--
Ezekiel-Hirizi ya Jini Chuma Ulete nimeisoma ktk tangazo la uganga gazetini. Mimi siijui ila nasikia tu watu wanataja masuala ya chuma ulete. Nimesoma pia magazetini kama nilivyonukuu katika kuchangia kwangu. Ila, fungua magazeti ya Kiswahili kwenye matangazo madogo madogo utaona hayo matangazo.
Angalia gazeti mojawapo kama NIPASHE ukurasa wa kumi 18, matangazo madogo madogo. Fungua KIU na mengineyo ambayo yana matangazo ya Waganga na ya biashara angalia usome, utaona mengio ambayo sikuyataja ktk kuchangia kwangu.
Naona ilitokea mtu mmojawapo nchini alionyeshwa ktk TV na magazeti alikutwa na fuvu la kichwa cha mtu ktk box na mabox mengine wazi mengi kiasi alielekezwa ayaweke hivyo hela zitajaa kwa nguvu hizo za giza. Sijui zitatoka kwa wengine majini yatakuja kuzileta. Wewe unafanya biashara yeye ana yake lakini anavuna yako. Huenda ni hivi. Mimi husoma haya matangazo ya uganga magazetini na kujiuliza-Mganga toka Nigeria-ana kibali huyu kuja kuweka bango TZ barabarani na pia namsoma humu gazetini? kuna rationale gani kusema mfano elimu inashuka TZ, wanafunzi wamefeli asilimia 90, Waziri wa elimu ajihuzuru. Kisha tunatangaza-Dawa ya akili darasani na kupasi mtihani; dawa ya biashara na kufanikiwa (no skill training and capacity building); hela za majini na kufanikiwa machimboni (no need of modern machinery and mineral processing equipments, training mining skills); kumpata umtakae na akaja masaa 2 baada ya kutumia dawa na akakutimizia yote utakayo na asiondoke tena au akutafute mwenyewe na kukupa utakacho. Tunatibu kwa njia ya simu pia na namba ya simu inawekwa. Vyama husika vya kukabili haya na GVT ipo wapi. Tunalaumu GVT kupitia media lakini kuwaje media itangaze kinyume na science na maadili? Ni jaa kali bila mitazamo ya maadili au ni makusudi au ni nini tatizo na written media? Mganga anatolewa ktk radio na TV kujisifu uwezo wa kuroga na kumkomoa mteja alijemkiuka na kumuhama. WHY media ishabikie haya na tuyatazame tukae kimya. Lawama daima ni kwa serikali tu. Jee tunaona vibanzi vyetu machoni pia. Haya matangazo ya kuganga njaa regardless ya yalivyo ni sawa? Fichua maovu ambayo inafanya watu wasio waadilifu kupanga mipango wamnase mtu kimakusudi aaibike imetolewa maoni humu kuwa itahatarisha uongo utapangwa uwe ukweli. Tuyaangalie kisha tujirekebishe inapobidi.Tuipende jamii na nchi yetu, tusiyumbishe jamii kwa elimu inayopingana na masuala ambayo ni kinyume na dini za kumcha Mungu.
--- On Sat, 4/5/13, ezekiel kunyaranyara <ekunyaranyara@yahoo.co.uk> wrote:
From: ezekiel kunyaranyara <ekunyaranyara@yahoo.co.uk> Subject: Re: [wanabidii] Re: AIBUUU.... PADRI WA KANISA KATOLIKI HUKO MOSHI AFUMANIWA LIVE NA MKE WA MTU AKIWA UCHI WA MNYAMA To: "wanabidii@googlegroups com" <wanabidii@googlegroups.com>, "khildegarda@yahoo co. uk" <khildegarda@yahoo.co.uk> Date: Saturday, 4 May, 2013, 14:14
Hilda U esomeka dada, lakini hebu nisaidie sijaelewa pale uliposema 'hirizi ya jini la chuma ulets' unaweza kunifafanul7a hapa hiki ni nini, naamini utafafanua kwa kuwa najua unajua mambo mengi... Sent from Yahoo! Mail on Android | From: Hildegarda Kiwasila <khildegarda@yahoo.co.uk>; To: <wanabidii@googlegroups.com>; Subject: Re: [wanabidii] Re: AIBUUU.... PADRI WA KANISA KATOLIKI HUKO MOSHI AFUMANIWA LIVE NA MKE WA MTU AKIWA UCHI WA MNYAMA Sent: Fri, May 3, 2013 7:09:22 PM Matanda-Tunamsifu sana mmiliki wa GP. Anafanya na amefanya kazi kubwa sana nchini na ni mfano wa kuigwa. Na ndiye aliyeanza kutoa vitabu vyenye simulizi halizi hata zile za ushirikina na wanga wanaofanya mpaka wachungaji kudanganya waumini. Historia halisi za maisha fulani alizoanzisha kuandikwa magazetini-zinatufundisha sana. Ila, tunaomba vijana wake na yeye waangalie haya yanayosemwa humu.
Sio siku zote baba ataingia jikoni kuangalia usafi. Unaweza ukaletewa karatasi kusaini ukahakikishiwa kila kitu muhimu kimeangaliwa kumbe -kanyaboya. Hata cocaine inaweza ikafishwa ndani ya magunia ya unga wa dona ukaja kukamatwa mwenye lori maana hujui kama ndani ya gunia/viroba vya dona kuna viroba vidogo ya cocaine au vipande vidogo vya meno ya tembo. Unahitaji wasaidizi waaminifu wa washiriki waaminifu pia ama sivyo utaingia matatani daima.
Pia, hatuongelei mtu binafsi lakini twaongelea magazeti yote yanayokiuka maadili na hata TVna radio za kuhoji waganga wa kienyeji wanaoonyesha ushirikina wa kuroga watu ni suala zuri na kujitangaza. Twaomba yasiendelee wahusika wayakabili. Unatoa siri za uganga aliofanya mtu (mfano-Diamond) - hatuelewi kama ni kweli au ni chuki baada ya kukuacha na wewe kukosa hela zake. Kama ulimganga na wewe mganga au mchawi hasa, kwa nini uingie ktk media usimlipizie kisasi kimya kimya akajua nguvu yako mpaka umtangaze ktk media kuwa atakujua wewe nani? Ni sawa na Daktari (medical doctor) kumpima na kumtibu mgonjwa mambo ya siri ambapo ni ethical issue asiseme lakini akigombana naye au akilewa pombe anasema siri za wagonjwa! Au mkunga wa jadi, ngariba atoe siri za maumbile ya watu kutokana na kazi yake. Hii si vema.
Tunaomba haki itendeke mtu anapokosa hata kama amefumaniwa; kama adhabu ni wote wamekosea; magazeti yasitangaze uganga wa kienyeji ulio kinyume cha maadili tumeonyesha mifano hapa. Gazeti linaonyesha story yote ya kuvizia na kupanga ili huyo mtu apatikane. Day one alishitukia mpango, day 2 mpango ukafanikiwa (wameshiriki kuipanga-wanajisahau). Mume anasema ukitaka tuishi budi tufanye tumnase nikufumanie (mpango).
Picha ya Diamond akisali karibu na maiti ila gazeti linasema alikuwa anachukua nyota ya bahati na kusafisha nyota yake (haya hayafai kimaadili ni kukuza imani potofu za kishirikina. Gazeti na waandishi wake waache haya). Mtu anapotolewa utupu gazetini na watu wanashuhudia au wanapigana uchi gazeti linaziba eneo nyeti kusaidia-hao waliokuwa wanapigana uchi hadharani wakamatwe waadhibiwe. Utaona watoto ndio wamejaa kushuhudia utupu na ngumi hizo.
Wote tujali maadili ya taifa. Magazeti yanahitaji hela na ndio tunajua shida na nia ya kuganga njaa. Maana kuna hata matangazo yaliyo kinyume cha maadili ili kugangha njaa. Tunaendelea kutaja na yanajijua- Dawa ya kukuza hips na makalio pia nonino iwe kubwa na urudie tendo zaidi ya mara 7 kwa siku; dawa ya kuwa na akili darasani na kupasi mtihani; kupata ajira; pesa za majini na utajiri wa dangu kwa wachimba madini; hiziri ya jini chuma ulete, utajiri wa biashara kwa yeyote tena wa haraka usio masharti. Dawa ya kuzima kesi (hata ya wizi na meno ya tembo na mauaji?). Haki ipo wapi? Utaifa upo wapi? Maadili hayakiukwi hapa? Kisha daima lawama-serikali ndio inanyima maendeleo! Kwa kutaka kupasi darasani bila ya kusoma bali kula dawa hiyo? Tunaisema serikali lakini hatujisemi sisi media tunavyokuza imani potofu na kuonyesha upungufu wa maadili pia pamoja na kuelimisha jamii katika mazuri. Utovu wa maadili na kukuza imani potofu ndio maana mauaji ya albino, kuwakata viungo, kuchomeana nyumba na mtu kuzikwa akiwa mzima kwa kisingizio cha uchawi yanakua. Nyumba 10-20 kuchomwa kwa siku ni Imani hizi. Tunaomba Guardian, Global Publishers, Kiu investments na wengineo wayaangalie haya matangazo kwa umma. wanaharakati tunawaomba-sio Loliondo, na Ulimboka tu na haya pia yanatuumiza kitaifa.
--- On Fri, 3/5/13, denis Matanda <denis.matanda@gmail.com> wrote:
From: denis Matanda <denis.matanda@gmail.com> Subject: Re: [wanabidii] Re: AIBUUU.... PADRI WA KANISA KATOLIKI HUKO MOSHI AFUMANIWA LIVE NA MKE WA MTU AKIWA UCHI WA MNYAMA To: "wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com> Date: Friday, 3 May, 2013, 16:01
Mmiliki wa GP ni hazina kwenye chama chetu na ni mmojawapo wa watu wanaoonekana kuwa ni mfano wa kuigwa kati ya "vijana" wa nchi hii. Ksema serikali imchukulie hatua ni sawa na kutegemea kipenzi cha Wengi "Mchumba" eti achukuliwe hatua kwa utovu wa nidhamu.......................... -- Send Emails to wanabidii@googlegroups.com Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines. --- You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group. To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com. For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
| -- Send Emails to wanabidii@googlegroups.com Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines. --- You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group. To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com. For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out. |
|
|
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment