Monday, 9 June 2014

[wanabidii] TAHADHARI KUHUSU UJUMBE WA BOMU NCHINI

Ndugu zangu ,

Kuna ujumbe unasambaa kuhusu BOMU toka nchi Jirani .

HUU UJUMBE NI WA UWONGO , UKIUONA UPUUZE , UJUMBE WENYEWE UKO KAMA HIVI HAPA CHINI .

HIVI WATANZANIA TUKOJE?!!
- Hebu soma hapa. Sms niliyotumiwa muda huu
*********************************************************
Habari zilizotufikia hivi punde. 
Mtanzania yeyote: kaa makini usiokote kitu chochote ambacho una mashaka nacho, kuna bomu zimerushwa toka nchi jirani Malawi/Rwanda zaidi ya 30 zenye uzito usiopungua tani 100. Hivyo basi uonapo kitu kipo kama chupa la chai chenye rangi ya fedha "usikiguse" piga namba 0756000042. 
SMS hii tuma kwa watu uwezavyo: 
Imetolewa na JWTZ/ LSL5CAMRM: 
Asante. 
JAMBO HILI USILICHUKULIE UTANI KAMA MESEJI ZINGINE ZA UTANI MNAZOTUMIANA!
*********************************************************
Binafsi inanisikitisha sana kuona mtu mzima na akili zako unakubali kutumika kuzambaza upotoshaji, uongo, na ujinga. Simu zimewafanya mkose akili kabisa za kutafakari mambo. 
Tani 100 zinarushwa??!! Toyota Hiace nzito kabisa ina tani 2. 
Lori la Scania lina tani 16
Kwahiyo hiyo sms inamaanisha kuna Hiace HAMSINI zimerushwa kuja Tanzania. Zimerushwa na nini??!
Yote kwa yote, hata kama ingekuwa imerushwa kilo 5, kwa akili yako unadhani JWTZ ingetoa taarifa kwa njia ya Whatsapp badala ya kupitia TV na Radio?! 
AMKENI WATANZANIA, JARIBU KUTAFAKARI KWA MAKINI KILA SMS YA KUTISHANA UNAYOTUMIWA. USIKUBALI KUFANYWA NA KUGEUZWA MJINGA WA KUSAMBAZA UJINGA. 
JITAMBUE!!!!


--

Yona Fares Maro

Institut d'études de sécurité - SA


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment