchi yetu na watu wake waondokane na umaskini.
 
Katika uchaguzi wa mwaka huu kuna vyama  vinajinasibu eti  vimezingatia usawa wa jinsia kwa kuweka mwanamke mgombea mwenza au mgombea wa Urais.  Ni sawa lakini hiyo ni geresha ya danganya toto  kwa sababu kwa mfumo wa sasa ambapo  usawa  wa 50 kwa 50 haujawekewa misingi kwenye Katiba  wanawake  wanatumika tu  kama wanaume  kupitisha sheria na sera za maendeleo za kunufaisha kikundi kidogo cha watawala wananchi wanaume na wanawake wakibaki mafukara wa kuputa.

Usawa wa jinsia  wa  kweli na wa kudumu  hauwezi kufikiwa hapa nchini  bila Katiba Mpya ya wananchi kuandikwa  na kuweka misingi ya kutekeleza  usawa wa jinsia kwa vitendo—misingi inayowaondolea wanawake vikwazo vya kugombea na  kushinda sawa na wanaume majimboni na kwenye kata na siyo viti maalum vya upendeleo—miaka 50 baada ya nchi kupa uhuru. 
Kwa hiyo ushuri wangu kwa wanawake  na wale wote wanaofanya kampeni  UKAWA ni kuwaeleza wanawake na wananchi ukweli kwamba  wakitaka mabadiliko ya kweli katika maisha yao wachague UKAWA  ndio waliobeba ajenga ya ukombozi—agenda ya kuwaletea Watanzania mabadiliko ya kweli yatakayojengwa kwenye misingi imara –Katiba Mpya iliyotokana na maoni ya wananchi. 

Swali la Pili: Watanzania tufanye nini  kuzuia CCM  kuiba kura  uchaguzi wa  mwaka huu 2015?  Mimi napendekeza yafuatayo:

Kwanza: Kila mwananchi mwanamke mwanaume wakiwepo wana CCM mnaouchukia  kuona watu wengi  wanateseka kwa umaskini na watawala wachache wana utajiri wa kupindukia,  kinachotakiwa  kama mnanataka uchaguzi wa mwaka huu uwe ni mwamzo wa kubadilisha maisha  ya kimaskini wanayoishi mamilioni ya Watanzania, ni kutunza kitambulisho  chako (kichinjio)  na siku ya kupiga kura  tarehe 25 Oktoba mwaka huu 2015 kwenda kupiga kura kuchagua UKAWA. Ninaipigia debe UKAWA—umoja unaojumuisha vyama vya CUF, NLD, NCCR Mageuzi na CHADEMA  kwa sababu  wana agenda ya ukombozi wa wananchi.
UKAWA  wana ajenda ya kuandika  Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi. Katiba Mpya itaweka misingi mipya ya kuongoza nchi kuleta mabadiliko-kuondoa umaskinini unaotengenezwa kwa  serikali ya CCM kukwapua fedha za wananchi  na jeuri ya kupora madaraka ya wananchi—yaani CCM kujifanya chama dola. 
Hata kama itakulazimu kusubiri siku mbili au hata wiki nzima hata mwezi mmoja kuweza kupiga kura fanya hivyo usikate tamaa. Kakikisha hukosi kupiga kura  maana hakuna ukombozi  wenye kuleta mabadiliko  katika maisha ya wananchi wengi ambao hupatikana  katika demokrasia ya vyama vingi vya siasa bila wananchi wenyewe  kushiriki  kuleta mabadiliko hayo kupitia sanduku huru la kura.

Umaskini  wa wananchi ninaouzungumza ni pamoja na ukosefu wa ajira ya kuwapatia walio wengi  wasio watumishi wa umma fedha za kujikimu.  Watumishi wengi wa umma  mfano  walimu, madaktari, wauguzi, askari, wahudumu wa maofisa na kulipwa  mshahara isiyokidhi mahitaji  ya msingi kama vile chakula, mavazi na malazi.
 
Kadhalika kulima kukopwa mazao yao na kutolipwa kwa muda mrefu.  Ukosefu wa barabara vijijini, ukosefu wa maji, watu kufa kwa kukosa dawa ili hali watawala wachache  wakiugua  wao wana haki ya kutumia fedha za umma kwenda kutibiwa nchi za nje.

Elimu duni inayosababishwa na shule ambazo si bora hazina  chakula kwa wananfunzi, usafiri, vitabu, maabara na miundo mbinu  mingine muhimu. Shule hazina hazina walimu  wenye ubora na  wanaofurahia kufanya kazi zao kwa vile wanaheshimiwa, kuthaminiwa  na kulipwa vizuri.

Vilevile umaskini na kuporw amadaraka wananchi kunakojidhihirisha kwa vyombo vya  dola  hasa polisi  kutumika  kibabe kunyanyasa wananchi kama vile nchi yetu bado iko kwenye ukoloni.

Pili: Kila  kila Mtanzania aliyejiandikisha kupiga kura anayeumwa na hali ya umaskini wa wananchi wengi  anapaswa kutunza kitambulisho chake cha kupiga kura (kichinjio) na asikubali kumuonyesha au kumpa mtu yeyote hata awe mwenyekiti nyumba kumi, mwenyekiti wa kitongoji, kijiji, mtaa , polisi  , mgambo au  mtu yeyote yule.
Hii ni muhimu maana wapo watu hivi sasa  wanapita nyumba kwa nyumba wakijidai wanafanya kampeni za nyumba kwa nyumba kumbe ni mbinu za kuwanunua au kuwadanganya na kuwaogopesha wananchi wanaotaka mabadiliko  ambao Rais Mstaafu Benjami Mkapa amewaita ''MALOFA NA WAPUMBAVU''.

Lengo la kuwadanyanga au kuwatia woga wananchi ni ili  wasipige  kura  ya kuwaletea mabadiliko  kwa kuikataa CCMambayo utawala wake  umewafanya wananchi wengi kuwa malofa na wapumbavu huku watawala wa serikali  ya CCM wakijilipa fdha za wananchi  na kupata utajiri  wa kukufuru.

Nawashauri wapiga kura kama ni fedha, nguo, chakula  watakuwa wanaletewa na CCM wakati wanapita kwenye kampeni walizosema watafanya nyumba kwa nyumba zipokeeni  maana pengine  hizo ni zile fedha za wananchi zilizoibiwa mwaka jana 2014 kwenye akaunti ya Tegeta escrow  Benki kuu ambazo nyingine zilibebwa kwa  tandarusi. Ni fedha za wananchi kuleni na kama ni nguo vaeni  ni mali yenu lakini usimpe tena kura yako maana atarudi tena kwenda kukwapua nyingine na hakuna kazi yoyote kuwaondolea wananchi umaskini  wataifanya miaka 5 ijayo.

Aidha kila anayepiga kampeni UKAWA  awaeleze wananchi ukweli huu. Wananchi wakiujua ukweli  kuhusu chimbuko la matatizo yanayowakabili  kuwa ni  serikali ya CCM kama taasisi kujihusisha na ufisadi na kuwapora wananchi madaraka,  wananchi wataelewa na watapiga kura  kikamilifu kuleta mabadiliko—kuchagua  UKAWA  kuendesha serikali tuone miaka mitano nao watafanya nini kuwaondolea wananchi umaskini. Wasipotimiza ahadi zao hasa —elimu bure hadi chuo kikuu na Katiba Mpya  uchaguzi wa 2020 watapigwa chini kupitia sanduku huru la kura . Bila kubadilishana vyama  kwa kuzingatia sera za maendeleo  umaskini unaowasumbua Watanzania wengi hautaondoka nchini.

Tatu: UKAWA viweke mawakala wenye uchungu na  maisha  ya mamilioni ya Watanzania. Mawakala ambao hawahongeki, hawadanganyiki. Mawakala wa UKAWA wanatakiwa wawe ni watu  wanaoweza kuvumilia njaa na wanaoweza kukesha hadi kazi ya kupiga, kuhesabu kura na kutangaza mshindi  ikamilike. Maana kwenye uchaguzi  wakala  ukipepesa ukipepesa macho kidogo tu wajanja wanachakachua.

Nne:  UKAWA kuweka mawakala makini  ambao siyo mamluki wa CCM-- watu  jasiri (siyo watu waoga) na wanaojua kusoma, kuandika na kuhesabu na wenye moyo wa kujitolea kwa faida ya walio wengi wanaoteseka  na maisha duni.  Kura ni hesabu kwa mtu asiyejua kusoma,  kuandika  na kuhesabu ni rahisi sana KUDANGANYIKA  maana hataweza kusoma na kuelewa kilichoandikwa.

Tano: UKAWA kuweka mawakala wenye uvumilivu—mtu ambaye anaweza kuvumilia njaa ikibidi  kukaa  bila kula  na kunywa  kwa zaidi ya  saa 24. Wako mawakala chaguzi zilizopita kwa kuendekeza ulaji na unywaji  wakiwa kazini kwenye vituo vya kupiga kura, waliagiza vinywaji na  vyakula na vinywaji. Lakini wajanja  waliweka kwenye vyakula na vinywaji hivyo  dawa za usingizi. Baada ya kula walijikula na  walikuja kuamka  uchaguzi  ulikuwa umewisha  na  kura za mgombea wao ambaye alikuwa anapendwa  na watu amekwishaibiwa kura zake wakiwa usingizini.

Ninachosema hapa ni kwamba  uchaguzi ni wa mwaka huu ni mapambano ya mamilioni ya wananchi masikini (wakiwepo wanaCCM wengi tu)  na kikundi cha watawala wa CCM wanaoendelea kujitajirisha kwa kuwa madarakani.

Hivyo mamilioni ya wananchi wanaoteseka na umaskini wakiamua kuvishinda vishawishi na ulaghai unaofanywa na watawala wa CCM  uchaguzi wa mwaka huu utaleta mabadiliko kwa mara ya kwanza kuwezesha mfumo wa vyama vingi kufanya kazi Tanzania. Zaidi fursa ya mamilioni ya wananchi  wanaoishi maisha ya kimaskini kushinda uchaguzi wa mwaka huu 2015  ni kubwa  kuliko wakati mwingine wowote katika historia ya vyama vingi nchini kwetu.

Sita:  UKAWA  wahakikishe inawaelekeza  mawakala wake mambo muhimu ya kufanya wakiwa kwenye vituo vya kupiga kura.  Mambo hayo ni pamoja na  kuhakikisha wanachukua kwa usahihi matokeo kwenye vituo na kisha wafuatilie kwenye halmashauri kuhakikisha anayeshinda ndiye anatangazwa mshindi.

Umuhimu wa kufuatilia hadi matokeo yatangazwe ni kuhakikisha waliopewa mamlaka kutangaza matokeo ya diwani, mbunge na Rais hawachakachui matokeo. Umma  ukiwa unafuatilia matokeo-wenye kutaka kufanya mchezo mchafu watauogopa umma. Hakuna kinachoshinda nguvu ya umma. MUNGU IBARIKI TANZANIA. 

Ninaruhusu Makala hii ichapishwe na yeyote anayetaka. Lengo ni kuelimishana  ili kuleta mabadiliko . Ukiwa na swali: niandikie:  ananilea_nkya@yahoo.com



Ananilea Nkya
 E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com

--------------------------------------------
On Sat, 8/22/15, 'raymond mauki' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: [wanabidii] Re: [Wanazuoni] LOWASSA KAFARA CCM KUJARIBU KUZUIA MABADILIKO [1 Attachment]
To: "Wanazuoni@yahoogroups.com" <Wanazuoni@yahoogroups.com>, "mabadilikotanzania@googlegroups.com" <mabadilikotanzania@googlegroups.com>
Cc: "WANA BIDII" <wanabidii@googlegroups.com>, "Paschally Mayega" <ngowe2006@yahoo.com>
Date: Saturday, August 22, 2015, 5:11 AM


Mama Nkya nimekuelewa sana
sana na sana, siku zote nimekuwa nikifuatilia harakati zako
ila sikujua msimamo wako uko wapi. Nashukuru kwa kuwaambia
watanzania kuwa kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni yake
haijalishi yupo wapi, ana nafasi gani kwa jamii au yupo
upande gani kisiasa. Ulichokiandika ni very simple and very
true hata mtoto wa darasa la nne ataelewa ila cha ajabu kuna
wasomi watakuja kupinga na wanaendeta kupinga ulichokiandika
tena wakitumia data za uongo kabisa. Ni ukweli uliowazi kuwa
watanzania wa leo sio wa mwaka 1995 wa Mrema na nashukuru
yeye mwenyewe amekiri hilo juzi kupitia kituo kimoja cha
redio(clouds fm), watanzania wa leo wanahitaji mabadiliko
chanya na wasipoyapata kwa amani basi watatumia njia
nyingine yoyote japo hatupendi ifike huko.Mama
Nkya, naomba ukipata muda unijibu haya mawili, 
 Je, tufanye nini watanzania lei hii ili kuzuia kabisa
mchezo wa ccm kutuibia kura zetu kwenye uchaguzi mkuu?
Ukizingatia wameshakiri kabisa watatumia njia yoyote
kushinda ikiwemo goli la mkono.Pili,
nini mchango wa wanawake kwenye harakati hizi za
leo,unadhani wameamka kiasi cha kutosha? 
Asante
na ubarikiwe sana,
RAYMOND
MAUKIKIGAMBONI,
DAR ES SALAAM.

  From:"ananilea nkya
ananilea_nkya@yahoo.com [Wanazuoni]"
<Wanazuoni@yahoogroups.com>
Date:Fri, Aug 21, 2015 at 23:42
Subject:[Wanazuoni] LOWASSA KAFARA CCM
KUJARIBU KUZUIA MABADILIKO [1 Attachment]

 
 



 


   
     
             
        [Attachment(s) from ananilea nkya
included below]
       
     
      LOWASSA KAFARA CCM KUJARIBU KUZUIA MABADILIKO

 

Na Ananilea Nkya



Nimeandika  hoja hii baada ya kusoma na kusikia  hoja
zinazotolewa na  baadhi ya Watanzania kwamba  eti CHADEMA ,
CUF, NCCR-Mageuzi  na NLD  -vyama vinavyounda UKAWA kwa
kumsimamisha  Edward Lowassa kugombea Urais  vimepoteza
usafi  wa kuongoza  mapambano dhidi ya ufisadi.



Ukweli ni kwamba viongozi wa CHADEMA na UKAWA kumsimamisha
Lowassa kuwa mgombea urais wamecheza kama Pele. Tena
wanastahili pongeze kubwa maana walitumia akili kali na
saikolojia ya hali ya juu kubaini kuwa CCM ilikuwa ilicheza
mchezo mchafu kisiasa kuwatumia wapinzania kumpakazia
Lowassa ufisadi na hatimaye CCM kupata nguvu ya kumtoa
Lowassa kafara ili eti CCM ionekane inajisafisha ufisadi.




Wanaodhani CHADEMA na UKAWA wamekosea pengine hawajaelewa
kuwa  tangu upepo wa mabadiliko  wa kukataliwa mfumo chama
kimoja kuwa madarakani kwa muda mrefu ulipoanza kuvuma
duniani kote mwishoni mwa miaka ya 1980,  baadhi ya wanaCCM
hawajakubali kwa dhati kabisa  ukweli huo na kuamini kwamba
CCM inaweza  kupunzishwa kuongoza nchi angalao kwa miaka
mitano.



Hasa baada ya Mwalimu Nyerere CCM kuondoka duniani, CCM
imebaki na viongozi ambao hawako tayari kutumia ujasiri
kuongoza mabadiliko kwa amani.  Baadhi ya vongozi wanaojali
zaidi maslahi ya wana CCM wachache wanaotumia kauli kama
hirizi kauli aliyowahi kuitoa Mwalimu Nyerere kuwa bila CCM
imara—Tanzania itayumba kujidanganya wenyewe na kudanganya
wananchi.



Wanasahau kwamba Mwalimu Nyerere kama mwanafalsafa na
mwanasiasa makini alikuwa anatoa maamuzi ya kijasiri kwa
faida ya taifa na wananchi kulingana na hali halisi ya
wakati husika kwa kusoma upepo wa wananchi. Kwa mfano
Nyerere aliwahi kusema CCM si mama yake akimaanisha Tanzania
na Watanzania ni muhimu zaidi kuliko umuhimu wa CCM kuwa
madarakani.



Mfano Mwalimu Nyerere mwaka 1992 alionyesha mfano kwamba
maslahi ya nchi na wananchi ndiyo muhimu kuliko maslahi ya
CCM alipokubali kwenda kinyume na uamuzi wa wanaCCM wengi
waliokuwa wamekataaa—mabadiliko—kuanzishwa vyama vingi
nchini ili vyama vibadilishane uongozi wa nchi --kuharakisha
maendeleo ya wananchi.



Lakini baada ya Mwalimu kuondoka dunaini kila mwanaCCM
anayechaguliwa kuwa Rais, kwa kuogopa kulaumiwa kwamba eti
kama CCM haitachaguliwa kupitia sanduku huru la kura atabeba
lawama za kufanya CCM iondoke madarakani, serikali zote za
CCM baada ya Mwalimu Nyerere kuondoka duaniani zimekuwa
zinajihusisha na ufisadi.



Serikali ya CCM imekuwa ikikwapua kwa wizi wa wazi mabilioni
ya fedha za umma na kufanya maovu mengine mengi kuhakikisha
CCM haiondoki madarakani. Hivyo chaguzi zinafanyika kama
geresha tu—kudanganya wafadhili na mataifa kuwa Tanzania
ni nchi ya demokrasia ya vyama vingi.



Mfano uchaguzi wa mwaka 2005 serikali ya CCM chini ya Rais
Mkapa ilikwapua fedha za wananchi kutoka Benki Kuu Akaunti
ya EPA shilling bilioni 133 ambazo ziliiwezesha CCM kumweka
madarakani Rais Kikwete.



Mwaka jana 2014 serikali ya CCM chini ya Kikwete ilikwapua
shilingi bilioni 306 kutoka akaunti ya Tegeta escrow Benki
Kuu kwa ajili ya kuiwezesha CCM kushinda uchaguzi wa
serikali za mitaa na uchaguzi mkuu unaofanyika tarehe 25
Oktoba mwaka huu 2015.



CCM wakishaingia madarakani jambo muhimu kuliko yote Rais na
serikali yake analolifanyia ni kubuni ufisadi wa kuipatia
CCM fedha na mbinu nyingine za kuiwezesha CCM ibaki
madarakani uchaguzi unaofuta. Hakuna kazi muhimu ya
kuwaondolea wananchi umaskini inayofanyika kwa kiwango na
juhudi kubwa.



Kwa sababu hiyo,  kikundi kidogo cha watawala, wengi wakiwa
ni kutoka CCM na familia zao wamejikuta wakinufaika kwa kuwa
  matajiri kufuru kwa muda mfupi ili hali  wananchi wengi
wakibaki maskini na mafukara wa kutupa.



Mfano  wabunge (kikundi cha watu wasiozidi 400) wengi wakiwa
  ni wanachama wa CCM  kila mmoja analipwa si chini ya
milioni  10 kila mwezi kama mishahara, wacha marupurupu  na
posho za vikao vya kamati, posho za safari na  mamilioni
mafao kila baada ya miaka mitano.  Lengo wawe na fedha
nyingi za kununua kura za wapiga kura maskini uchaguzi
unaofuata CCM ibaki madarakani.



Ndiyo sababu kila mwananchi wakiwepo watu muhimu kama walimu
wa vyuo vikukuu na madaktari hivi sasa nao  wameamua kuwa
wanasiasa.



Zaidi baadhi ya wanaotafuta madaraka ya kisiasa wanatumia
mbinu chafu sana  ikiwa ni pamoja na ushirikina wa kuuwa
watu wenye ulemavu wa ngozi (albinism) waweze kupata nafasi
ya kuingia katika kundi la  watawala—kupata utajiri wa
kutisha katika kipindi cha miaka mitano.



Mfamo Wabunge waliomaliza muda wao mwaka huu 2015    kila
mmoja ameondoka na kiinua mgongo zaidi ya shilingi milioni
200.  Hii ni kufuru katika nchi inayojinasibu kuwa ni
maskini na inapita huko na huko duniani kuomba misaada!



Hata hivyo kwa kadri ufukara unavyoendelea kuwatafuna
wananchi wengi, na kwa kadri uelewa wa  wananchi
wanaoteseka kwa  umaskini  unavyoongezeka kwamba CCM na
utawala wa  serikali yake ndicho chanzo cha umaskini wao,
CCM  imebaini kuwa haiwezi tena  kushinda uchaguzi kupitia
sanduku huru la kura kwa kutegemea kete moja tu—kununua
wananchi mafukara  peke yake.



Hivyo katika miaka ya hivi karibuni CCM imeanza kuendesha
siasa za maji taka—kuchafuana wao kwa wao na hatimaye
wameamua kutoana kafara-lengo kuu likiwa ni kuzuia wananchi
wasitumie sandundu la kura kufanya mabadiliko—kuchagua
vyama vingine kuongoza nchi. 



Hivyo Rais Kikwete, hata kama ndani ya umungu wa moyo wake
hakubaliani na CCM inavyotumia ubabe kukataa mabadiliko
kinyume na asili ya binadamu, amekuwa akifanya mambo
kutimiza matakwa ya baadhi ya wanaCCM —kujaribu kuzuia
mabadiliko—ili tu kuepuka lawama- amalize muda wake bila
kuonekana ndiye kasababisha wananchi kuipunzisha CCM uongozi
kwa kipindi cha miaka mitano.

 

Kwa kufanya hivyo Rais Kikwete amejikuta akiporwa ujasiri
wake aliokuwa nao kama mwanasiasa  ambaye Mwalimu Nyerere
alimuamini.



Kumbuka Mwalimu Nyerere alinukuliwa na gazeti la  Nipashe na
Majira 26/5/95 akisema  baada ya Rais Mwinyi  baadhi ya
vijana ambao alikuwa anaona wana nia ya dhati kabisa  na
uwezo mkubwa wa kuongoza Tanzania  ni Benjamin Mkapa, Jakaya
Kikwete na Edward Lowassa.

Lakini kwa Kikwete kukubali kuyumbishwa na wana CCM wachache
wasiokubali mabadiliko anaonekana kufumbia macho utekelezaji
wa kile mwanafalsafa Mwalimu nyerere alichokisema---kwamba
Watanzania wanataka mabadiliko.



Mfano Rais Kikwete alipata fursa ya kusimamia mabadiliko kwa
kuandika Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi.
Lakini kikundi kidogo cha wahafidhina ndani ya CCM
kilimtisha akajikuta anaweka pembeni ujasiri wake aliokuwa
nao wa kusimamia mabadiliko hayo muhimu kwa maendeleo ya
taifa hili.



Kama uamini jiulize ni kwa  nini  Kikwete aliachia Bunge la
Katiba lililojaa asilimia 80  ya wanachama likazika Rasimu
ya Katiba ya wananchi pale Dodoma mwaka jana 2014  -- Rasimu
ambayo ingeleta Katiba yakuweka  misingi ya kuleta
madadiliko Tanzania—mabadiliko ya kuhakikisha kikundi
kidogo cha watawala hakijitajirishi kwa ufisadi na kujigawia
mali  za umma huku mamilioni ya wananchi wakibaki maskini na
mafukara wa kutupa?



Baada ya Kikwete kupoteza fursa  ya kuleta mabadiliko  kwa
kuandika Katiba Mpya,  umma uliofukarishwa  umeendelea
kupata uelewa kuwa CCM na serikali  yake ndicho chanzo cha
umaskini wao. 



Hivyo ili kuendelea  kubaki madarakani  serikali ya CCM
imekuwa  ikijihusisha na ufisadi ili ipate fedha za
kuwarubuni walala hoi wakati wa kampeni za uchaguzi.



Mfano mwaka 1995 Rais Benjamini Mkapa alijikuta serikali
yake ikifanya ufisadi  katika  akaunti EPA (bilioni 122)
zilizotumiwa na CCM kumuweka  Kikwete madarakani.



Ukitafakari utaona kwamba katika ufisadi Tegeta escow,
serikali ya CCM imekapua billion 306 mara tatu ya ufisadi wa
EPA mwaka 1995 ilipokwapua bilioni 122 ili kipate fedha
nyingi zaidi la kuwalaghai wapiga kura mafukara ambao
wameendelea kupata uelewa kuwa CCM inaiba fedha za umma
kununua wapiga kura wakati wa kampeni za uchaguzi.



Hivyo serikali ya CCM inayoongozwa na Kikwete ambayo
imeshuhudia nguvu ya wananchi kudai mabadiliko ikiwa kubwa
kuliko wakati mwingine wowote, inajaribu kila mbinu chafu na
safi ili CCM ibaki madarakani baada ya uchaguzi mwaka
huu.



Ndiyo sababu  serikali ya CCM  kupitia msemaji wa chama
hicho Nape Nnauye imeanza kuwaambia Watanzania kuwa  CCM
lazima ishinde uchaguzi wa mwaka huu hata kama ni kwa
kutumia goli la mkono (wizi au lolote lile chafu).



Zaidi  Rais  Kikwete  amefikishwa mahali  pabaya
kulazimika  kubuni  mchezo  mchafu kujaribu kuwadanganya
Watanzania  kuwa eti  CCM na serikali yake ni safi,
haijihusishi na ufisadi unaofukarisha wananchi isipokuwa
wanachama wachache wa CCM ndio mafisadi.

 

Ili  kujaribu kutafuta kujenga  uhalali wa CCM kubaki
madarakani baada ya uchaguzi wa  mwaka huu 2015, Kikwete
amejikuta akilazimika  kumtoa  kafara Lowassa  kwa
kumpakazia  ufisadi wa  Richmond.



Wananchi wanauliza kama Lowassa alikuwa ndiye mhusika  wa
Richmond  ni kwa nini  Spika wa Bunge  Anna Makinda (mmoja
wa watawala  wa CCM),  hakuagiza  tume ya Bunge iliyoongozwa
na Mbunge wa CCM Harrison Mwakyembe kumhoji Waziri Mkuu
Edward Lowassa?

 

Pili wananchi wanahoji kama CCM haijamtoa Lowassa kafara
kwa kumbebesha ufisadi wa chama hicho  ili kupumbaza hasira
ya  wananchi dhidi ya ufisadi wa CCM kwenye uchaguzi wa
Oktoba mwaka huu 2015  ni kwa nini  Rais Kikwete alikubali
Waziri wake Mkuu  Edward Lowassa  ajiuzulu kwa ufisadi wa
Richmond 2008 wakati ufisadi wa kutisha  ulifanywa na
serikali ya CCM kwenye akaunti ya Tegeta escrow 2014
Kikwete aliwatetea mawaziri  waliogawiwa fedha hizo na Ikulu
ilikuwa ndiyo mtuhumiwa namba moja?

 

Mimi si mwanasiasa wa chama chochote cha siasa hapa nchini
ninachoangalia ni chanzo cha umaskini wa wananchi wengi
Tanzania.

 

Ndiyo sababu Watanzania wengi nikiwepo mimi mwenyewe kwa
sababu  tulipewa habari nusu nusu zilizotolewa kimkakati na
serikali ya CCM kuhusu kashfa ya Richmond  kumpakazia
Lowassa ufisadi, tulipubwazwa tukaisaidia CCM  kumchafua
Lowassa kuwa ni fisadi wa Richmond. 



Lakini baadhi ya wananchi walianza  kujua kuna ukweli
uliofishwa kuhusu Richmond pale TV moja ilipokuwa imemwalika
Lowassa aotoe yake ya moyoni live siku chache baada ya
kujiuzulu, lakini kipindi hicho cha TV kikafutwa ghafla.

 

Hata hivyo ukweli huo umekuja kujulikana mwezi Julai mwaka
huu Lowassa alipotoa hadharani baada ya kuachana na CCM na
kujiunga na CHADEMA.



Sasa wananchi    wamefahamu kuwa  CCM  chini ya serikali ya
Rais Kikwete iliamua kumtoa Lowassa kafara kwa kumpakazia
ufisadi wa  Richmond  ili  kuiokoa CCM isiadhibiwe vikali
na wananchi kwenye sanduku huru la kura  –kwa ufisadi
alinawasababishia umaskini na ufukara.



Ndiyo sababu  hivi sasa  CCM na baadhi ya wanahabar
wanapakazia  CHADEMA  na  UKAWA  kuwa  eti ni mafisadi 
baada ya kumpokea Lowassa (kafara wa CCM)  na  kumpitisha
kuwa mgombea wa  Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.




Isitosha hivi sasa kikundi  cha watawala wachache wa
serikali ya CCM wanahaha na wanamzonga Kikwete azuie
mabadiliko kwa mkono kwa  kufanya kila uchafu  kupumbaza
Watanzania kwa kutumia kete ya eti  Lowassa ni  fisadi wa
Richmond  hivyo hana sifa ya kugombea Urais wa Tanzania,
bali Magufuli ndiye mtu safi.



Wananchi wenye akili zao wanajiuliza hivi mwenye kashfa za
kifisadi kati ya Lowassa na Magufuli ni nani?  Ni Lowassa
aliyepakaziwa Richmond au ni Magufuli aliyeongoza watawala
kujiuzia kwa bei chee nyuma za umma zilizogarimu wanannchi
mabilioni ya fedha?



Wananchi pia wanajiuliza kama Lowassa ni fisadi wa Richmond
ni kwa nini serikali ya CCM haijamshitaki mahakamani miaka
minane tangu ufisadi huo ulipotokea?



Hivyo  pengine  baada ya Lowassa kutafakari nafsi yake na
kuona kuwa CCM imemtoa kafara asigombee Urais  ili kuzuia
mabadiliko, ameamua kufanya  maamuzi magumu  ya kuhama CCM
--kushiriki kuongoza masikini  na mafukara  wanaotafuta
mabadiliko.



Lowassa ameamua kutekeleza alichokitabiri Mwalimu Nyerere
kwamba CCM isipokubali kuongoza wananchi wapate mabadiliko
wanayoyataka—wananchi watayatafuta mabadiliko hayo  nje
ya CCM.



Ni dhahiri CCM ilipoteza fursa adimu ya kuongoza wananchi
kwenye kuleta mabadiliko kwa kuandika Katiba  Mpya-- kuweka
misingi ya kukomesha mfumo wa utawala  unaowezesha watawala
kuwa matajiri wa kupindukia  huku mamilioni ya wananchi
wakiwa mafukara na nchi ikinuka aibu ya umaskini  wa
kijitakia  ikiwa rasilimali nyingi za asili.



Wanaomchochea Rais Kikwete asikubali mabadiliko yachukue
mkondo wake, wameunda timu ya kampeni yanye wajumbe wengi
waliohusika kumpakazia Lowassa ufisadi wa Richmond ili eti
kwenye kampeni waendelee kumpaka ufisadi  Lowassa, CHADEMA
na UKAWA wakidhani Watanzania hawana akili ya kutafakari.



Lengo lao ni moja. Wanajua kabisa kuwa kwa kutumia sanduku
huru la CCM  haiwezi kuchaguliwa. Wanataka kutumia
kisingizio  kuwa  CHADEMA  na UKAWA imechafuka eti kwa
kumsimamisha Lowassa Urais  ambaye CCM imemtoa karafa –
kwa kumpakazia ufisadi wa Richmond.

Lakini baada ya kupata salamu za wananchi kupitia mafuriko
yao kwenye kumtambulisha Lowassa kwamba wao wanaelewa fisadi
kamili ni CCM, sasa CCM imeshtuka imeanza kutumia polisi
kuwaadhibu wananchi. Pengine baadaye itatumia jeshi
kabisa.



Zaidi imeamua kujaribu kampeni za  ardhini -nyumba kwa
nyumba, bila shaka kutumia mabilioni ya fedha serikali ya
CCM ilizokwapua Tegeta escrow kununua shahada na kura za
mafukara.

 

Kwenye kampeni za  nyumba kwa nyumba mtu kwa mtu ndiko
ufisadi mbaya wa kisiasa unakofanyika—kununua, kutisha na
kuumiza    wananchi mafukara.

Swali ni je Watanzania wangapi wapiga kura watakubali CCM
inapopita majumbani mwao kuuza shahada zao  kwa sukari,
kanga au fedha hata kama CCM itaamua kumpa kila mpiga kura
shilingi milioni moja?

 

  Ni mpiga kura gani atakayekubali KUDANGANYIKA  kwa
kununuliwa na  CCM  kwa vijizawadi vya fedha nguo KUSALITI 
mamilioni ya watanzania  wanaoendelea kuteseka  kwa ufukara
kila baada ya uchaguzi kwisha na CCM kubaki madarakani?



Wananchi  pia wanauliza je mabilioni ya escrow yatawanunua
wajumbe wa NEC ili  wavuruge daftari la wapiga kura, au
wachakachue kama uchaguzi wa 2010  au wataharibu daftari la
wapiga kura, mashine  na vifaa vya kupigia kura, au
kuchelewesha kwa makusudi kufungua vituo vya wapiga kura
ili  kuvuruga uchaguzi CCM  ishinde kwa goli la mkono?

 

Kadhalika wananchi wanauliza wanaomshinikiza Kikwete
asikubali mabadiliko wakiona hilo haliwezekani je watamuua
Lowassa waliomtoa kafara au  viongozi wa CHADEMA na UKAWA
waliompokea Lowassa na kumwezesha kufikia azma yake ya
kujitolea kuwatumikia watanzania  ili kuvuruga uchaguziwa
mwaka huu?



Wananchi wanauliza maswali hayo  baada ya kubaini kwamba
huenda  wasiomtakia mema Kikwete astaafu kwa amani
wamejaribu kuwalaghai baadhi ya viongozi wakuu wa UKAWA ili
kujaribu kuvuruga UKAWA – lakini UKAWA kwa vile ni sauti
ya mafukara-sauti ya umma  imeendelea kuwa moto mkali wa
nyika  dhidi ya CCM.

 

Hivyo binafsi namshauri Rais Kikwete akubali kuwa baba wa
pili wa Taifa hili baada ya Nyerere kuondoka. Akubali
kusimamia wananchi watumie sanduku huru la kura kwenye
uchaguzi wa mwaka huu 2015 kupata mabadiliko ya uongozi
wanayoyataka.



Wananchi wana imani na UKAWA  kwamba wakiingia madarakani
Katiba mpya inayotokana na maoni ya wananchi itaandikwa.



Huo utakuwa ni mwanzo wa mabadiliko wanayoyataka
wananchi—kuhakikisha watawala hawajitajirishi kupindukia
kufisadi fedha za wananchi huku wananchi wengi wakibaki
mafukara.  CHADEMA  na UKAWA  wasipotimiza hili na kuonyesha
  kwa vitendo maendeleo watakayokuwa wameyaleta kwa miaka
mitano, ni lazima wananchi watatumia sanduku la kura
kuwapunzisha.



Ninaamini ni wenye kutetea maslahi binafsi tu ndiye
atakayemlaumu Rais Kikwete kwamba eti CCM isipochaguliwa
Oktoba 25, Kikwete atakuwa ni chanzo  cha wananchi kuamua
kuipunzisha CCM  kwa miaka mitano.

 

Nitakuwa wa kwanza kuwapinga watu hao na kumtetea Kikwete
hata kama ni kwa kuamua  kuingia kwenye siasa  kwa kujiunga
na CCM .

 

Hakika Rais Kikwete  ukisimamia  wananchi  wazungumze kuhusu
hatma ya uongozi wan chi yao kwa kutumia sanduku huru la
kura  bila CCM kuingiza  mkono mchafu, wewe mwenyewe
ukistaafu utaishi kwa amani na furaha huku baadhi yetu
tukikuona kama baba wa Pili Taifa taifa hili, baada ya
Mwalimu Nyerere.

 

Mwisho ninaruhusu yeyote anayetaka kuchapisha au kutangaza
redioni natelevisheni niyoyoyaandika hapa TV au kuchapisha
na kuwasambazia Watanzania wote popote walipo ujumbe huu
afanye hivyo. Wanawaza kuwasambazia watu mitaani,
kwenyemikutano ya kampeni, mashuleni vyuoni popote
pale—lengo likiwa moja—sote Watanzania tuujue ukweli
kuhusu ufisadi na mchango wake katika kuwafanya Watanzania
waishi katika umaskini.  Lakini muhimu kila Mtanzania ajue
hakuna mshindi wa kujisifu—mshindi ni  nchi yetu Tanzania
na  Watanzania  wote.



MUNGU IBARIKI YANZANIA.



Ananilea Nkya

 E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com

   
     

   
    __._,_.___

            Attachment(s)
from ananilea nkya | View
attachments on the web
   
 
 

          1 of 1 File(s)

         
       
               
      LOWASSA  KAFARA WA
CCM.docx
 
         
   
     

   
       
        Posted by: ananilea nkya
<ananilea_nkya@yahoo.com>       
     
     

   
                          Reply
via web post
                      •
           
                Reply to sender           
          •
           
              Reply to group           
          •
            Start a New
Topic
          •
                            Messages in this
topic
                (1)
                     

       








 




    Visit Your Group

     
      New Members
      2
   
 



 
    • Privacy • Unsubscribe • Terms of Use






   

 
 
 
 



     




     

  .


   


 

__,_._,___






--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment