Wednesday 8 May 2013

Re: [wanabidii] Zitto Kabwe : Taifa lina nyufa

Lo! Nani hakuelewa hotuba hii? Swala la BAKWATA mbona kaliweka sawa? Natumaini anayetaka ukweli amegundua. Ni swala la kukubali tu.

----------
Sent from my Nokia Phone

------Original message------
From: Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
To: "Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Wednesday, May 8, 2013 11:16:33 AM GMT+0300
Subject: [wanabidii] Zitto Kabwe : Taifa lina nyufa

NDUGU KABWE Z. ZITTO, MB – BUNGENI TAREHE 6 MEI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ili niweze
kuchangia leo katika mjadala huu muhimu sana.

Hapa Afrika kulikuwa kuna nchi, na bado ipo, inaitwa Ivory Coast. Ilikuwa
ni nchi ambayo inasifika sana kwa amani na utulivu; na ilikuwa ni nchi ya
kupigiwa mfano. Leo hii Ivory Coast imegawanyika vipande vipande. Ukienda
leo Ivory Coast unakuta wanaoitwa Ivorite na wanaoitwa wageni ambao wazazi
wao walienda Ivory Coast kufanya kazi miaka mingi sana. Lakini pili katika
mgawanyiko huo kuna mgawanyiko mkubwa sana wa kidini kati ya watu wa Ivory
Coast wanaotokea Kaskazini na watu wa Ivory Coast wanaotokea Kusini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tulikuwa tuna Sierra Leone nchi ambayo wageni
walikuwa wanakirimiwa katika hali ambayo haijawahi kutokea hapa duniani.
Lakini leo Sierra Leone ina rekodi kubwa sana ya watu wenye ulemavu kwa
sababu ya vita ya wenyewe kwa wenyewe.

Naomba nichukue nafasi hii kufuatia matukio ambayo yametokea hivi karibuni
na hasa jana na siku zilizopita ninanukuu hotuba ambayo Rais wa Awamu ya
Tatu Mheshimiwa Benjamin Mkapa aliitoa katika Bunge hili tarehe 4 Novemba,
1998. Alisema:

"Mr. Speaker, after three years of my presidency, I can dare to modify the
words of famous Zanzibar maestro Siti Binti Saada by saying, Tanzania is a
good country, let one who wishes to come do so. God has showered blessings
on our country. It is a country of unity, peace, love, rejoicing and
exciding generosity. It is a country of people who love equality and
justice. Our national unity brings from our firm believe in equality of
human beings before God and before the Law. A Unity reinforced by correct
policies of national building. Policies based on the principles of social
justice, peace, harmony and development for all. A unity which is extra
sensitive to policies, statements behavour and actions which may sore seeds
discard hatred and suspicious among Tanzanias"

Mheshimiwa Mwenyekiti sitatafsiri. Lakini naomba kila Mbunge ajiulize leo
iwapo Rais Mkapa tukimpa fursa ya kuja kuhutubia Bunge hili anaweza
akayatumia maneno haya tena? Hakuna mtanzania yoyote anayeweza kuthubutu
leo kutumia maneno haya tena kwa sababu nchi yetu ina nyufa. Ina nyufa
ambazo kwa kujua au kwa kutokujua sisi kama watu ambao tumepewa wajibi na
wananchi wa kuitunza nchi hii na kuipeleka pamoja tumejikuta tukiingia
katika kutoa kauli, maneno na vitendo ambavyo ni "irresponsible"
vinavyopelekea kugawanya nchi; na yanayotokea sasa ni matumizi ya nyufa
hizo.

Asubuhi hapa Mheshimiwa Lissu amesema, ametoa rekodi ya namna ambavyo
wanasiasa wa chama kinachoongoza (CCM) wamekuwa wakitoa kauli dhidi ya
vyama vya upinzani kuhusiana na masuala haya ya kidini. Wametoa mfano
kuhusu chama cha CUF kilipoitwa chama cha waislam, wamekitolea mfano kuhusu
CHADEMA kinavyoitwa mpaka sasa chama cha wakristo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, inawezekana ikawa ni rahisi sana tuka-"point
fingers" kwa wenzetu nyie, ni rahisi sana; lakini CUF wakati wanaitwa ni
chama cha waislam ambao walikuwa hawaitwi ni chama cha waislam
hawakunyoosha mkono kupinga. Wakati CHADEMA kinaitwa cha cha Kikristo ambao
hawaitwi hivyo hawakunyoosha mkono. Matokeo yakeni nini? Tumejenga hofu
kubwa sana katika Taifa na hii ni lawama kwa wote. Wote kama nchi ili
tuseme kwamba hapa tumekosea na tuanze upya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, adui anapokuja kwenye nyumba anaangalia ni wapi
ambapo ni rahisi kamba kukatika. Tumeji-"expose", tumejiweka wazi. Leo mtu
anayetaka kuishughulikia Tanzania ata-deal na udini tu. Kwa sababu anajua
watanzania hivi sasa wamegawanyika katika misingi hiyo. Jana limetokea
tukio Arusha, angalia kwenye mitandao ya kijamii mara moja watanzania
wenyewe kwa wenyewe na ukiangalia majina ya watu wanaojadiliana wanaanza
kusemana kwa dini zao. Ndiyo hatari ambayo tumeifikia; na ndio anachokitaka
adui. Ni hicho. Atakuja, wanaitwa "Agent Provacateur", watapiga, mtabaki
mnagombana ninyi. Tukiruhusu NYUFA hizi ziendelee hatutakuwa taifa. Ni
lazima sote kwa pamoja tusimame imara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, waislam na wakristo nchi hii hawana chuki kwa sababu
wanaishi pamoja, ni marafiki, ni ndugu na kama ingekuwa kwa mfano waislam
wanawachukia wakristo waislam wangevunja makanisa au wangechoma makanisa au
wangewalipua wakristo. Wakati wa tukio la Mwembechai ndipo ambapo Polisi
waliingia mskitini wakaua watu, wanawake wakateswa kwenye magereza na
kadhalika, watu wakakaa miezi mitano gerezani bila kushtakiwa lakini
hapakuwa na mtukio yoyote ya namna hii. Waislam na wakristo wa nchi hii ni
wamoja. Wananchi wetu ni wa moja lakini sisi viongozi kwa kutoa kauli
ambazo ni "very irresponsible" tunawagawa watu wetu na ni lazima tukatae
hali hii. Tunafanya nini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, lazima twende mbele. Kwanza ni lazima sasa Serikali
ijenge utamaduni wa kufuatilia "grievances" zote ambazo wananchi wanazo
bila kujali dini zao. Pili turuhusu watu kuwa huru kusema. Nimesikia hapa
watu wanasema kwamba maandamano ni tatizo nakadhalika. Maandamano si
tatizo, ukimzuia mtu kuandamana akiweka hasira zake kesho atafanya nini?
Atatoka na bomu. Turuhusu "honest discussions" miongoni mwetu kama wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatu ni lazima sasa tuseme ya kwamba ni marufuku
kuwa na kauli za chuki "hate speeches". Kama hatuna vipengele vya kisheria
tutunge sheria kwa sababu kumekuwa na "hate speeches" nyingi sana katika
hii nchi na hakuna hatua ambazo zinachukuliwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, state, dola, ihakikishe inajiondoa kwenye shughuli
za uendeshaji wa mambo ya kidini. Ijiondoe kabisa. Kwa mfano kuna lawama ya
muda mrefu sana ya waislam kuhusu BAKWATA, Waislamu miaka mingi toka mwaka
1969 wakati Serikali imeunda BAKWATA wanalalamika. Leo hii Serikali ikitaka
kuzungumza na waislam inafanya nini? Inaenda kuwaita BAKWATA. Hawana
legitimacy ya waislam, hamtaweza ku-addres masuala ya waislam lakini ni
rahisi sana kuweza kuongea na CCT kwa sababu CCT ni chombo ambacho kina
uhuru wake. Kwa hiyo Serikali ijiondoe kwenye uendesheji wa shughuli za
kidini. Hapa ndipo tutakapoweza kuhakikisha kwamba tunakuwa na nchi moja
nchi ambayo ina amani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namaliza kwa kusema nchi hii si ya waislam peke
yake, nchi hii si ya wakristo peke yake. Nchi hii si ya CCM au ya CHADEMA,
CUF au ya NCCR-Mageuzi au TLP na kadhalika. Nchi hii ni moja, nchi hii ni
ya Jamhuiri ya Muungano wa Tanzania. Lazima wote tusimame kuhakikisha
tunailinda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushuru sana asante.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.



--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment