Thursday 9 May 2013

Re: [wanabidii] Re: [Mabadiliko] Neno La Leo: Ya Arusha Na Kamba Inapokatikia...

MIKE ZUNZU
 
Wakinyongwa kumi wengine watakaa kwenye mstari kuliko hali ilivyo! mbona china wananyonga na wachina waliosafi wapo na wanaendeleza nchi? tatizo hapa kwetu watu wanaoneana haya unaiba hela ya umma unaambiwa rejesha na mambo yanaisha hii sio sawa hata kidogo, na ukumbuke ni baada ya watu kugundua je wasingegundua nani angelejesha huoni watu kama hawa walistahili kunyongwa kwani una udugu nao mpaka uwaonee huruma au na wewe ni mmoja wao,
 
 Hawa wote walioko madarakani asilimia 80 ni wezi wanastahili kunyongwa lakini kwa vile wao ndo kila kitu hatujakata tamaa siku si nyingi atakuja mtu tofauti na wao tutataka kila alieiba akishuhudie kitanzi ndipo akili zitawakaa sawa watakaobaki. je si unawaona wanavyotoa maneno ya kejeli kule bungeni?


2013/5/8 Augustine Rukoma <arukoma66@gmail.com>
Mantiki ya deo ni muhimu kuitafakari haka bomu kana uwezo mdogo
hakahitaji watu kutoka uarabuni. Sasa sana vnaweza elewakama wa tz
walipewa mafunzo yakukatengeneza kutoka uarabuni

On 5/7/13, Martin Mkenda <mgmkenda@gmail.com> wrote:
> Deo,
> Awe ametoka uarabuni au china....ni gaidi tu....
> Kwa sasa sio busara kusema kwa hakika kwamba hao wasaudi wanahusika ama
> la....na kuhusika sio kuleta bomu tu....hata kuwezesha utengenezaji!
>
>
> 2013/5/7 Deogratius J. Koyanga <deokoyanga@gmail.com>
>
>> kaka Mjengwa, hakuna tukio la ugaidi Tanzania, bomu gani la kigaidi lile?
>> tutafakari hata uwezo wa bomu lenyewe tusipotoshe jamii. Mtu atoke
>> uarabuni
>> hadi Tanzania kuja kurusha Bomu ambalo haliwezi hata kudhuru watu 10?
>> mimi
>> ninaamini walioliterngeneza bomu na kulirusha ni watanzania wenzetu na
>> wapoa hapa hapa tusiwasingize waarabu. tunapotoshwa sana na kusukumwa na
>> hoja za wazungu kuaminishwa kuwa kila mwarabu ni ghaidi. kila  mlipuko
>> umetoka uarabuni. ni upotoshaji huo.
>>
>> Tumsake mchawi wetu hapa nyumbani na tukomeshe huu unyama.
>>
>>
>> ----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
>> *"Ufalme wa Mungu umekaribia, Tubuni na kuiamini Injili..."Mark 1:15*
>>
>>
>> 2013/5/7 Maggid Mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com>
>>
>>>
>>>
>>>
>>> Ndugu zangu,
>>>
>>>
>>>
>>> HAYA ni moja ya maandiko yangu muhimu katika  kazi yangu ya uandishi na
>>> uelimishaji jamii.
>>>
>>>  Ni kwa kutambua ukweli, kuwa nchi yetu imepatwa na shambulizi la
>>> kigaidi. Imetokea Arusha, ingeweza kutokea popote pale katika ardhi ya
>>> nchi
>>> yetu. Tunawapa pole wahanga wa tukio hili. Ni msiba wetu sote.  Tuwe
>>> sasa na mioyo ya ustahamilivu.  Tusikimbile kunyosheana vidole. Tuwaache
>>> tuliowapa dhamana ya kuchunguza waifanye kazi yao. Wajibu wetu wa
>>> kizalendo
>>> ni kutoa ushirikiano.
>>>
>>>
>>>
>>> Naam, kama nchi, tunapitia sasa kwenye kipindi cha majaribu makubwa. Huu
>>> ni wakati wa kuizunguka bendera yetu ya taifa. Ni wakati wa kuonyesha
>>> umoja, uzalendo  na mshikamano wetu kama taifa. Umoja, uzalendo  na
>>> mshikamano wetu ni silaha muhimu na kubwa kabisa Watanzania tumeendelea
>>> kuimiliki tangu enzi na enzi. Ndio silaha tunayoendelea kuimiliki hadi
>>> sasa. Tuna lazima ya kupambana hadi risasi ya mwisho kuhakikisha adui
>>> hatupokonyi silaha hii.
>>>
>>>
>>>
>>> Ndugu zangu,
>>>
>>>
>>>
>>> Hii ni Nchi Yetu. Ni nchi yetu sote, Watanzania wa imani zote. Tutambue
>>> sasa, kuwa kwenye safari tunayokwenda kama taifa, mbele yetu kuna
>>> mawimbi
>>> makubwa. Kwa pamoja tutavuka, kwa kugawanyika tutazama.
>>>
>>> Wahenga wetu walisema; kamba hukatikia pabovu. Watanzania wa imani
>>> tofauti tuna historia ya kuchanganyika na kuishi kwa amani na upendo.
>>> Hatuna hulka ya kubaguana. Tukianza sasa dhambi ya kubaguana, basi,
>>> itaendelea kututafuna.
>>>
>>> Na siku zote, uzoefu ni mwalimu mzuri . Mathalan, uzoefu unatufundisha,
>>> kuwa kuwasha moto ni jambo jepesi sana, lakini, kuuzima moto,  ni kazi
>>> ngumu sana.
>>>
>>> Ona, moto ulioanza kwenye nyumba moja ya nyasi kijijini, waweza kusambaa
>>> haraka na hata kuteketeza kijiji kizima. Na tangu utotoni
>>> tumetahadharishwa
>>> hatari ya kucheza na moto.
>>>
>>> Naam, binadamu usicheze na moto, labda iwe kwenye mazingaombwe.
>>>
>>> Na ningependa hapa  tuyakumbuke maneno ya busara na hekima nyingi kutoka
>>> kwa Bi. Joy Mukanyange ( Pichani). Huyu alikuwa Balozi wa zamani wa
>>> Rwanda
>>> nchini Tanzania. Mama huyu aliyatamka maneno haya miaka 13 iliyopita,
>>> takribani miezi sita kabla ya kifo cha Baba wa Taifa. Bi. Joy Mukanyange
>>> alikiona kile ambacho Watanzania hatukukiona. Ni kama vile alikuwa
>>> mtabiri,
>>> maana, alichokisema mama yule leo ndio tunaanza kukiona. Siku ile ya
>>> Aprili
>>> 6, 1999, katika iliyokuwa Kilimanjaro Hotel, Bi Joy Mukanyanga
>>> aliyatamka
>>> haya;
>>>
>>>  " Naogopa, kwani nimeanza kuona dalili zinazojengeka za mgawanyiko wa
>>> kidini nchini Tanzania na eneo lote la Maziwa Makuu, hali ambayo inaweza
>>> kusababisha maauji ya halaiki kama yale yaliyotokea nchini mwetu mwaka
>>> 1994." Alisema Balozi yule wa Rwanda kabla ya kuendelea kutoa ufafanuzi
>>> wa
>>> historia ya Rwanda na matukio yaliyosababisha mauaji yale ya Wanyarwanda
>>> ya
>>> wao kwa wao. Ndio, Bi Joy Mukanyange alikiona kile ambacho Watanzania
>>> hatukukiona.
>>>
>>>
>>>
>>> Na tutafanya makosa makubwa, kama hata sasa, tutajifanya kuwa hatukioni
>>> kile ambacho Balozi Joy Mukanyange alikiona . Watanzania tukubali sasa
>>> kuwa
>>> tumepatwa na bahati mbaya sana ya baadhi ya Watanzania wenzetu kuanza
>>> kupandikiza mbegu za chuki miongoni mwetu. Kuna wanaotaka tuanze
>>> kubaguana
>>> kwa misingi ya kidini.
>>>
>>>  Hili ni jambo la hatari sana. Ni hulka ya mwanadamu, anapokuwa
>>> matatizoni kumtafuta kondoo wa kafara. Mtu mwingine wa kummyooshea
>>> kidole
>>> kwa matatizo yake. Hali duni ya uchumi wa nchi, hali duni za maisha na
>>> umasikini wa watu wetu isiwe chachu ya kuanzisha vurugu za kijamii.
>>>
>>> Maana, taratibu tumeanza kuizoea misamiati ya sisi na wao. Mathalan,
>>> sisi
>>> Wakristo na wao Waislamu. Sisi Wachagga na wao Wazaramo. Tunasahau, kuwa
>>> katika nchi yetu hii hakuna Sisi na Wao, kuna SISI tu.Tutakapokumbwa na
>>> maafa ya kitaifa watakaoathirika ni SISI, hakutakuwapo na WAO.
>>>
>>> Hatari kubwa ninayoiona ni tatizo la wengi wetu kuwa na ufahamu mdogo
>>> juu
>>> ya dunia tunayoishi sasa, kibaya zaidi, ufahamu mdogo wa historia yetu.
>>> Hivyo basi, kupelekea hali ya kutojitambua kama taifa.
>>>
>>> Ndio, uelewa wa historia ya jamii husika ni jambo muhimu sana. Kiumbe
>>> huwezi kuelewa ya leo, kesho na kesho kutwa kama huelewi ya jana.
>>> Kuielewa
>>> historia yako ni kuelewa ulipo na unakokwenda. Historia ni kama maji ya
>>> mto, yakipita hayarudi. Historia ni wakati, ni muda. Kihistoria jana ni
>>> sawa na zamani.
>>>
>>> Karne nyingi zilizopita wahenga wetu walitafsiri muda kama mkusanyiko wa
>>> matukio ya zamani na sasa. Waliamini kuwa yaliyotokea zamani na
>>> yanayotokea
>>> sasa ndiyo yenye kusaidia kubashiri yatakayotea kesho, yataamua
>>> mustakabali
>>> wetu.
>>>
>>>  Dalili tunazoziona sasa za kupandikiza mbegu za chuki kwa misingi ya
>>> udini si dalili njema. Haya yatatupelekea kwenye maafa. Tuliopata bahati
>>> ya kutumia kalamu zetu hatuna budi kuliweka hili hadharani. Ni wajibu
>>> wetu
>>> wa kizalendo.
>>>
>>> Narudia, Hii ni Nchi Yetu. Katika ulimwengu tunamoishi kuna mamilioni ya
>>> watu ambao hawana nchi. Wahenga wetu walishiriki katika kuijenga nchi
>>> hii,
>>> wametutarajia sisi tuendelee kuijenga na kuilinda heshima na hadhi ya
>>> nchi
>>> yetu. Mengine yanayofanyika sasa sio tu yanaitia doa nchi yetu, bali,
>>> yanaiaibisha nchi yetu.
>>>
>>>  Ndugu zangu,
>>>
>>> Hatuna haja ya kubaguana kwa misingi ya dini, ukabila na rangi. Sisi
>>> wote
>>> ni Watanzania. Tuna historia ya kujivunia. Ni historia yetu wenyewe.
>>> Kinyume na baadhi yetu wanavyofikiri au wanavyotutaka tufikiri, historia
>>> yetu haikuanzia enzi za Mwarabu , Mjerumani au Mwingereza. Historia yetu
>>> haikuanzia enzi za TANU wala Afro Shiraz.
>>>
>>>  Na dini hizi za kimapokeo zinazotufanya sasa tufarakane zimekuja na
>>> kuzikuta dini zetu za asili, na bado tunazo. Na hakika, Afrika
>>> hatugombanii
>>> matambiko. Afrika kila ukoo una tambiko lake, hivyo basi, dini yake.
>>> Kamwe
>>> hutasikia Waafrika wanagombania matambiko. Hutasikia Waafrika
>>> wakigombana
>>> kwa tofauti za matambiko yao.
>>>
>>>
>>>
>>> Na sisi ni Waafrika. Hii leo mahala ambapo unaweza kuwagawa Watanzania
>>> na
>>> hata kufanikiwa kuwafanya wachinjane ni kwenye kwenye tofauti zao za
>>> imani hizi za kimapokeo; Uislamu na Ukristo.
>>>
>>> Naam; kamba hukatikia pabovu. Tusikubali dini iwe ndiyo penye ubovu
>>> kwenye kamba inayotuunganisha Watanzania.  Nahitimisha.
>>>
>>> Maggid Mjengwa,
>>>
>>> Msamvu, Morogoro.
>>>
>>> 0754 678 252, http://mjengwablog.co.tz
>>>
>>>
>>>
>>> --
>>> Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
>>> Kuchangia mada tuma kwenye Email hii:
>>> mabadilikotanzania@googlegroups.com
>>>
>>> Kujiondoa Tuma Email kwenda;
>>> mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
>>> Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
>>>
>>> TEMBELEA Facebook yetu:
>>> http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
>>>
>>> For more options, visit this group at:
>>> http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
>>>
>>> ---
>>> You received this message because you are subscribed to the Google
>>> Groups
>>> "Mabadiliko Forums" group.
>>> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send
>>> an
>>> email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
>>> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>>>
>>>
>>>
>>
>>  --
>> Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
>> Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
>>
>> Kujiondoa Tuma Email kwenda;
>> mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
>> Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
>>
>> TEMBELEA Facebook yetu:
>> http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
>>
>> For more options, visit this group at:
>> http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
>>
>> ---
>> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
>> "Mabadiliko Forums" group.
>> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
>> email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
>> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>>
>>
>>
>
>
>
> --
>
> Martin Mkenda
>
> --
> Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
> Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda;
> mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
> Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
>
> TEMBELEA Facebook yetu:
>  http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
>
> For more options, visit this group at:
> http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
>
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Mabadiliko Forums" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>
>
>

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.



--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment