Pamoja na kuwa nafikiri kuwa Rais Kikwete angeweza kupunguza safari zake lakini ukweli ni kuwa Mbatia ameonyeshqa sura yake asili ambayo ni kinyume na tulivyokuwa tunamuona. Tulimuona kama kiongozi anayetanguliza uzalendo kuliko itikadi. Baada ya kuona UKAWA inayumba ameamua kutumia kila kitu ikiwa ni pamoja na heshima yake. Kwa kweli Mbatia ana kazi kubwa sana kujiosha na huenda ikamgarimu muda kurudia pale tulipomdhania.
--------------------------------------------
On Sun, 9/27/15, fadhil fadhil <fadhil.fadhil96@gmail.com> wrote:
Subject: [wanabidii] Mbatia na Ukawa uzushi na uongo dhidi ya rais Kikwete haviwezi kumpeleka ikulu Lowassa
To: "'Hildegarda Kiwasila' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Sunday, September 27, 2015, 5:43 PM
By
mkulimawakiteto
Kadri siku za kufanya uchaguzi mkuu
unavyokaribia ndivyo tunavyowajua wanasiasa wetu na kuwato
maana kwa
kuwa wamekuwa wakionyesha uhalisia wao kwa kushindwa kuficha
asilia na
hulka zao kwa jinsi walivyo akiwemo Mwenyekiti wa Nccr
Mageuzi Jemsi Mbatia.
Mbatia amekuwa mzushi na
Muongo katika
harakati zake na Ukawa ili kuwaghiribu watanzania
wafanikishe kumpeleka
ikulu Edward Lowassa kwa njia yeyote ile hata kama ni kwa
kusema uongo
ili mradi tu mgombea wao ashinde uchaguzi mkuu bila
kuangalia athari za
maneno yao ya uongo wanayojaribu kuyapandikiza vichwani mwa
watanzania.
Nilikuwa namchukulia Mbatia kama
mwanasiasa mkweli na Mweledi na makini lakini nimekuja kujua
kuwa hayupo
hivyo kama tulivyokuwa tukidhani watanzania wengi, Mbatia amekuwa kama wanasiasa
wengine wachumia tumbo ambao wamekuwa wakipoteza heshima zao
kila kukicha.
Akizungumza hivi karibuni na waandishi wa habari Jemsi
Mbatia
alidai kuwa ktika kipindi cha miaka 10 chenye wastani wa
siku 3,650
Rais Kikwete amesafiri mara 409 na alikuwa akikaa nje ya
Tanzania kwa
wastani wa siku tano katika kila safari hivyo jumla yake
kuwa 2,045.
Mbatia akijumuisha
salafri hizo za rais Kikwete alisema jumla ya asilimia 56 ya
muda wake aliokaa madarakani hadi kufikia sasa, Mbatia
alifika mabali zaidi kwa kusema uongo kwa kusema hgarama
ambazo taifa
imezibeba kutokna na safari hizo kwa mujibu wa safari hizo
ni trilioni
4.5.
Serikali iliingilia kati uzushi huo na Mbatia
na kueleza uhalisia wake. Wizara ya mambo ya nje na
ushirikino wa
kimataifa ilitoa ufafanuzi kuwa tangu rais Jakaya Kikwete
aiingia
madarakani mwaka 2005, kiasi kikubwa kabisa cha bajeti
kuwahi kutengwa
kwa viongozi wakuu rais, makamu wa rais na waziri mkuu ni
shilingi
bilioni 50 ambazo zilitengwa kwa mwaka 2014/2015. Kwa ajili
ya idara ya
itifaki.
Kwa miaka mingine yote imekuwa wastani kati ya bilioni 5
mpaka 25
kulingana na mahitaji ya idara husika ilisema taarifa hiyo
ya wizara ya
mamabo ya nje.
Hebu Tuangalie baadhi ya mafanikio ya safari za rais
kikwete tangu
aingie madarakani, Inawezekana kuwa rais Kikwete ndiye kuwa
ndiye
anayeongoza mara kwa mara kwa safari za kwenda Marekani
kuliko tawala
zote tatu zilizopita.
Katika ziara hizo za Marekani za rais Kikwete, wakati wa
utawala wa
George Bush ulisaidia misaada ya kupambana na maralia dawa
na chanjo na
vyandarua.
Halikadhalika tulipatiwa msaada wa dola za kimarekani
million 700
kupitia mfuko wa milleniam challenge (MCC) fedha ambazo
zimesaidia
ujenzi wa barabara za Mtwara-Masasi-Tunduru Songea hadi
Mbamba Bay na
ile ya Rukwa hadi Sumbawanga.
Pia rais alifanya ziara katika nchi za Brazil na India
ambapo katika
ziara yake ya nchini India ilizaa mradi mkubwa wa kuboresha
miundombinu
ya maji ndani jiji la Dar es Salaam pamoja na ujenzi wa
chanzo kipya cha
maji cha katika mto Ruvu, Bagamoyo.
Ziara za rais Kikwete nchini nBrazil ndizo zilizoiwezesha
Tanzania
Kupata wataalam wa mahiri katika utafiti wa gesi na miradi
iliyozaa
ujenzi wa visima vya gesi katikika mkoa ya Mtwara
uliopeleka umeme wa
uhakika kwa wana Mtwara.
Safari za rais Kikwete nchini Korea zilileta matunda ya
ujenzi wa mto
Magarasi ambapo ujenzi wa mto huo umeufungua mkoa wa kigoma
ambao
ulikuwa nyuma kimaendeleleo. Kigoma imefunguka kwa shughuli
zote za
kiuchumi ikiwemo utalii ambazo zitaboresha maisha ya wana
Kigoma.
Hali kadhalika Ziara za rais Kikwete nchini China ilipelekea
kuzaa
ziara kubwa ya rais Xi Jinping wa china ambayo ilikuwa ziara
yake ya
kwanza barani Afrika. Katika ziara ya Xi wa china
tulishuhudia Tanzania
ikiingia mikataba mikubwa 17 ya miradi mbalimbali ya
kimendeleo
isiyokuwa na hata chembe ya masharti wala hasara kwa
Taifa.
Baadhi ya mikataba hiyo ni pamoja na ujenzi wa bandari ya
bagamoyo
itakayokuwa bandari kubwa kuliko zote ukanda wa jangwa la
Sahara la
Afrika. Ujenzi wa viwanda vya aina mbali mbali ambapo ujenzi
wote huo
utaongeza ajira nchini.
Pia kulisainiwa mkataba wa ushirikiano wa kitaaluma
utakaowawezesha
maelfu ya watanzania kupata ufadhili wa kusoma fani
mbalimbali katika
vyuo vikuu nchini China kwa kufanya hivyo adui ujinga
tutazidi
kumthibiti.
Rais Kikwete amefanya juhudi kubwa za kutangaza vivutio
vya Utalii
Nchini akiwa nje katika zira zake ambazop zimewasidi
kuongeza idadi ya
watalii na safari za, Mashirika ya Ndege ya Qatar Airways,
Fly Dubai na
Turkish Airlines kuongeza idadi ya safari zao nchini
Tanzania. Juhudi
hizo zimesaidia kuwashawishi watalii wengi zaidi kuitembelea
Tanzania.
Idadiya watalii wa nje imeongezeka kutoka 1,095,884 mwaka
2013 hadi
watalii 1,102,026 mwaka 2014/2015. Mapato yatokanayo na
utalii
yaliongezeka kutoka Dola za Marekani milioni 1,853 mwaka
2013 hadi Dola
za Marekani 1,983 mwaka 2014, sawa na ongezeko la asilimia
saba (7).
Yote hayo kutokana na zira za rais Kikwete Nje ya Tanzania.
Mbatia anapaswa
anapoeleza hasara za
Safari na gharama zake pia awe anaeleza faida ya safari hizo
lakini
asipofanya hivyo atakuwa sawa na wanasiasa wengine wachumia
tumbo ambao
huwapotea haraka katika tasnia nzima ya siasa hapa nchini.
Pia namalizi kwa kusema Tunajua kuwa hiki ni kipindi cha
uchaguzi ni vizuri Mbatia
na wenzake wakatangaza ilani yao kuwa nini Watawafanyia
Watanzania
badala ya kueneza uongo ambao huwa haudumu hata siku moja
kwa kuwa
hautachuwa muda mrefu kugundulika na muenezaji wa uongo huo
kuishia
kudharauliwa.
Namuhusia Mbatia badala
ya kutumia muda
mwingi kuzua mambo ya uongo ni bora akatumia muda huo
kueleza na kunadi
sera na ilani ya ukawa na kumsafisha mgombea wo Edward
Lowassa na kashfa
mbalimbali za kifisadi zinazomundama.
0789976314
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment