Thursday 9 May 2013

[wanabidii] Mbunge anapojibu hoja za mbunge mwenzake waziri afanye nini?

Wana mabadiliko ninapotazama Bunge napata tabu sana. Mara nyingi mbunge yeyote yule anapotoa hoja katika kuchangia tunategemea Waziri wa wizara husika ndie atakaejibu hoja za wabunge wote wakati atakaposimama kutoa  majumuisho na kuwasilisha hoja rasmi.Lakini cha ajabu wakati mbunge kutoka kambi ya upinzani anapochangia na  kutoa hoja alizotumwa na wananchi wa jimbo lake, akimaliza kama anaefuatia kuchangia ni mbunge kutoka CCM  badala ya kutoa hoja zake alizotumwa na wananchi wa jimbo lake  anaanza kujibu hoja za mbunge mwenzake alizotoa na kukanusha yale aliyosema mbunge wa upinzani wakati hiyo ni kazi ya waziri na sio kazi ya mbunge.Sasa waziri yeye atafanya kazi gani? Hii imekaaje? ni kutetea chama au ni kuonyesha umahiri wa kuwakandamiza wapinzani ili pengine mbunge huyo aonekane anafaa na hatimae kupata cheo au ni nini? Sijui kama comrades mmeliona hilo.
Suleiman Swalehe

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment