Mimi sielewi; Mwananchi anapokula njama na kutumia suala la Gas kama kitu cha kumfanya aanze kuchoma nyumba, kuharibu mali za wasio na hatia, kuvunja madaraja kwa baruti, kukata miti ya umeme kwa vile wa upande mwingine wamegoma kuandamana kuwakomoa wasipate umeme. Kisha baadhi wa wanakijiji wenzake wakaungua na kufa kwa moto achomao; wakampiga mtumishi wa serikali au muandishio; akina mama na wagonjwa wakakosa huduma hospitali kwa vile usafiri wa aina yoyote utachomwa moto ukionekana barabarani na daraja limebomolewa. Baada ya uharibifu wote huu wa mali nyingi, kinaingia kikosi cha jeshi. wananchi wana silaha za jadi za mishale ya sumu, mikuki, mawe na matairi na petroli ya kuwasha moto tairi na magogo njiani. Wanajeshi wa Serikali inabidi watumie silaha kali ambazo zinaua-wakapigwa wachache wakafa au mmoja akafa. Hili linakuwa ni kosa kubwa ilioje kuliko makosa yote waliyofanya wananchi! Fikiria kati ya aliyeuawa ni baba au ndugu yako aliyegoma kuandamana au akienda shamba kwa gari lake hajui kinachoendelea. Na aliyepigwa risasi ni yule akiwalenga mshale wanajeshi au akitumia silaha aliyokuwa nayo ya bunduki au aliyekuwa akikatiza ikampata kwa bahati mbaya. Yaani daima ni askari tu wakosa waannchi ni clean? Je, ikiwa daima twaona upande mmoja tu wa GVT tukiambiwa tunajitafutia umaarufu wa NGO zetu au mashirika yetu kuonekana ili yapate misaada daima kwa kutumia suala la gas kama issue itakuwa kosa? Mimi ninaona, shirika ambalo linapenda kusaidia kukomesha vurugu hizi, lijipange, au litafute hela na kupanga mpango mkakati, au lijitolee kufanyakazi na GVT ya kujua ni kitu gani cha kuwaelimisha wananchi waelewe kuhusu mafao yao katika gas hii ili kuelimisha wananchi kieleweke. Ikiwezekana, serikali, izidi kutoa kimaandishi magazetini kwa mwaka, itoe tarehe na majina, mafao yote ambayo yamekwisha kupatikana na kutolewa maeneo ya mali asili-gas_Mtwara, Songosongo etc; Umeme (Pangani, Kidatu, Kihansi, Mtera), uwekezaji mfano ktk machimbo ya almasi, dhahabu, makaa ya mawe etc, Mbuga za Hifadhi- Mikumi, Udzungwa, Loliondo, Ruaha, Seleous, NCAA, Mkomazi, Kigoma Malagarasi etc. Kuwe na gazeti moja la serikali liandikwe kiingereza na Kiswahili kila baada ya miezi 6 litoe taarifa na takwimu nchi nzima. Wasiogope kuorodhesha hata majina ya waliosomeshwa hata wakiwa ni watoto wa madiwani na wabunge list ndefu maana wengine wakiambiwa kuchagua wafaidika wanachagua jamaa zao huku wao ni viongozi au wachaguliwa wawakilishi wa wananchi ila wanajipa wenyewe kipaumbele, kisha wanasaidia kuwatia wananchi hamasa za vurugu kuficha maovu yao. Nani kaenda ziara-aandikwe; kapata scholarship, mikopo, mafunzo ya ujasiriamali etc. Baada ya wananchi kufanya vurugu kuua wafanyakazi au kuharibu mali zao, kisha watataka kusaidiwa na hao hao wafanyakazi mfano wa zahanati, hospitali, polisi na mahakamani-jee wanaelewa matokeo ya kuchomea watumishi wa GVT au mashirika binafsi mali zao na kisha kuhitaji msaada toka kwao wakiwaendea kazini au shuleni? Vurugu hizi, zitawapa mwanya wahamiaji haramu kupita, askari toka congo walioadhimia kuja kutukomoa kuja kutujua kutuwekea mbinu za kutuua; majambazi kuingia maeneo kuua na kufanya vurugu maana wanajua chuki iliyojengwa kwa police, FFU, JWTZ hawatofika mapema wakiitwa vijijini kusaidia- hawatokwenda. Tunajichimbia kaburi. Jinsi magari binafsi na nyumba zilivyochomwa ni si jambo la kufurahia kwamba GVt imekomoka, ni la kusikitisha. Mbona tunachomeana nyumba kila siku na kuuliana familia, kuibiana mifugo kila mwezi na kuuana, kuvamia magulio na kupigana risasi, kuwaficha wakimbizi na kuwapitisha wahamiaji haramu, kupanda na kuuza bangi na kusumbua askari kuzing'oa; kukata viungo albino, kuoza wasichana wadogo kisha tunatoa taarifa amefariki au amehama shule kumbe kapelekwa kwa mume; kumbaka msichana au ma nakisha kumkata viungo na serikali inateseka kutuelimisha na hatuelimishiki. Na NGO zinashindwa kuelimisha wananchi haya yanakotokea ndani ya koo na vijiji ili yaishe. Leo haki hii ipo tu pale GVT inapopambana na wananchi? Sio pale wananchi wanapouana wenyewe kwa wenyewe daily-NO, zinakaa kando? hatuoni kuwachachamalia hao wananchi na kuwazingira kudai haki muuaji na mchomaji nyumba kwa Imani za kishirikina akamatwe na yale magomvi ya Batemi na Loita na kunyonga vitoto vifugaji masuala ya karne before and after independence yaishe maana na huko nako NGO za haki na maendeleo ni kila kijiji. Excuse me! Ninauliza maana ninaona kama issue hizi za haki na usalama wa raia zinanichanganya. matumizi ya nguvu nikiangalia TV nchi nyingine wanavyopambana na wananchi na askali kufatua risasi wakaua na kuuana askari na wananchi-ninaona hapa Tanzania nguvu bado kidogo. kama ile ya S.Afrika. walipofyatua risasi chache wananchi-askari wakajibu kwa kuzimimina. Ni hivyo India, Pakistan na wanavyobondana Uk na USA. Ni tatizo la sisi waafrika kytaka kusifiwa. kama mtu akikupinga maoni na tabia zao-unamfanya adui. Hivyo hata ukiwa unafanya vurugu mwandishi anaona si vizuri asiseme aseme ni vizuri ili usimpige? huu utakuwa utoto yaani daima mwandishi au mtu wa radio akusifie tu ili asije akapigwa? ujinga. kusema mbaya wakati si nzuri ni bora kuliko kupaka mafuta kwa mgongo wa chupa. Viwanda Dar vipo vingi Mtwara ndio vitaanza, gas lazima ije Dar, Morogoro, Tanga na Mbeya kuvifufua na kuvipunguzia gharama ya umeme. --- On Sun, 26/5/13, Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com> wrote:
|
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment