Sunday 29 June 2014

Re: [wanabidii] KIGOGO WA CHADEMA , MSAFIRI MTEMELWA AACHIA NGAZI RASMI

Aliyeleta habari hii ni mwamajukwaa anayejulikana kama Mabadiliko Chadema au naota tu!


2014-06-30 0:42 GMT+03:00 MABADILIKO CHADEMA <mabadilikochadema@gmail.com>:

Msafiri Mtemelwa aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Taifa wa Vijana wa NCCR-Mageuzi kabla hajashirikiana na Augustine Mrema kwenye 'mission' iliyotumika kukirudisha nyuma kama si kukiua chama hicho, hatimaye amejiona ni 'misfit' ndani ya CHADEMA na kuomba kuondoka 'rasmi' kwenye chama hicho.

Habari ambazo zimenifikia kutoka kwa watu wake wa karibu zinasema kuwa Mtemelwa aliomba kukutana na Katibu Mkuu wa CHADEMA, ili walau apate kitu chochote kutoka kwenye chama hicho kwa maana ya 'mkono wa kwa heri', kwa kuwa amekuwa mtumishi wa chama hicho kwa nafasi ya ofisa kwa muda mrefu (tangu alipojiunga na CHADEMA), hivyo afikiriwe katika hali yoyote.

Habari hizo zimezidi kutiririka zikimnukuu Mtemelwa akiwaambia watu wake wa karibu kuwa hakutegemea ushirikiano alioupata katika maombi yake ya kufikiriwa kupewa mkono wa kwa heri kwa kuzingatia nafasi yake aliyokuwa nayo ya Ofisa, ambayo inasemekana kwamba alikuwa na fikra hasi kuwa asingesikilizwa kutokana na matendo yake kwa nyakati tofauti tofauti dhidi ya chama hicho.

Kinyume na matarajio yake, Katibu Mkuu wa CHADEMA alimsikiliza Mtemelwa kuhusu maombi yake, ambapo muombaji alikubaliana na kiwango kilichopangwa kwa kuzingatia maombi yake, huku pia akipewa notice ya mwezi mmoja, kwa maana ya kwamba angelipwa 'mkono wa kwa heri' pamoja na stahili ya posho yake ya mwezi mmoja huu wa sita.

Sasa habari kutoka kwa marafiki wake wa karibu (ambao wanamfahamu kwa tabia ya uropokaji na kutotunza neon), wamemnukuu akianza kulalamika namna anavyoshawishiwa afanye mkutano na waandishi wa habari ili eti atangaze kuwa amehama ndani ya CHADEMA lakini anakidai chama hicho.

Maelekezo hayo anayapata kutoka kwa MM na MM 1 (hawa wanajulikana) na kundi lao ambao nao wanapata maelekezo kutoka kwa walioko nyuma yao wanaowapatia fedha za mkakati wa kupambana na CHADEMA.

Kutokana na tamaa ya fedha (ni moja ya sifa zake kama itakavyooneshwa hapo chini), Mtemelwa kasikika akiwaambia rafiki zake kuwa amekubali kufanya press conference kati ya leo Jumapili, Jumatatu ya kesho au keshokutwa Jumanne. Tayari MM 1 yuko anandaa taarifa kwa vyombo vya habari ambayo Msafiri Mtemelwa atatakiwa kuisoma mbele ya waandishi watakapoitwa!

Makubaliano ya kikao hicho ni kwamba ndani ya hiyo taarifa kwa vyombo vya habari, MM 1 atatakiwa kutengeneza kila aina ya uongo anaoweza kadri ya kipawa chake cha kupika mambo kinapoishia.

Wanasema kuwa uongo au matusi dhidi ya CHADEMA na viongozi wake yatakayosemwa na Mtemelwa yanaweza kuwarubuni watu wachache kwa sababu eti alikuwa Ofisa wa Chama hicho.

Tuhuma za kuuza ubunge, Zitto kukataa kumsaidia

Marafiki zake hao wanasimulia namna ambavyo Mtemelwa alishiriki Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995 alipogombea jimbo la nyumbani kwao, Rufiji.

Wanakumbushia namna alivyokacha kampeni na kurudi Dar es Salaam siku moja kabla ya kufanyika uchaguzi akisingizia kuwa amepatwa na dharura. Kitu cha kushangaza ni kwamba alirudi Dar es Salaam kwa kutumia gari la mgombea wa CCM, Mbonde.

Wasimuliaji wanasema Mtemelwa angeshinda uchaguzi ule. NCCR-Mageuzi ilikuwa inatisha. Naye alikuwa anakubalika jimboni mle, akisaidiwa sana na chama chake. Lakini ndiyo hivyo…tena akarudishwa Dar es Salaam na gari la mgombea wa CCM.

Baada ya uchaguzi huo ndiyo wakaanzisha vurugu na timbwiri timbwiri lililoififisha NCCR-Mageuzi. Wakatumiwa na CCM na kile kinachoitwa 'mfumo' wakapambana kweli kweli dhidi ya akina Marando. Wakarudisha nyuma matumaini ya Watanzania wanyonge.

Walipofanikiwa mission hiyo, kundi hilo wakakimbilia TLP (ambako hadi leo Mrema yuko akigeuza chama kuwa mali yake, akibebwa na CCM), na kupoka madaraka huko.

Wakiwa NCCR-Mageuzi, dhambi ya usaliti na umamluki haikuwaacha. Kwa sababu ya tamaa ya fedha, wakakosana na Mrema, akakimbilia Chama cha Wananchi (CUF).

Kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2000, Mtemelwa aligombea udiwani Kata ya Mbagala kwa tiketi ya CUF, ambako alishindwa vibaya. Wapinzani wake walitumia kete ya tuhuma za 'kurudishwa' na gari la mgombea wa CCM mwaka 1995. Dhambi ikamfuata CUF pia, ambako alilazimika kuhama na kutua CHADEMA.

Alipofika CHADEMA, akionekana kuwa mtu aliyejutia na kujifunza kutokana na makosa yake, akateuliwa kuwa Ofisa Makao Makuu, ambapo pia akapewa majukumu ya kukaimu nafasi ya Mkurugenzi wa Kampeni na Uchaguzi.
Mwaka 2010 kwa kujua madhira ya kile kilichompata Mbagala kutokana na kile alichofanya Rufiji, hakwenda kugombea Rufiji kwao, badala yake akakimbilia Urambo, Tabora ambako pia anayo nasaba.

Ni kwenye kampeni hizo za 2010, swahiba wake na mtu wanayeshawishiana kwa mambo mengi, Zitto Kabwe hakufika Urambo kumpigia kampeni nduguye. Akamwambia hawezi kupiga kampeni (za CHADEMA) dhidi ya mgombea wa CCM ambaye alikuwa ni Samuel Sitta akisema ni Baba yake!

Pamoja na swahiba wake kumtosa, yeye mwenyewe hakufanya kampeni za maana pia. Watu wakakumbushia kile kilichofanyika Rufiji mwaka 1995 cha kurudishwa na gari la mgombea wa CCM katikati ya kampeni. Kwamba huo u-baba wa kutengeneza, ilikuwa ni sehemu ya 'business'.

Hatimaye amebwaga manyanga

Sasa marafiki zake wanasema kuwa maboresho yanayoendelea ndani ya CHADEMA ya kujipanga kwa ajili ya majukumu makubwa mbele ya safari, yamekuwa yakimnyima raha kwa sababu atalazimika kurudi kutumikia nafasi yake stahili yaani ya uofisa ambapo angepaswa kuwa chini ya moja ya kurugenzi za chama hicho.

Hiyo inatokana na kwamba chama hicho kimeondoa Kurugenzi ya Kampeni na Uchaguzi katika mfumo wake, kwa sababu kwa namna chama hicho kinavyoendesha shughuli zake na operesheni, wakati wa kampeni za uchaguzi, chama kizima huwa kinahusika, sasa majukumu mengine ya kurugenzi hiyo yakarudishwa chini ya ile Kurugenzi ya Benson Kigaila na machache yamekuwa chini ya Kurugenzi ya Uenezi.

Baada ya kujiona ni 'misfit' amefikia hatua ya kuomba aondoke, kuliko kuendelea na nafasi yake ya Ofisa wa Makao Makuu. Kwa mujibu wa vikao vya mamluki na wasaliti vinavyoendelea kufanyika, ameagizwa afanye hiyo press conference ya kutukana CHADEMA, kutukana viongozi na kuzua uongo mwingine, wakati wowote kuanzia sasa, kama alivyofanya akiwa NCCR, TLP, CUF na mara kadhaa alipokuwa hapo hapo CHADEMA.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment