Friday 27 June 2014

[wanabidii] Re: MWANACHUO WA RUCO ACHOMWA MOTO AKIDHANIWA NI MWIZI...!

Mwanafunzi ambaye amefahamika kwa jina moja la LEMA Alikua akisoma mwaka wa 4 kozi ya sheria katika chuo kikuu kishiriki cha Mt.Augustino Tawi la Iringa (Ruaha University College-RUCO).

Taarifa  za awali zilizotufikia zimeeleza kuwamnamo tarehe 24.06.2014 mwanafunzi huyo alikua ametoka kuangalia michuano ya kombe la dunia na akiwa amelewa akawa anatafuta chakula cha jioni na ilikua majira ya saa 5 Usiku, Mwanafunzi huyo aliingia kwenye mgahawa ambao biashara ilikua imefungwa kwa muda huo lakini ndani kulikuwapo na Binti ambaye alianza kupiga kelele kwa kudhani alikua mwizi. Na kwakua eneo hilo mkulikuwa na mlinzi(Mmasai) ndiye aliyeanza kumshambulia mwanafunzi huyo.

Baada ya tukio hilo wakatokea watu  (2) waliojitambulisha kuwani askari wakaamuru mwanafunzi huyo asipigwe kwa madai ya kumfikisha kituoni.

Lakini baada ya mwendo mfupi kuelekea kituoni wananchi wenye hasira kali walimchukua kijana huyo kinguvu na kwenda kumchoma moto.

Mpaka sasa Kijana huyo amelazwa katika wodi ya watu mahututi (ICU) katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa.

On Friday, June 27, 2014 12:47:26 AM UTC-7, Jane Mwakalukwa wrote:
LEMA mwanachuo aliyechomwa moto
Maskini: Mwanafunzi wa Chuo Anusurika Kifo Baada ya Kuchomwa Moto Akidhaniwa ni Mwizi

Kijana huyu anaitwa LEMA, anasoma chuo cha ruaha a.k.a RUCO huko iringa. Alikuwa sheria mwaka wa nne. Ameitiwa mwizi kumbe sio akachomwa moto. Ameungua ila hajafa, hivyo ndivyo alivyo.. Alitoka kutazama mpra alivokua anarud akawa anaenda bar apate chochote muda ukawa umeisha mlinz akampgia kelele za mwizi wakampiga lakini aliwaambia watu wasimpeleke police akawaelekeza ye siyo mwizi na kitambulisho aliwaonyesha lakini hawakuelewa wakamuwasha moto. Kijana huyu ameungua asilimia 85% ya mwili wake.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment