Friday 17 May 2013

[wanabidii] UDHAIFU WA SERIKALI NA MMOMONYOKO WA MAADILI MITAANI.

Mwaka 2009 kama kukumbukumbu zangu ziko sahihi serikali ilipiga marufuku mabanda ya kuonyesha video mitaani kwa kile ilichokieleza kuwa kumekuwa na malalamiko toka kwa jamii kuwa mabanda hayo yalikuwa hatalishi hasa kwa watoto wadogo badala ya kwenda shule huishia kwenye mabanda hayo kuangalia picha.
 
Tatizo langu si tamko la serikali bali ni kuona jinsi watendaji wa serikali wenye dhamana walivyoshindwa kutekeleza agizo hilo matokeo yake ni kuenea zaidi kwa mabanda hayo na matokeo yake sasa hivi ikifika mida ya usiku watu wakilala mabanda hayo sasa huonyesha picha za ngono kwa watoto wadogo, na hatimae sasa kesi za watoto wadogo kuingiliana kimwili kinyume na maumbile zimekuwa nyingi kupita kiasi,
 
Tumejaribu kuongea na wajumbe wa nyumba kumi wa CCM hakuna kinachofanyika na kibaya zaidi mabanda mengine yako karibu kabisa na vituo vya police na wala ni kama hawalijui lile tamko la serikali na pia wenyeviti wa serikali za mitaa ni kama hawajui wajibu wao kuhusu maagizo ya serikali na pale ambapo maagizo husika yanaigusa jamii ya chini.
 
Nawaomba wale wenye dhamana na hili wajaribu kutusaidia kili kukiokoa kizazi kijacho.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment