Sunday 29 June 2014

Re: [wanabidii] MWANANGU MPENDWA, NAOMBA UNISIKILIZE KWA UZURII KABLA HUJAOA....

Wanawake leo wanataka haki sawa.lakini ukigawa mahitaji kaatika pande mbili sawa hawataki kusikia

On Jun 29, 2014 12:48 AM, "Erick Maro" <rikmaro@gmail.com> wrote:

Safi sana

On Jun 29, 2014 12:33 AM, "jones konga" <lufj.24@gmail.com> wrote:
ujumbe mzuri sana kwa vjana wetu

On 6/28/14, Fakhi Karume <fkarume@gmail.com> wrote:
>
>
> MWANANGU MPENDWA, NAOMBA UNISIKILIZE KWA UZURII KABLA HUJAOA….
>
> 1. Mwanangu, mwanamke anaweza kuwa mkeo, mwingine anaweza kuwa mama wa
> watoto wako, lakini ukipata mwanamke ambae atakuwa kama mama kwako, mama
> kwa wanao na mama kwa familia, tafadhari mwanangu usimuache huyo!
>
> 2. Mwanangu, usimfanye mwanamke wako kuwa ndio wa kupika na kufanya kazi
> zote za jikoni peke yake, tabia hiyo sio nzuri Kwani hata nyakati zetu,
> mashamba yetu yalijulikana kwa majina yetu wanaume lakini tulifanya kazi
> pamoja!
>
> 3. Mwanangu, nikikwambia wewe ni kichwa cha familia, simaanishi kutuna kwa
> pochi lako, usiangalie kabisa pochi yako, angalia kama utaona tabasamu
> usoni kwa mke wako. Pesa sio kila kitu katika ndoa na haileti ukuu wa
> familia!
>
> 4. Mwanangu, ukitaka kuwa na maisha marefu, mwache mkeo awe na jukumu la
> kuratibu mshahara wako au kipato chako, haitakuwa rahisi kwa yeye kutumia
> hela hovyo wakati akijua kuwa nyumbani kuna mahitaji ya msingi, lakini hela
>
> zikiwa mikono mwako ataendelea kuomba hata kama utakuwa umeishiwa!
>
> 5. Mwanangu, Usithubutu kumpiga mkeo, maumivu ya kipigo hukaa ndani ya moyo
>
> wake kwa muda mrefu sana na huacha kidonda ambacho hukawia sana kupona. Ni
> hatari sana kuishi na mwanamke mwenye majeraha moyoni!
>
> 6. Mwanangu, sasa unaamua kuoa,kama bado utaendelea kuishi maisha kama ya
> ubachela na mke wako, sio muda mrefu utakuwa bacheol tena. ukioa Badilika
> anza kuishi maisha ya mke na mume!
>
> 7. Mwanangu, zamani,tulikuwa na wake wengi na watoto wengi kwa sababu
> tulikuwa na mashamba makubwa na mavuno yalikuwa makubwa, lakini kwa sasa
> maisha yamebadilika, kwa hiyo mkumbatie mwanamke wako peke yake kwani
> hakuna ardhi tena na mahitaji ya watoto ni makubwa sana. Angalia ukubwa wa
> familia yako!
>
> 8. Mwanangu, chini ya mwembe ambao nilikuwa nikikutana na mama yako inaweza
>
> kuwa ni hoteli kubwa kwa nyakati zenu,lakini kumbuka, kitu pekee
> tulichoweza kufanya chini ya mwembe ilikuwa ni kukumbatiana
> pekee.nakushauri ukikutana na marafiki wa kike kikubwa unachoweza kufanya
> nao ni kupeana mikono na ikizidi ni kukumbatiana hadharani sio vinginevyo!
>
> 9. Mwanangu, usibadilike mara utakapoanza kupata mafanikio Zaidi, kuliko
> kuwahudumia hao viruka njia wa mtaani ambao hawajui mmetoka wapi na mkeo,
> nakushauri utumie na kufurahia mafanikio yako na mkeo ambae aliweza
> kusimama imara wakati wote wa mapito yenu magumu.
>
> 10. Mwanangu, kumbuka unapoanza kusema au kuona mke wako kabadilika, ujue
> kuwa kuna kitu ambacho ulikuwa ukikifanya umeacha kukifanya. Jitathmini na
> anza kufanya au kutimiza wajibu wako.
>
> 11. Mwanangu, usijaribu kumfananisha au kumlinganisha mke wako na mwanamke
> mwingine wa nje, kwani hata yeye anakuvumilia sana na hajakufafanisha na
> mwanaume mwingine yoyote huko nje na ndio maana aliamua kuwa na wewe.
>
> 12. Mwanangu, sasa hivi kuna hiki kitu kinaitwa haki za wanawake, sawa,kama
>
> mwanamke anasema ana haki sawa na wewe katika nyumba, basi gawanya mahitaji
>
> yote ya ndani kwenu katika sehemu mbili zilizo sawa,halafu timiza nusu yako
>
> na mwambie atimize nusu iliyobaki.
>
> 13. Mwanangu, nilimuoa mama yako akiwa bado kigoli (bikra) na nilikuwa
> naenda sana kwao kabla sijamuoa, lakini kutomkuta mkeo bikra kusikufanye
> umlaumu kuwa alikuwa muhuni, kumbuka wanawake wa enzi zetu na wasasa ni
> tofauti, ulimchagua mwenyewe na ukigoli wake hukuujua kabisa. Usiingize
> mambo ya kabla ya ndoa kwenye ndoa yenu.
>
> 14. Mwanangu, sikuwapeleka dada zako shule kwa kuwa nilikuwa mjinga kama
> waze wengi wa hapa kijiji wasemavyo, tafadhari usifanye ujinga huu, kwani
> kiwango cha mafanikio ya wanawake sasa kimefanya wanaume waonekana ni watu
> wa kawaida sana na sio muhimu kama zamani, Ukijaliwa watoto wape elimu.
>
> 15. Mwanangu, zamani enzi za ujana wetu, wanawake walikuwa na urembo wa
> asili, ingawa siwezi kukudanganya, wengine waliongeza urembo kwa kujichora
> hina na hata kutoboa pua na masikio lakini usisahau hawakuonyesha maumbile
> yao nyeti hadharani kama sasa. Hakikisha mkeo analijua hili!
>
> 16. Mwanangu, mama yako na mimi hatuna hisa katika kila kitu kinachoendelea
>
> kwenye maisha yenu, jaribuni kutatua changamoto zenu wenyewe bila kila mara
>
> kuja kwetu kuomba usuluhishi. Ndoa ni pamoja na ukomavu wa kutatua
> changamoto zenu bila kuziuza kama gazeti kwa kila mtu.
>
> 17. Mwanangu,nilimnunulia mama yako kifaa cha kupikia vitumbua ili aanzishe
>
> mradi wa kuuza vitumbua, pia nilimsaidia kununua cherehani yake ya kwanza,
> tafadhari msaidie mke wako kutimiza ndoto zake kulingana na uwezo wako kama
>
> ambavyo unahangaika kutimiza ndoto zako.
>
> 18. Mwanangu, usiache kutusaidia mimi na mama yako, utu uzima una
> changamoto nyingi sana na Mungu akikujalia utaziona muda ukifika. Pamoja na
>
> kutimiza majukumu yako kama baba wa familia kumbuka pia bado tunaishi na
> wewe ni mtoto wetu.
>
> 19. Mwanangu, kila upatapo muda wa kusali, Sali na familia yako, kuna kesho
>
> ambayo huijui, ongea na MUNGU wako ambae anajua kila kitu kila siku!
>
> 20.NAKUTAKIA MAISHA MEMA YA NDOA MWANANGU….NAKUPENDA!
>
> --
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
>

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment