Thursday 23 May 2013

Re: [wanabidii] UPDATES ZA KINACHOENDELEA MTWARA NA SAKATA LA GESI


Mmmmmmmmmmm. Kama ni kweli, kinauma sana. Ebu tafakari kama ni mama yako, baba yako, mtoto wako, kaka yako, dada yako au ndugu yako wa karibu au rafiki yako anafanyiwa haya katika nchi inayodhaniwa kuwa ni ya amani, Tanzania! Baba wa taifa Mwalimu Nyerere, nakulilia machozi ya huzuni  sana  sasa kama vile umekufa leo. Nakulilia kwa sababu ya wanawake, watoto, vijana, wababa na wababu wa Mtwara walioko katika dhahama. Mungu ibariki Tanzania.
 

From: Juma Mzuri <jumamzuri@gmail.com>
To: Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Thursday, May 23, 2013 4:05 PM
Subject: [wanabidii] UPDATES ZA KINACHOENDELEA MTWARA NA SAKATA LA GESI
  • Kuna madai ambayo hayajathibitishwa kwamba wanawake wanabakwa na maaskari, wanapigwa risasi kutokana na vijana wote kukimbia maporini.
  • Mwanamke anayekadiriwa miaka 25 mjamzito auawa kwa kupigwa risasi maiti ipo Ligula.
  •  Mwanafunzi wa CHUNO afikishwa hospitali  Ligula na majeraha ya risasi mguuni.
  • Maduka maeneo ya Magomeni yamechomwa moto ikiwamo pia mali za Askari magereza na uhalifu ukifanyika vidole vinawaelekea Polisi.
  • Afisa Usalama wa Taifa ambaye anamiliki nyumba ya wageni naye amevamiwa na kuporwa mali ikiwamo fedha katika gesti yake. Haijajulikana ni kiasi gani cha mali kilichopotea.
  • Mabomu yanaendelea kupigwa tofauti kwa sasa hayapigw mfululizo.
  •  Mabomu yametulia. Hali ya ukimya imetawala.
  • Mabasi 5 ya Champion yamebeba Wanajeshi yako njiani yanakuja.
  •  Serikali yatoa tamko yasema watu 91 wanashikiliwa.
  • Bunge laahirishwa tena. Kupisha uchunguzi na kuepusha uchochezi kutoka kwa baadhi ya wabunge. (Kwa mujibu wa Spika)
  •  Maeneo ya Magomeni, Chikongola, Nkanaledi, Mikindani  maaskari wanaingia majumbani mwa watu na kumsomba mtu yeyote ambaye ni mwanaume awe amehusika awe hajahusika na kumkamata. Pia inaripotiwa na uhalifu unafanywa na maaskari hao hao.  Jambo linaloamsha hisia kwa wananchi.
  • RPC anaongea na vyombo vya habari na kuwasihi wananchi waende makazini. Lakini kiuhalisia hali sio shwari.
  • Mahakama ya mwanzo ya Mitengo imechomwa moto
  • Mpaka sasa ni vita baina ya wananchi na maaskari. Mabomu yamesikika pamoja na milio ya risasi masaa 24. Na milio ya Risasi na mabomu inaendelea kusikika.
  • Raia wapatao 7 wameripotiwa kufariki (wengine walipelekwa hospitali ya Ndanda Ndogo na mmoja ameripotiwa kupokelewa Ligula.
  • Nyumba za viongozi zinaendelea kuchomwa moto.
  • Majibizano baina ya Polisi na Raia yanaendelea maeneo ya Magomeni, Nkanaledi na Mikindani.
  • Maduka yamefungwa na hakuna huduma zozote
Barabara zimewekwa vizuizi magogo na matairi yamechomwa moto. Hakuna njia ya kupita.  
MTWARA LEO
PICHA NA FARID HEMED

-- Send Emails to wanabidii@googlegroups.com Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer:Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.--- You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.  

0 comments:

Post a Comment