Friday 17 May 2013

Re: [wanabidii] UJERUMANI INAHUSIKA NA MGOGORO WA GESI MTWARA

Mbona utafiti huu wa gas na mafuta baharini unafanyika Mafia kuanzia miaka mingi 2007-2008 hivi na ni ile meli ya utafiti ndio wasomali wakitaka kuiteka! Mbona kule hakuna vurugu na kuna kampuni na watumishi wa kigeni. Huko Mtwara kulikoni?

Mtwara, Lindi wana bahari poa na wana resources za kila aina za ardhi nzuri. Wana mabonde mazuri na poa sana na mashirika ya maendeleo kibao wanaohamasiosha uzalishaji mihogo, ulezi, mtama, mbaazi zinakua huko balaa na kilimo cha mpunga kwa umwagiliaji maji. Kuna maembe kichizi Bakhresa ananunua, minazi sijapata kuona Lindi-Mtwara kama mchicha. Utalii wa Kilwa kuunganishwa na wa Mikindani. Jamani kuna chuo cka Kilimo-Naliendele na Miradi ya Clinton Foundation (CHAI) ya ujenzi na uboreshaji wa Zahanati/Health centres, FAO, CONCERN na miradi ya Idara ya Kilimo. Kuna mpaka miradi ya kilimo mpaka ng'ombe na mbuzi wa kisasa wa maziwa. Wageni kibao Mtwara wa utafiti wa mafuta na Gas hoteli zimejaa wanafanya biashara kuuza mazao. Mandege na helikopta zinaruka kama vipepeo na wamejenga extension ya airport kwa videge vyao. Wasomali wameingiaje haijulikani wamefungua mahoteli huko. wahindi, wachina, wazungu wanachangia pato wako huko bwerere. Jane Goodall Foundation wapo ktk kuhamasisha value added crops na MKUHUMI masuala ya misitu na tabia nchi (REDD) na its benefits inapamba moto miaka. Lakini ukipita vijijini vijana barazani wanacheza karata na kuchoma vihindi, malundo ya nazi na makumbi; mikorosho na michungwa porini, mabonde mazuri ya kilimo tupotupo tu tumekaa kitako walimao wazee. Kimbilio ni DSM sio kilimo tumuuzie Bakhresa maembe mafupi bali ni ile miti mirefu aliyoacha babu. wamejazana Lindi na Mtwara mjini biashara ya vitu kutoka china, Indonesia etc vinguo, baiskeli, vyombo vya nyumbani etc sio kilimo-retail trade ya industrial goods from abroad ndio predominant.

Vijijini michungwa East Africam tall ipo porini inaivunwa kutoka porini kukua na kuzaa inashindana na kivuri cha miti pori.

H
ata tuandamane kuhusu Gas-hatutofaidika sana bila ya sisi wenyewe wazawa kuongeza juhudi katika kilimo na ardhi nzuri ipo bwerere. Gas na mafao yake itatuongezea kuboresha miundo mbinu ili tuweze kusafirisha mazao kwenda Msumbiji, Namibia, Botswana kutumia Southern Corridor na kuleta DSM kupitia daraja la mkapa. Makumbi ya nazi na vifuu tusichome moto tusuke mazuria, mapambo kupata hela na vifuu mapambo. Utaona njia yote kijijini kila nyumba inauza petroli nje ktk chupa za plastiki kuwauzia bodaboda. Mtoto miaka kumi hajaanza shule anawinda ndege. Walimao ni wazee tu vijana kitako kucheza pool asubuhi saa moja utawaona ambapo huchezwa kama kamali.

Hata tuandamae, tuchome nyumba za viongozi kama tunakaa na kubweteka watakuja wengine kutoka mikoa mingfine na kutumia nafasi zilizopo mkaendelea kukaa na kupambana, kufungwa na kuacha familia zeunu zinateseka. Adui yako-ni wewe mwenyewe usiyejituma na kupenda kujiendeleza. utachoma nyumba, utaua at the end of the day-hujasoma hutopata kuajiriwa budi ujiariri; percent ya mafao itakayokuja itakuwa'shared benefits' za huduma sio kukujaza wewe hela. Je, utaweza kujikwamua bila ya wewe kujituma ukazalisha mali? Ona ktk kisogo chako pia sio cha mwenzako tu.
 
--- On Fri, 17/5/13, Emmanuel Muganda <emuganda@gmail.com> wrote:

From: Emmanuel Muganda <emuganda@gmail.com>
Subject: Re: [wanabidii] UJERUMANI INAHUSIKA NA MGOGORO WA GESI MTWARA
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Friday, 17 May, 2013, 13:56

Hivi, ninyi CCM mtaendelea kutafuta mchawi mpaka lini? Mmeshindwa kuipakazia Chadema sasa mnakuja na singo ya Ujerumani.
Hivi mnadhani Watanzania ni mazuba kiasi hicho? Watu wamechoshwa kunyonywa na ubinafsi wa serikali ya CCM.
em

2013/5/17 Yona F Maro <oldmoshi@gmail.com>
Ndugu zangu

Kwa taarifa ambazo sio rasmi na ambazo zinaendelea kufanyiwa kazi
usiku na mchana sasa hivi kidole cha uhusika wa vurugu kadhaa
zinazohusiana na gesi mkoa wa mtwara na lindi kinanyoosha  kwa taifa
la ujerumani na maslahi yake kwa gesi na mafuta katika maeneo ya
mwambao na karibu na huko .

Ombi langu ni kuwataka watanzania wenzangu kutokuingia kwenye mitego
hii .

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment