Wednesday 8 May 2013

Re: [wanabidii] Re: [Mabadiliko] Neno La Leo: Ya Arusha Na Kamba Inapokatikia...

Dada Khildegarda,
"Ukitaka tuwe kama China kunyonga au kuua mtu akitoa au kupokea rushwa au kufisadi-utaua wangapi" Nimenukuu sentesi yako hiyo kwasababu nahitaji kuilinganisha na kauli ya jamaa mmoja bwana Imran Khan wa Pakistan, kwenye kampani za kuwania urais wa nchi hiyo alisema yeye akichaguliwa ata deal na wala rushwa, kwamba katika viongozi wa Serika 80% ni wala rushwa au alishakula rushwa wakiwa madarakani, kwamba kama ni kwa mfumo wa sheri za nchi za magharibi watu hao wangelikwa vifungoni, akasema hata hao 20% ni questionable kana hawana doa.
Hivyo upo sahihi, tatizo wenzetu wameshika mpini na sisi tumeshika ncha ya upanga, je tutaweza kufurukuta kweli? 


From: Hildegarda Kiwasila <khildegarda@yahoo.co.uk>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Wednesday, 8 May 2013, 7:31
Subject: Re: [wanabidii] Re: [Mabadiliko] Neno La Leo: Ya Arusha Na Kamba Inapokatikia...


Arusha ni mji wa Kimataifa na wa Kitalii-wamepata pa kuharibu jina na uchumi hata wa vijana wetu wa sekta ya utalii ambao wapo busy masaa 24. Kamba imekatikia mahala imara badala ya pabovu kama DSM mwembechai, Buguruni, Mbagala, Liwale, Ruangwa.

Tutafanya nini wakati mtanzania kichwa cha mwendawazimu, maneno mengi vitendo hakuna au pungufu vya kujenga maendeleo? Ukitaka tuwe kama China kunyonga au kuua mtu akitoa au kupokea rushwa au kufisadi-utaua wangapi maana fisadi hata aliyeajiriwa leo anafisadi kesho unamuona na gari ya kusotasota. Baada ya nusu mwaka-anajumba la ufahari. Kama ni police-ana kitambi balaa ana DCM na ikikamatwa ni bovu abiria mnasikia dreva anasema-hii hapa karatasi gari hii ni ya afande.... Police anawaruhusu muondoke maana ni junior asije akakosa kazi. Ndio hawa wanaweza kutumika hovyo hawana uchungu na nchi na jamii zao bali macho ku-pesa tu!!

Kijakazi mtumwa kutupa bomu kanisani anaweza kuwa katumwa akarushe bomu kanisani ili limuue mwakilishi wa Papa apate pesa. Ni sawa wale wa kukata albino mikono ili eti apate milioni 600-ana wazimu. azipate wapi-amekamatwa.

Pesa si mchezo na list nzima ya maharamia inaweza kuwa wakristu- si fedha mamilioni yataingia wameahidiwa? anajua ataua ndugu zake lakini anachoangalia ni kitu hela tu kwingine ameweka pazia.

Na ndio hapo unapoweza kusikia pia kuwa nyumba 10 za familia kadhaa zimechomwa moto kwa kumdhania mmojawao kuwa mchawi kamuua ndugu yao. Ndugu kafa kwa ukimwi-wameweka pazia katika yote kasoro imani za kishirikina. Walipochoma nyumba moja moto ukarukia na za wengine maana biashara ya petroli kwa ajiri ya bodaboda ndio biashara kuu vijijini sikuhizi na wanalaza petroli ndani ya nyumba.

Waambie wauza petroli na kuzijaza ndani ya nyumba zao kuwa moto unaweza kuwaunguza watakuambia-ajali haina kinga Mungu akitaka utakufa anyway.

Mwarabu alipoona bomu limeripuka na halikumuua mwakilishi wa Papa akaona akimbie . Magari ya abiria yamezuiwa kutoka ili yakaguliwe-wakakodi bodaboda. Mwarabu kama ni mwislamu sio mkristu, mtupa bomu mkristu-issue ni kwamba- mtupa bomu na wa kuripua msikiti atakayeweza kuingia ndani hawezi kuwa mkristu si watamshitukia? Lazima awe wa dini husika-Mwislamu. Yule wa bodaboda angemsoselea yule mlengwa awe wa dini nyingine si angetambulika mara maana twajuana vijijini/mitaani. Lakini naye angeumia? Hakutaka kufa, alitaka afaidi mshiko wake hivyo akatupia kwa mbali akiwa na bodaboda. Mtu wa dini husika anaweza kutumika.

Kama ukristu ni tatizo-wanapigana wenyewe kwa wenyewe nchi za kiislamu-somalia, Iraq, afghanistan, Mali, Syria etc na misaada wanayotegemea ni kutoka nchi za kikristu zipeleke volunteers, mahema, chakula. Sasa, ukistu ndio unabomoa Somalia, Syria etc? Jema lipi duniani? Ona wanavyojimaliza pia Congo-laana na balaa gani hili? Tusiwaige hao. Hawa nao waafrica nchi zao mali kibao wanauana badala ya kuzalisha mali na wanategemea misaada toka ulaya na nchi masikini kama wao. Nchi itakuwa na Rais wangapi kila myu anataka awe kiongozi? tuepuka haya.

Jee, anayeua bin adam asiyekosa kwa makusudi-ataingia peponi kweli? Ujingan na ni Imani ya Kijinga.

Akili zetu tunapohamasisha na kusema-tutahakikisha nchi haitawaliki---je, leo hii kabomu tu tunaumana na vifo vya wachache. Kutotawalika maana yake si mauaji ya wengi? Tunalielewa hili?

Unapomfanya jirani yako ndiye adui yako lakini mna nguvu sawa na resources zimewazunguka wewe umebweteka tukueleweje? Lakini yeye akilima wewe wakwanza kuchuma mazao shambani kwake-Je, wewe malalamiko yako yatakuwa na mshiko/uzito. Kwa nini usijitahidi kama yeye. Hapa ninazungumzia umasikini unaolalamikiwa na kuwa sababu ya chuki. Mabonde yaliojaa aje mchina akufanyishe kazi ndio ulime?  fika hadi Kilombero soko la wiki kuna mitumba toka ulaya kibao na apples toka S.Africa; maembo toka Sudan/Mombasa, vichubua uso kutoka China. Hivi vimeletwa na wafanyabiashara wa huko kuvitoa Dar na mbali kwingineko. Ila lalamiko kuu-mchele wa Kilombero hauna Soko? wanawezake kukodi malori, kupakia vichubua uso na maembe, maroba ya mitumba toka mbali, wasiweze kujiunga kwa umoja kukodi lori na kupakia mchele kuuza dar na kwingineko ndani ya TZ ambako bei ni 2,000/= hadi 2,500/=??? Kuna akili na hoja za sababu hapa? Njaa hii isiyotupa mantiki ya kujituma kwa kuzalisha mali na kuuza kifaida bali kuhanja kwa wenzetu kununua ili kuja kuuza viharibu figo (Chemicals za uso na mwili)  ndio vya maana tatizo.

Wakristu ni wavumilivu wa muda mrefu sana, mimi ninakua  mkubwa toka s.y. msingi ninashuhudia makanisa yetu yakifanyiwa vituko ndani siku za misa za sikukuu; sanamu za kikristo zikitolewa mapangoni na kunyewa kinyesi, kukojolewa na wenzetu wa dini ingine mpaka sasa masanamu hayo yamejengewa  milango ya chuma kuzuia matendo hayo. Tuvumiliane lakini wachokozi waache.

Mauaji na mapigano yatakuwa mengi, sio tu ya kidini na kisiasa bali ya matumizi ya ardhi ambayo yameanza muda mrefu. Ardhi haiongezeki. ikiwa tutaachia mtu alime kwa kuhamahama kijiji, wilaya, mkoa kwenda huko akate miti, achome mkaa, alime, auze hela akajenge kwao au kununua mifugo. Mwingine ana ardhi  ndogo analimbikiza mifugo beyond carrying capacity hakuna kuwalazimisha wafuge sustainably kama uwezo wa ardhi ulivyo bali wahame waende wapendako-tutauana wengi sana. Mifano duniani ipo ya matumizi endelevu na waliwezake kuwafanya wapunguze mifugo kupunguza madhara. Tuige hayo. Hata vijiji na ardhi vikipimwa na watu kupewa hati bila ya sustainable farming na livestock keeping-tutauana sana.

Moto utawaka-hasa kama sheria za uhamiaji hatutazingatia na kujifanya wajuaji na watu wa njaa sana au tamaa kwa kuficha wahamiaji-tutaingiza mengi maovu. Ulinzi ni wetu wote. Turudishe mfumo wa ubalozi wa kutoa taarifa za wageni na kukagua lodging usiku na majumba ambayo tunawasiwasi nayo. Turudishe mafunzo ya mgambo vijijini, gwaride mashule ya msingi, sekondari na high school. Vyuo vya kijeshi na kila mmoja amalizae secondary school and above aende JKT kama inavyosemekana sana itarudi hii itatusaidia kujenga uzalendo na utayari kutetea nchi yetu inapovamiwa na sio kufurahia. Itatupa ujasiriamali pia.


--- On Wed, 8/5/13, anna nyanga <luguanna@yahoo.com> wrote:

From: anna nyanga <luguanna@yahoo.com>
Subject: Re: [wanabidii] Re: [Mabadiliko] Neno La Leo: Ya Arusha Na Kamba Inapokatikia...
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Wednesday, 8 May, 2013, 4:46

Watanzania, tufike mahali tuseme nini kifanyike kunusuru taifa letu?

From: Augustine Rukoma <arukoma66@gmail.com>
To: mabadilikotanzania@googlegroups.com
Cc: wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Wednesday, May 8, 2013 6:36 AM
Subject: [wanabidii] Re: [Mabadiliko] Neno La Leo: Ya Arusha Na Kamba Inapokatikia...

Tulio wakabidhi dhamana walewa chakali sasa wamejisalimisha FBI

On 5/7/13, Maggid Mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com> wrote:
> Ndugu zangu,
>
>
>
> HAYA ni moja ya maandiko yangu muhimu katika  kazi yangu ya uandishi na
> uelimishaji jamii.
>
>  Ni kwa kutambua ukweli, kuwa nchi yetu imepatwa na shambulizi la kigaidi.
> Imetokea Arusha, ingeweza kutokea popote pale katika ardhi ya nchi yetu.
> Tunawapa pole wahanga wa tukio hili. Ni msiba wetu sote.  Tuwe sasa na
> mioyo ya ustahamilivu.  Tusikimbile kunyosheana vidole. Tuwaache tuliowapa
> dhamana ya kuchunguza waifanye kazi yao. Wajibu wetu wa kizalendo ni kutoa
> ushirikiano.
>
>
>
> Naam, kama nchi, tunapitia sasa kwenye kipindi cha majaribu makubwa. Huu ni
> wakati wa kuizunguka bendera yetu ya taifa. Ni wakati wa kuonyesha umoja,
> uzalendo  na mshikamano wetu kama taifa. Umoja, uzalendo  na mshikamano
> wetu ni silaha muhimu na kubwa kabisa Watanzania tumeendelea kuimiliki
> tangu enzi na enzi. Ndio silaha tunayoendelea kuimiliki hadi sasa. Tuna
> lazima ya kupambana hadi risasi ya mwisho kuhakikisha adui hatupokonyi
> silaha hii.
>
>
>
> Ndugu zangu,
>
>
>
> Hii ni Nchi Yetu. Ni nchi yetu sote, Watanzania wa imani zote. Tutambue
> sasa, kuwa kwenye safari tunayokwenda kama taifa, mbele yetu kuna  mawimbi
> makubwa. Kwa pamoja tutavuka, kwa kugawanyika tutazama.
>
> Wahenga wetu walisema; kamba hukatikia pabovu. Watanzania wa imani tofauti
> tuna historia ya kuchanganyika na kuishi kwa amani na upendo. Hatuna hulka
> ya kubaguana. Tukianza sasa dhambi ya kubaguana, basi, itaendelea
> kututafuna.
>
> Na siku zote, uzoefu ni mwalimu mzuri . Mathalan, uzoefu unatufundisha,
> kuwa kuwasha moto ni jambo jepesi sana, lakini, kuuzima moto,  ni kazi
> ngumu sana.
>
> Ona, moto ulioanza kwenye nyumba moja ya nyasi kijijini, waweza kusambaa
> haraka na hata kuteketeza kijiji kizima. Na tangu utotoni tumetahadharishwa
> hatari ya kucheza na moto.
>
> Naam, binadamu usicheze na moto, labda iwe kwenye mazingaombwe.
>
> Na ningependa hapa  tuyakumbuke maneno ya busara na hekima nyingi kutoka
> kwa Bi. Joy Mukanyange ( Pichani). Huyu alikuwa Balozi wa zamani wa Rwanda
> nchini Tanzania. Mama huyu aliyatamka maneno haya miaka 13 iliyopita,
> takribani miezi sita kabla ya kifo cha Baba wa Taifa. Bi. Joy Mukanyange
> alikiona kile ambacho Watanzania hatukukiona. Ni kama vile alikuwa mtabiri,
> maana, alichokisema mama yule leo ndio tunaanza kukiona. Siku ile ya Aprili
> 6, 1999, katika iliyokuwa Kilimanjaro Hotel, Bi Joy Mukanyanga aliyatamka
> haya;
>
>  " Naogopa, kwani nimeanza kuona dalili zinazojengeka za mgawanyiko wa
> kidini nchini Tanzania na eneo lote la Maziwa Makuu, hali ambayo inaweza
> kusababisha maauji ya halaiki kama yale yaliyotokea nchini mwetu mwaka
> 1994." Alisema Balozi yule wa Rwanda kabla ya kuendelea kutoa ufafanuzi wa
> historia ya Rwanda na matukio yaliyosababisha mauaji yale ya Wanyarwanda ya
> wao kwa wao. Ndio, Bi Joy Mukanyange alikiona kile ambacho Watanzania
> hatukukiona.
>
>
>
> Na tutafanya makosa makubwa, kama hata sasa, tutajifanya kuwa hatukioni
> kile ambacho Balozi Joy Mukanyange alikiona . Watanzania tukubali sasa kuwa
> tumepatwa na bahati mbaya sana ya baadhi ya Watanzania wenzetu kuanza
> kupandikiza mbegu za chuki miongoni mwetu. Kuna wanaotaka tuanze kubaguana
> kwa misingi ya kidini.
>
>  Hili ni jambo la hatari sana. Ni hulka ya mwanadamu, anapokuwa matatizoni
> kumtafuta kondoo wa kafara. Mtu mwingine wa kummyooshea kidole kwa matatizo
> yake. Hali duni ya uchumi wa nchi, hali duni za maisha na umasikini wa watu
> wetu isiwe chachu ya kuanzisha vurugu za kijamii.
>
> Maana, taratibu tumeanza kuizoea misamiati ya sisi na wao. Mathalan, sisi
> Wakristo na wao Waislamu. Sisi Wachagga na wao Wazaramo. Tunasahau, kuwa
> katika nchi yetu hii hakuna Sisi na Wao, kuna SISI tu.Tutakapokumbwa na
> maafa ya kitaifa watakaoathirika ni SISI, hakutakuwapo na WAO.
>
> Hatari kubwa ninayoiona ni tatizo la wengi wetu kuwa na ufahamu mdogo juu
> ya dunia tunayoishi sasa, kibaya zaidi, ufahamu mdogo wa historia yetu.
> Hivyo basi, kupelekea hali ya kutojitambua kama taifa.
>
> Ndio, uelewa wa historia ya jamii husika ni jambo muhimu sana. Kiumbe
> huwezi kuelewa ya leo, kesho na kesho kutwa kama huelewi ya jana. Kuielewa
> historia yako ni kuelewa ulipo na unakokwenda. Historia ni kama maji ya
> mto, yakipita hayarudi. Historia ni wakati, ni muda. Kihistoria jana ni
> sawa na zamani.
>
> Karne nyingi zilizopita wahenga wetu walitafsiri muda kama mkusanyiko wa
> matukio ya zamani na sasa. Waliamini kuwa yaliyotokea zamani na yanayotokea
> sasa ndiyo yenye kusaidia kubashiri yatakayotea kesho, yataamua mustakabali
> wetu.
>
>  Dalili tunazoziona sasa za kupandikiza mbegu za chuki kwa misingi ya udini
> si dalili njema. Haya yatatupelekea kwenye maafa. Tuliopata bahati ya
> kutumia kalamu zetu hatuna budi kuliweka hili hadharani. Ni wajibu wetu wa
> kizalendo.
>
> Narudia, Hii ni Nchi Yetu. Katika ulimwengu tunamoishi kuna mamilioni ya
> watu ambao hawana nchi. Wahenga wetu walishiriki katika kuijenga nchi hii,
> wametutarajia sisi tuendelee kuijenga na kuilinda heshima na hadhi ya nchi
> yetu. Mengine yanayofanyika sasa sio tu yanaitia doa nchi yetu, bali,
> yanaiaibisha nchi yetu.
>
>  Ndugu zangu,
>
> Hatuna haja ya kubaguana kwa misingi ya dini, ukabila na rangi. Sisi wote
> ni Watanzania. Tuna historia ya kujivunia. Ni historia yetu wenyewe.
> Kinyume na baadhi yetu wanavyofikiri au wanavyotutaka tufikiri, historia
> yetu haikuanzia enzi za Mwarabu , Mjerumani au Mwingereza. Historia yetu
> haikuanzia enzi za TANU wala Afro Shiraz.
>
>  Na dini hizi za kimapokeo zinazotufanya sasa tufarakane zimekuja na
> kuzikuta dini zetu za asili, na bado tunazo. Na hakika, Afrika hatugombanii
> matambiko. Afrika kila ukoo una tambiko lake, hivyo basi, dini yake. Kamwe
> hutasikia Waafrika wanagombania matambiko. Hutasikia Waafrika wakigombana
> kwa tofauti za matambiko yao.
>
>
>
> Na sisi ni Waafrika. Hii leo mahala ambapo unaweza kuwagawa Watanzania na
> hata kufanikiwa kuwafanya wachinjane ni kwenye kwenye tofauti zao za imani
> hizi za kimapokeo; Uislamu na Ukristo.
>
> Naam; kamba hukatikia pabovu. Tusikubali dini iwe ndiyo penye ubovu kwenye
> kamba inayotuunganisha Watanzania.  Nahitimisha.
>
> Maggid Mjengwa,
>
> Msamvu, Morogoro.
>
> 0754 678 252, http://mjengwablog.co.tz/
>
> --
> Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
> Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda;
> mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
> Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
>
> TEMBELEA Facebook yetu:
http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
>
> For more options, visit this group at:
> http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
>
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Mabadiliko Forums" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>
>
>

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.



--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 


0 comments:

Post a Comment