Thursday 2 May 2013

[wanabidii] Taarifa kwa umma kuhusu tangazo la kazi Serikalini la Machi 26, 2013

Waombaji wa nafasi za kazi Serikalini kwa tangazo lililokuwa limetolewa tarehe 26 Machi, 2013 kupitia Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ambalo mwisho wa kutuma maombi ilikuwa terehe 9 Aprili, 2013 wametakiwa kuangalia majina yao katika tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kuanzia tarehe 13 Mei mwaka huu ili kujua endapo wamechaguliwa kwa ajili ya kufanya usaili wa nafasi walizoomba.

Naibu Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Bw. Lucas Mrumapili amesema ofisi yake imepokea jumla ya barua za maombi ya kazi 20,763 ambazo mchanganuo wake  kwa tangazo la Kiingereza imepokea barua za maombi 6,332 na kwa tangazo la Kiswahili imepokea barua za maombi 14,431 ambapo Ofisi yake iko katika hatua za mwisho za kukamilisha  uchambuzi wa maombi hayo ili kuweza kuendelea na zoezi la usaili.

Mrumapili amebainisha kuwa kwa tangazo la Kiingereza lililokuwa na  nafasi wazi 185 ni kwa ajili ya Waajiri kutoka katika Taasisi za Umma zifuatazo; Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (NAO), Chuo Kikuu Mzumbe (MU), Chuo cha Serikali za Mitaa (LGTI), Wakala wa Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC), Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI), Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI), Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Arusha (ATC), Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST), Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO), Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG),

Amewataja Waajiri kuwa ni pamoja na Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC), Wakala wa Huduma za Ufundi na Umeme (TEMESA), Kituo cha zana za Kilimo na Ufundi Vijijini (CAMARTEC), Chuo cha Maji (WDMI), Chuo cha Mipango Dodoma(IRDP), Chuo cha Takwimu cha Afrika Mashariki (EASTC), Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi (TAFIRI), Taasisi ya Magonjwa ya Mifupa Muhimbili (MOI), Chuo cha Bandari Dar es Salaam (DMI), Wakala wa Mafunzo ya Uongozi wa Elimu (ADEM), Taasisi ya Ustawi wa Jamii (ISW), Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA), Wakala wa Serikali Mtandao (eGA), Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) pamoja na Chuo cha Diplomasia na Uhusiano wa Kimataifa (CFR).

Amesema kwa upande wa Tangazo la Kiswahili lilikuwa na nafasi wazi 949 ambapo Waajiri  wake ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Katibu Mkuu wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa Kimataifa, Afisa Mtendaji Mkuu Wakala wa Vipimo, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Katibu Mkuu Wizara ya Kazi na Ajira, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara. Katibu Mkuu Wizara ya Sayansi na Technolojia, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi, Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Katibu Ofisi ya Rais Maadili.

Wengine ni Katibu Tawala wa Mkoa Kagera, Iringa, Ruvuma, Mbeya, Mwanza, Shinyanga, Manyara, Dar es Salaam, Morogoro, Geita, Pwani, Mara, Kilimanjaro, Lindi, Singida, Tabora, Tanga, Katavi na Arusha, Mkurugenzi Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Mkurugenzi Halmashauri Manispaa Iringa, Songea, Shinyanga, Morogoro, Singida, Kigoma/Ujiji na Temeke.

Nafasi nyingine ni kwa ajili ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya Mufindi, Kyela, Rungwe, Mbeya, Chunya, Biharamulo, Bukoba, Muleba, Namtumbo, Songea, Morogoro, Makete, Mkuranga, Mbinga, Tunduru, Ukerewe, Sengerema, Ilemela, Busega, Maswa, Meatu, Shinyanga, Kishapu, Kilosa, Msalala, Rufiji, Rorya, Ruangwa, Lushoto, Mkinga, Mpanda, Monduli, Ngorongoro,Kigoma, Nachingwea, Rombo, Same, Singida, Urambo, Tabora, Babati, Mbulu, Simanjiro, Kiteto, Handeni, Pangani, Kibondo, Chamwino, Mtwara, Nanyumbu, Mpwapwa, Kongwa naTandahimba. Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Njombe, Kibaha, Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) na TEMESA.

Aidha, amewataka waombaji na wadau wengine  kurejea Matangazo ya nafasi za kazi yaliyokuwa yametolewa tarehe 26 Machi, 2013 ili kujikumbusha kuhusu nafasi husika zilizokuwa zimetangazwa.Alimalizia kwa kusema kuwa waombaji ambao hawataona majina yao pindi majina yatakapotangazwa wajue hawakufanikiwa kutokana na kutokukidhi vigezo vya tangazo kwa nafasi husika walizokuwa wameomba, hivyo wasisite kuomba kwa mara nyingine pindi nafasi hizo zitakapotangazwa tena.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
Ofisi ya Rais-Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.  

30 Aprili, 2013. 

Kwa maelezo zaidi; wasiliana na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kwa Barua pepe; gcu@ajira.go.tz  au Simu; 255-687624975


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment