Unayosema ni kweli Deo, hii itakuja kutokea nami nilichangia kusema-inapangwa na kisha unadaiwa hela na ukitoa baada ya muda wanakufuata kuomba tena ili picha isitolewe. Mpaka unaona bora uhame mji na unaathirika kisaikolojia. Hii ya Padri huenda nayo imepangwa maana katika baadhi ya maeneo na hasa vijijini watu wamewageuza watu wa Mungu kama sehemu ya kipato wakiangalia fedha za sadaka wanazokusanya. Hivyo kila mtu mwenye njaa anamlenga padri au Mkatekista au Mchunganji. Mapadri wenye huruma ya kusaidia masikini ndio wanalengwa na kuingizwa mtegoni. Wanawake wanaujanja mwingi. Ukiongea na madaktari watakueleza matatizo wanayopata kwa hao kujifanya wanaumwa kumbe haumwi na anaeleza anaumwa sehemu za siri ili apimwe huko na dokta akianza kumpima anaanza vituko. wapo madaktari wachache wenye ushirikeri na ujasiri wa kumtimua mkuku kumtoa nje. Desturi hasa ya mwanaume wa kiafrika hataki kushindwa. Ndio maana utakuta hata daktari anaweza akawa HIV positive sio kutokana na uzembe wa kutokutumia protective gear wakati wa kazi bali unprotected sex. Wanawake akija mwalimu mpya, kiongozi mpya kahamishiwa kijijini au ofisini-wanamlenga. Wapo maalum wenye kazi hiyo. Kuwalenga hata viongozi wa wilaya, Mkoa, Wizara, wabunge. Nilimuona mkuu wa Mkoa mmojawapo akiwa jirani yangu Mkoa wa Mara miaka hiyo aliwaambia Police wale walinzi nje ya nyumba yake kufukuza wanawake wowote walipao njia ya mkato pale au kuja home kumuona wasubiri ofisini unless amewaambia kuna mtu wa jina fulani na mara nyingi hamwambii mtu amfuate home bali ofisini. Aliwalaza baadhi ndani kwa kufika kwake bila kuitwa. Wakakoma kujitembezatembeza. Wakamsingizia mengi. Wapo akina mama ambao specialization yao ya mabwana ni viongozi. Kukiwa na miradi mipya kama machimbo, ujenzi wa barabara, kiwanda, bwawa la maji-tayari changu doa hujazana huko kutoka hata nchi jirani. wake za watu jirani na mradi huvunda ndoa hasa wale walio katika polygamy hutumia nafasi hiyo kutafuta wao binafsi. Ndio madhara ya miradi huja kuonekana baada ya miaka kadhaa ya mradi kuisha HIV/AIDS, kuonekana kubwa vijiji vya miradi. Bunge likianza-vyangu doa hukimbilia huko. Sex tourism-msimu wa watalii nao wapo wanaowawinda watalii. Haya hufanyika kwa makusudi. Wapo vijana-kazi yao kuwinda akina mama wenye majina na hela kisha kujitangaza au mitandaoni. Desturi za sasa watu kumuwinda mtu mashuhuri au msanii mtajwa msifika. Kawa na huyu leo kesho yule. wanajua madhara ila inatafutwa Sifa tu licha ya matatizo mengine. Unajiuliza mtu ukiona picha magazetini-jinsi mtu alivyotolewa utupu gazetini mbona hashitaki? kama Global Publisher inawaonea, kuna watu wanapiga picha kuziuza gazetini (tuache hizi za fumanizi); daily ni Wema, Diamond picha za hovyo, barua zao za siri; picha za mtu zimeibwa kwenye laptop aliyopelekewa fundi kuitengeneza akakopi na kutoa gazetini-kwa nini hao watu wasishitaki wakapata mamilioni? Huyo aliyeitoa picha ya siri toka simu, kuwavizia au toka laptop si atajulikana na kutoza fedha nyingi na pia gazeti? Hii ikiwatia hasara-wataacha mambo ya kipuuzi. Jee, wananchi wanajua sheria za media na taarifa za uongo au kuviziwa kisiri ukatolewa picha za utupu na kumfedhehesha mtu ktk chombo cha habari hata kama kakosea usimtoe uchi? Jee pia ikijulikana kuwa ile ya Padri ilisukwa kumrubuni-sheria gani itatumika? Kutokujua haya masuala ya sheria ndi tunaona watu wanaachia yanakua, na kuna mtandao wa Fichua Maovu ambao watu wanaweza kuwa wanautumia vibaya, kukuita mahala mtu fulani wamtakao yupo, kuwapiga picha ya pamoja mmekaa meza moha wewe huelewi nia kisha inatoka gazetini. Fujo za kisiasa sasa zinaonekana kuhamia katika jamii kwa media kuunda mtandao sio tu kusaidia kufichua maovu (ambayo si vibaya), bali kuunda kuonyesha mfumo wa maovu wa kupanga/kupika. Kama ni kufichua maovu waende mtaa hadi mtaa pia kufichua brothels ambazo zipo zinauza watoto, changudoa watu wazina na mashoga na wasaidie wanaoathirika kutolewa ktk media kiuonevu kupata haki zao pia. Mwisho-mbona baadhi ya magazeti yanayotangaza utovu wa maadili-katika gazeti lao na matangazo madogo madogo wanatangaza masuala ya Kinyume na maadili au kushabikia ushirikina? Mfano-kumtoa gazetini hata katika TV Mganga wa Diamond anavyoongea ushirikina alivyomfanyia Diamond.Au kuafiki kusema Diamond akichukua nyota ya Bibi Kidude akiwa maiti pembeni.Aibu gani hii! Ukweli gani upo hapa ni kama mganga katoa hongo kumfedhehesha mtu ktk mambo binafsi na anapewa nafasi kama Rais au Kiongozi kusema mambo ya uchawi kushamirisha Imani potevu. Kama wqanaipenda Jamii kutaka kufichua maovu-Baadhi ya Magazeti nchini yanatangaza uganga na ushirikina-huu ni uovu. Mfano Tangazo : Mganga kutoka Nigeria Kiboko ya Wachawi Atua DSM-cheo kazini, pete na mkufu wa bahati, Akili Darasani, na mengine mengi, pili anatibu kwa njia ya simu na mafanikio baada ya siku 3; ......ni Dawa ya mvuto wa mapenzi, humvuta mume, mke, mchumba au yoyote yule umtakae baada ya masaa 3 tu. Mvuto wa biashara, kazini na umfanye umtakae akutafute mwenyewe na hata kuacha tena. Piga simu namba....utaletewa data hizi (bila ya shaka kupelekewa nyumbani). Jee, kama dawa hiyo mama kaiweka kumuwekea Padri au Mume wa mtu au kijana kaivaa hivyo kumchuma mke wa mtu-hayo ndio maadili ambayo Fichua Maovu au Global Publishers inayotajwa hapa inayataka? Baraza la Utamaduni Taifa na Chama cha Waganga wa Tabibu Mbadala, Chama cha Waandishi wa Habari waangalie masuala haya ya maadili, picha gazetini na matangazo ya biashara. watu wa Media wasiangalie Kipato tu na kuuza magazeti bali pia MAADILI.. --- On Thu, 2/5/13, Deo Kibambizi <kibambizi@gmail.com> wrote:
|
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment