Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imeshauriwa kuwa na uraia kwa watu wake pamoja na kuvipa hadhi vikosi vyake maalumu ili viweze kumiliki silaha za kivita chini ya mfumo wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Ushauri huo ulitolewa jana na baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakati wakichangia makadirio na matumizi ya Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Vikosi Maalumu iliyowasilishwa na Waziri wake, Haji Omar Kheir, Chukwani mjini Unguja jana.
Akichangia bajeti hiyo, Mwakilishi wa Koani, Mussa Ali Hassan alisema wakati umefika kwa vikosi vya SMZ kupewa hadhi ya kumiliki silaha za kivita badala ya kumiliki silaha za kawaida kama ilivyo sasa kwa mujibu wa sheria.
Hassan alisema kuna vikosi vya SMZ ambavyo havina tofauti na askari wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), ambavyo vilishiriki kupambana na majeshi ya Idd Amini yalipovamia Tanzania mwaka 1978.
Alisema ni wakati mwafaka na unaofaa kwa SMZ kununua silaha kama mizinga, vifaru, helikopta za kivita na boti za kijeshi pamoja na silaha nzito kama RPG.
Wajumbe wengine, Amina Idd Mabrouk (Viti Maalumu), Jaku Hashim Ayoub(Muyuni), Raha Suleiman (Viti Maalumu), waliitaka Serikali kuangalia masilahi ya askari wa vikosi vya SMZ ikiwamo kuwapatia vitendea kazi pamoja na kuwajengea makazi bora.
Wawakilishi hao kwa nyakati tofauti walidai kuwa nyumba nyingi za makazi ya askari ni chakavu na hazistahili kukaliwa na askari ambao wanalinda nchi huku wananchi na viongozi wakiishi kwenye makazi bora.
Pia waliitaka SMZ kutambua umuhimu wa kuwalipa posho na marupurupu stahiki kwa muda wa kazi wa ziada askari wa vikosi vya SMZ pamoja na kuwaingiza katika Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF).
Akizungumzia uraia, Mwakilishi wa Chambani, Mohamed Mbwana Hamad alisema: "Huwezi kuwa na nchi bila ya kuwa na raia." Alitaka Wazanzibari kupewa uraia wao katika mfumo wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kusema ni jambo la kushangaza Wazanzibari kuitwa wakazi na si raia.
Alisema Wazanzibari wote wanatakiwa kupewa hadhi ya uraia na wageni ndiyo wanaostahili kuwa na vitambulisho vya ukaazi kama ilivyokuwa miaka ya nyuma, hatua ambayo itaipa hadhi nchi na kutambulika kitaifa na kimataifa.
mwananchi
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment