Sunday 29 June 2014

[wanabidii] UAMUZI WA JULIUS MTATIRO NA GIZA NYUMA YA PAZIA

Hakuna kijana au mzee wa Taifa hili asiyejua mchango wa Julius Mtatiro kwenye siasa za Upinzani hapa Tanzania. Ni mfano wa kijana anayeweza kuthubutu kujenga hoja na kuibua tafakuri ambazo ni zenye kujnga mustakabali chanya katika siasa ndani ya CUF na nje pia.

Kuna wakati Chama cha CUF kiliyumba na baadhi ya viongozi wake pia kukata tamaa lakini akiwa Naibu Katibu Mkuu Taifa alisimama akapigana akakifikisha Chama mahala kilipo akiwa ndio Kiongozi kijana mwenye mvuto kwa tabaka hili muhimu.

Leo safu mpya ya uongozi Mtatiro hayupo. Kuna wakati pengine watu waliamini angeweza kutumikia chama katika nafasi zaidi ya ile ya Naibu Katibu Mkuu lakini haikuwa hivyo. Magdalena Sakaya amepata nafasi hiyo nandiye Naibu Katibu Mkuu mpya. Mtatiro hajafikia uwezo wa kushindana na Maalimu Seif na Lipumba? Na kama ndio wanamuandaa kuwa mrithi hapo baadae hawaoni kama alipaswa awe ndani ya Uongozi ili aendelee kupata uzoefu? Ama kaogopa yasimtokee ya Zitto Kabwe na je unadhani nini hatma ya kukosekana kwake katika safu hii inayoendelea kuongozwa na wakongwe Prof Lipumba na Maalim Seif?

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment