Sunday 12 May 2013

[wanabidii] Rais Jakaya Kikwete awateua Mabalozi wapya na kumhamisha mmoja

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, amefanya uteuzi wa Mabalozi Wapya kujaza nafasi zilizo wazi na kuanzisha Ofisi za Ubaloz inchini Uholanzi na Comoro.  Aidha Mheshimiwa Rais amefanya uhamisho wa Balozi kutoka kwenye kituo kimoja.

Mabalozi wateule na aliyehamishwa kituo ni kama ifuatavyo:-

1.    Bw. Wilson M. K. Masilingi, ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi. Bw. Masilingini Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa, Arusha, (AICC) na aliwahi kuwa Mbunge katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kati ya mwaka 1995 – 2010. Aidha, katika kipindi cha mwaka 1998 – 2005 alikuwa Waziriwa Nchi, Ofisi ya Rais mwenye dhamana ya masuala ya Utawala Bora.

2.    Bw. Chabaka Faraji Ali Kilumanga, ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Comoro. Hadi uteuzi huu unafanyika, Bw. Kilumanga alikuwa Balozi Mdogo katika ofisi ya Ubalozi nchini Uingereza.

3.    Bw. Modest Jonathan Mero, ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania kwenye Ofisi za Umoja wa Mataifa, Geneva.  Kabla ya uteuzi Bw. Mero alikuwa Afisa wa Mambo ya Nje Mwandamizi kwenye Ubalozi wa Tanzania katika Ofisi za Umoja wa Mataifa, New York.

4.    Kadhalika, Mheshimiwa Rais amemhamisha Balozi Philip Sang'ka Marmo kutoka Ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa China na kwenda Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani.

------MWISH0-----

(John M. Haule)
KATIBU MKUU,
WIZARA YA MAMBO YA NJE
NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA,
DAR ES SALAAM.

12 MEI, 2013


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment