Msimamizi wa ufundi wa Magari aina ya Mercedes Benz kutoka kampuni ya CFAO Motors Bw. Winner Mushi (wa tatu kushoto) akionyesha matumizi ya kifaa maalum cha ukaguzi wa Malori ya Mercedes Benz (Star Diagnosis Machine) kwa baadhi ya mafundi na wasimamizi wa ufundi wa magari ya kampuni ya Bakhresa Group.

Bakhresa Group ni mmoja wapo wa wateja wa CFAO Motors ambao wanamiliki malori ya Mercedes Benz. Bw. Heico Herzog Mtaalamu wa ufundi (Flying Doctor) kutoka Mercedes Benz Ujerumani,(wa tatu kulia) akisimamia shughuli hiyo iliyoendeshwa na Bw. Mushi.

Wengine ni Key Account Manager wa Mercedes Benz, Bw. George Washington (kulia), Meneja wa Usafirishaji kutoka kampuni ya Bakhresa Group, Bw. Abdallah Seif (kushoto), Jarangi Nyabagara ambaye ni fundi wa Mercedes Benz (wa pili kushoto), na aliyechuchumaa ni Mohammed Shariff Meneja wa Karakana ya Bakhresa Group.

Na Mwandishi Wetu,

KAMPUNI ya CFAO Motor Tanzania hivi karibuni imezindua huduma mpya ya "Service Camp" ambapo chini ya huduma hii wa wamiliki wa malori yanayotengenezwa na Mercedez Benz watapata huduma ya ukaguzi bure na mafunzo kwa madereva wao.

Akizungumza na mwandishi wetu, jijini Dar es Salaam Key Account Manager wa Mercedez Benz, Bw George Washington amesema kwamba wameamua kuanzisha huduma hiyo ili kuweza kuwahudumia wamilimi wa magari hayo kwa karibu zaidi.

"Mpango huu utapeleka huduma karibu na wateja na kwa kuwa hapo mwanzo wamiliki wa malori walikuwa hawapati huduma za matengenezo vizuri barani Afrika," amesema

Amesema kuwa kuna upungufu katika kuwahudumia wamiliki wa malori ya Mercedez Benz Afrika na hivyo wameona ni busara kuja na 'Service Camp' ili kuwapeleka wateja huduma za matengenezo na mafunzo kwa madereva wao huko walipo.

Aliongeza kwamba huduma hiyo ya 'Service Camp' itakuwa ikitolewa kwa njia mbili tofauti ambazo ni kwenda kwa mteja na kukagua malori bila gharama yoyote.

Amesema kwamba vile vile chini ya huduma hiyo watakuwa wakitoa mafunzo kwa madereva wa malori ili waweze kujajua vizuri magari hayo pindi wanapopata tatizo la kiufundi.

Bw.Washighton aliongeza kwamba vile vile watakuwa wanawafundisha madereva jinsi vipuri vya Mercedez Benz vinavyopaswa kuwa ili kuweza kutambua vipuri bandia kwenye soko la nchini au karakana mbalimbali.

"Tunawaonesha vipuri halisi na vipuri bandia kwa sababu kuna madhara katika kutumia vipuri bandia ambapo madhara yanaweza yasionekane katika muda wa siku chache bali huonekana baada ya muda mrefu,"

"Ukianza kuangalia gharama ya kutengeneza gari baada ya madhara kutokea unakuta gharama yake ni kubwa kuliko ambapo ungetumia vipuri halisi," alieleza Bw Washington.

Alisisitiza kwamba kwamba hatua ya pili ni kuweka kambi barabarani ambapo malori mengi ya Mercedes Benz yanapita, hivyo kila ambaye anamiliki lori aina ya Mercedes Benz na anataka kufanyiwa ukaguzi, hupata huduma hiyo bila gharama, na hatimaye taarifa kamili zake za ukaguzi kurudishwa kwa mmiliki wake.

Washington amesema kwamba kampuni ya CFAO inataka kuwa karibu zaidi na wateja wake, kwani inataka wateja waone kwamba kuna watu wanaowajali ili kudumisha na kuimarisha uhusiano kati yao na wateja wao.

Muuzaji wa vipuli vya magari ya Mercedes Benz nchini kutoka kampuni ya CFAO Motors, Emmanuel Sembua akimfafanulia jambo Meneja wa Usafirishaji kutoka kampuni ya Bakhresa Group, Bw. Abdallah Seif jinsi ya kutambua vifaa feki vya magari vya Mercedes Benz ili kujieupusha na matapeli ya vifaa hivyo.

"Tunataka wateja wetu waone kwamba iwapo magari yao yanapata matatizo, kuna watu ambao watawafuata na kuwahudumia kwa wakati unaofaa. Kama unavyojua haya ni malori kwa ajili ya transport business, hivyo hayapaswi kuwa mabovu kwa wakati mrefu kwa kuwa hiyo itawasababishia hasara wateja wetu. Wameyanunua ili wayatumie kwenye biashara na kazi zao, sasa, yakiwa out of service, hiyo ni hasara, na sisi hatutaki wateja wetu wapate hasara," aliongeza Washington.

Alipoulizwa kuhusu upatikanaji wa huduma hiyo ya "Service Camp", Washington amesema kwamba hii ni mara ya kwanza huduma hiyo kupatikana hapa nchini, ila kwa nchi jirani ya Kenya, huduma hiyo imeshapatikana mara tatu. Aliongeza kwamba huduma ya "Service Camp" itapatikana tena mwezi Novemba mwaka huu.

"Tutaitoa huduma hii kwa muda mfupi hapa Dar es Salaam kisha tutahamia mikoani na huu ni mpango endelevu, sio kitu cha mara moja," alisisitiza.

Akizungumzia kuhusu huduma iliyotolewa kabla ya kuanzishwa kwa "Service Camp", Washington amesema kwamba awali walikuwa na huduma inayoitwa "Technical Exchange", ambayo ilikuwa na lengo ya kubadilishana uzoefu wa kiufundi kati ya wasimamizi wa karakana za wamiliki wa magari hayo na mafundi wa CFAO.

Meneja wa Usafirishaji kutoka kampuni ya Bakhresa Group, Bw. Abdallah Seif na Meneja wa Karakana ya Bakhresa Group, Mohammed Shariff wakipewa maelezo na Muuzaji wa vipuli vya magari ya Mercedes Benz nchini kutoka kampuni ya CFAO Motors, Emmanuel Sembua (kulia) ya Battery zinazouzwa na kampuni ya CFAO Motors yenye garantii na uwezo mkubwa kwa malori.

"Tumegundua kwamba baada ya kuifanya hii technical exchange kumekuwa na mafanikio makubwa sana na tumeenda mbele na kuiboresha zaidi na tutafika wakati ambapo kutakuwa na washindi, kwani tumeona tuwashindanishe hawa mafundi wakuu kwa nia ya kuongeza ufanisi wao ili waweze kuyasimamia magari ya waajiri wao vizuri zaidi.

"Kutakuwa na washindi ambao tutawapeleka Ujerumani, kule kwenye kiwanda, ili waweze kuona jinsi ambavyo magari yanaundwa na kusimamiwa,

"kuanzia ubunifu hadi majaribio na mwisho kwenda kiwandani kwa ajili ya uundwaji. Huu ndio mpango ambao tunao hivi sasa na mpaka mwaka kesho tutakuwa tumempata mshindi ambaye tutampeleka Ujerumani ili atuwakilishe kule na kuona jinsi mambo yanavyoendesha. Kwa mantiki hii mpango huu nao pia ni mpango endelevu," amesema Washington.

Washington alihitimisha na kusema kwamba mpango huu wa "Service Camp" unahusu magari ambayo ni malori pekee yaani Atos, Actros na Atego, na kwamba magari madogo hayatahusishwa na mpango huu.

Picha ya pamoja baada ya zoezi hilo.

Amesema kwamba kwa sasa huduma hii inapatikana kwenye karakana zilizopo kwenye ofisi za CFAO zilizopo Barabara ya Nyerere na kwa upande wa Road Inspection, wamiliki wa malori ya Mercedes Benz watajulishwa mapema.

Aliongeza kwamba kuhusu mwezi Novemba, kituo kikuu cha kwanza nje ya Dar es Salaam kitakuwa Kibaha kwa kuwa barabara hiyo inatumiwa na magari mengi yanayokwenda mikoani.

Hatimaye, vituo vingine ambavyo vimepangwa vitatangazwa mapema iwezekanavyo ili wateja wa CFAO wapate muda wa kutosha kujiandaa.

KAWAIDA

Zainul A. Mzige,Operation Manager,
MO BLOG,
+255714940992.
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to

0 comments:
Post a Comment