Tuesday 21 May 2013

[wanabidii] Re: Ungependa nani apeperushe bendera ya CCM 2015?

On Saturday, 18 May 2013 23:01:45 UTC-12, Abdalah Hamis wrote:
> Miongoni mwa watu wanaotazamiwa kuchukua fomu kuwania Urais ni Mhe.
>
> Bernard Membe, Mhe. Mwigulu Nchemba, Mhe. William Ngeleja, Mhe.
>
> Emmanuel Nchimbi, Mhe. Dr. Harrison Mwakyembe, Mhe. John Magufuli,
>
> Mhe. Steven Wassira, Mhe. Samwel Sitta, Mhe. Edward Lowassa. Watatu wa
>
> mwanzo ni wanachama wa kundi la M2015 (Mustakabali 2015) tulolianzisha
>
> miaka mi2 iliyopita, halifungamani na yeyote, wkt ukifika tutaamua
>
> kumpa nani kati ya hao. Je wewe ungependa nani apeperushe bendera ya
>
> CCM 2015?
>
>
>
> Hamisi Kigwangalla FacebookPage

Jamani Kigwangala kaleta wazo serious nami namuunga mkono. Hao waliotajwa tutake tusitake kwa CcM ya sasa ndo walio bora. Ni ukweli kwamba hata ukipita vijiweni majina hayo yanayotajwatajwa, na zaidi ya hapo baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikitaja majina hayo tangu baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2010. Mi ninaona hawa jamaa tuwajadili kwa performance zao na kwa njia ya elimination kama ifuatavyo:

1. Membe - Huyu hana lolote la maana analoweza kujivunia zaidi ya ubingwa wa fitna tu. Pia ana jeuri, hajali watu, anajikweza mno na ana makundi hivyo hafai.

2. Mwigulu - Ni mgeni katika siasa,ila ni mpambanaji, ana uzalendo, isipokuwa anapungukiwa uzoefu wa kuongoza Serikali, hivyo anahitaji muda zaidi.

3. Ngeleja - Huyu jamaa ni mpiganaji, mzalendo wa kweli, mtulivu, hana papara, hakurupuki, ana roho ya ya paka, ni mvumilivu balaa! Nakumbuka kwa utendaji wake mzuri alitumika kama Naibu waziri wa Nishati kwa kipindi cha mwaka ! tu akapanda. Na alikabidhiwa wizara ya Nishati na Madini katikati ya misukosuko ya Buzwagi, Richmond/Dowans,mgawo wa umeme, mafuta, na madini. Lakini ninamkubali kwa jinsi alivyosimamia sheria ya Madini ya 2010 ambayo inaipa Serikali fursa ya kumiliki hisa za bure migodini, pia inayataka makampuni ya madini kununua bidhaa hapa nchini na alipandisha mrabaha wa madini kutoka 3-4%. Aidha, alianzisha kupitia EWURA utaratibu wa kupanga bei elekezi na kikomo kwenye mafuta, akaanzisha uagizaji wa mafuta kwa pamoja(bulk procurement),akadhibiti uchakachuaji wa mafuta kwa kulinganisha ushuru kwenye dizeli, mafuta ya taa na petrol, n.k. Pia ndiyo muasisi wa bomba la gesi linalojengwa ambalo litashusha bei ya umeme kati ya 40-60%, n.k Huyu anajadilika na anaweza.

4. Nchimbi - Huyu hana record yoyote ya ya maana ila ni bingwa wa fitna. Aidha si mwaminifu,aliwahi kujiita Dr kabla ya kuhitimu PhD.

5. Dr Mwakyembe - Ni mchanga ingawa ni mchapakazi, ila ni mtu wa fitna, kisasi na makundi, anahitaji muda zaidi kwa sababu wakati mwingine hufyatuka bila consultations. pia ni mzushi aliyebobea.

6. Dr Magufuli - Hili ni jembe la ukweli isipokuwa anahitaji kufungwa gavana. Ni mpenda sifa binafsi, hashauriki na ana doa la kuuza nyumba za Serikali.

7. Wassira - Huyu ni kada wa ukweli ingawa umri unamtupa kisogo, ni mnafiki na mwenye choyo, alipokuwa NCCR Mageuzi alikuwa akiikashifu sana CCM, hivyo hafai. Amekuwa akisinzia bungeni.

8. Sitta - Huyu ni kada wa siku nyingi ila umri unamtupa kisogo,ni mfitini ile mbaya, ana choso na ni mtu wa kisasi na makundi. Ni muasisi wa CCK na akina Mwakyembe, hivyo hafai hata kidogo kwa sababu anaweza kukitelekeza Chama akiudhika.

9. Lowassa - Huyu ni kada wa ukweli,sifa yzake zinajieleza. ila ni mtu wa makundi, visasi, chuki na fisadi asilia!


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment