Media haipo immune na sheria. Tusiige ulaya-tutunze maadili yetu. Tuache kuviziana. Wanaume wakae chonjo na wanawake kwa sasa. Wanawake wakae chonjo na wanaume pia. Wote sio wema. Tunashuhudia pia wale ambao ni HIV positive kuwarubuni watoto wa kike wa wenzao ili kuwaambukiza kwa makusudi kumkomesha mzazi ambaye yeye ana tofauti nae. Ukitofautiana naye au ukiwa mpinzani kwa namna moja au nyingine na anajua una familia-anamsaka mkeo au mwanao kwa pesa nyingi hata $ ili amuambukize. Kama ni ke akuletee nyumbani. Hivyo, wasichana wanaweza kutumwa akusake na kujipendekeza kwako akisha kukupata anakwenda kulipwa posho ya mihela. Keshakuletea matatizo hata kama ni Kaswende. Kama una girlfriend weak-anamfuatia ambaye ana afya ya matatizo. Anamlipa kijana ampatie uambukizo akuletee wewe unayejidai sana na ana tofauti nawe. Atampa mihela mingi na magari kumbadilishia mradi mama amuone kijana/mwanaume huyo ana hela. Siku unamfuata hapo kumsaka nyumba hiyo anapokupeleka unaambiwa huyo hujaga tu hakai hapo-hawamjui. Hii ndio inayoendelea kwa sasa. Akisha hakikisha amempata-anaacha mahusiano haendelei na hapatikani kwa simu wala mtaa huo na ofisi anayokupekeka kukuambia yupo wala si ofisi yake. Siku hiyo ndio utaambiwa ukweli hapo ofisi hiyo kuwa ni kanyaboya hapo hajaajiriwa hujileta tu kwa aliosoma nao au walioishi mtaa mmoja. Wanaotengana muda mrefu hasa wababa hufanya hivyo pia kumrejea mke kwa nia hiyo. Kisha wazee huingilia na kusuluhisha kuomba ndoa ya kikristu irejee wasitengane tena. Baada ya mofa inakuja kujulikana kuwa mrejeo umeleta tatizo. Mawizarani na taasisi-wasichana kutembelea ofisi fulani daima ambayo ina wageni-wazungu kwenye mradi fulani ushoga unawika ili mradi ajisogeze labda atamuwinda na kumpata mmoja. Hakai ofisini kwake daima ni kutembelea hapo tu. Na sasa nyongeza ya wasichana wanaofagia au kufanya usafi maofisini-taasisi walioletwa na makampuni binafsi chini ya mikataba ya kazi-ni kuhurumia tu ndoa za watu na kuwahurumia wao wasichana. Mishahara yao midogo wanatafuta misaada ya nauli daily kwa kuitikia miito mingi maofisini kwenye milango iliyofungwa na viyoyozi zikiunguruma. Hawa hawaelezi background ya mtu ila wanaangalia kipato tu msaada wa nauli daily. Bado haya ya mume na mke kuwa ndani ya ndoa lakini wana mihanjo na waume wengine kuwa na mahusiano na mashoga na hata kumpangia chumba au nyumba. Ni miezi michache tu shoga kafumaniwa na mke wa mtu Temeke lakini ni huyo shoga kijana tu aliyepigwa na yule mama na mashabiki wake lakini mume hakupigwa au hata kuvuliwa nguo wala kutiwa bisibisi sehemu nyeti. Mama akilinda penzi na ndoa. Kijana akaambiwa na mwenye nyumba kuwa-ahame nyumba (japokuwa akipokea kodi ya baba huyo) na vitu vya kijana vikatupiwa nje. Hapo alipangiwa na huyo baba mume wa mtu. Watu (wapangaji) wakamtonya mke baada ya kuona wanazidiwa masalo hapo ndani baba aikileta kwa kijana. Mama nae alionyeshwa maringo yake bure mume anashoga nyumba fulani mitaa hiyo anakoishi. Kijana hafiki hata miaka 20 akaambiwa na mke kuwa yeye huyo kijana ndio anamuharibu mume na kumfundisha uovu-jee hii inapanda kichwani. katoto kadogo katamfundishaje uovu mtu mzima? Hapo akiokoa NDOA ambapo ni miaka au miezi mingi akichangia na kashoga anajibaraguza. Tabia hizi za kumfumania mwenzako ukamtuhumu mmoja tu ni unduma kuwili na kama ni adhabu wapewe wote na iwe katika vyombo vya kisheria. Akitembezwa mtu uchi au kutiwa bisibisi umma usaidie akamatwe hapo apelekwe polisi. Akiwepo police anashuhudia, kisha awaambie wayamalize nyumbani-naye akamatwe maana si mtii wa sheria ni mpotofu. Na hata kesi za vichanga kubakwa wanaambiwa mkayamalize nje kifamilia na kiujirani. Mbaya sana. Kuna haja ya kuwa na mikakati ya kufufua maadili, upendo kwa utamaduni wetu na tucheze sana hata ngoma za jadi ktk sherehe za kitaifa kama afanyavyo mh Jakaya kupenda utamaduni. Pia tufundishwe sheria ambazo kwa sasa jamii inahitaji kuzijua ili kuweka amani na kulinda maadili. Hata huu mchezo kwamba kukiwa na maandamano au matatizo ya malipo basi wananchi wavamie nyumba za watumishi fulani wa umma, au viongozi au kuvunja biashara za watu na magari kote wapitako uishe. Unayemvunjia mali zake siye aliyekukosea. Au unachoma mahakama na kituo cha polisi-jamii yako ina kesi mbali mbali hapo unaathiri vizibiti, unatesa wenzako. Nawe ukipata shida utahitaji polisi au zahanati na mahakama au la. Unamatatizo shuleni-mkavunja vioo vya shule, kuchoma nyumba za walimu, madarasa. Mtihani wa form 4 waja-matasoma na kufanya mitihani wapi? Budi tuwe na akili kukichwa tusiwe vuvuzela kwa visingizio-'watu wenye hasira kali'. Mbona akifungwa familia yake itateseka pia!! Hasira itakwisha? kuongezeka? au kuchanganyikiwa huko jela? Ni mzigo pia wa society kujaza wafungwa na kuwalisha. Wote tujirekebishe-pamoja na Media kukuza mambo na MAPICHA ya HOVYO na matangazo ya kukuza USHIRIKINA. Tujilinde na kulinda mahusiano na ndoa zetu. Weekend Njema. --- On Fri, 3/5/13, Deo Kibambizi <kibambizi@gmail.com> wrote:
|
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment