Matanda-Tunamsifu sana mmiliki wa GP. Anafanya na amefanya kazi kubwa sana nchini na ni mfano wa kuigwa. Na ndiye aliyeanza kutoa vitabu vyenye simulizi halizi hata zile za ushirikina na wanga wanaofanya mpaka wachungaji kudanganya waumini. Historia halisi za maisha fulani alizoanzisha kuandikwa magazetini-zinatufundisha sana. Ila, tunaomba vijana wake na yeye waangalie haya yanayosemwa humu. Sio siku zote baba ataingia jikoni kuangalia usafi. Unaweza ukaletewa karatasi kusaini ukahakikishiwa kila kitu muhimu kimeangaliwa kumbe -kanyaboya. Hata cocaine inaweza ikafishwa ndani ya magunia ya unga wa dona ukaja kukamatwa mwenye lori maana hujui kama ndani ya gunia/viroba vya dona kuna viroba vidogo ya cocaine au vipande vidogo vya meno ya tembo. Unahitaji wasaidizi waaminifu wa washiriki waaminifu pia ama sivyo utaingia matatani daima. Pia, hatuongelei mtu binafsi lakini twaongelea magazeti yote yanayokiuka maadili na hata TVna radio za kuhoji waganga wa kienyeji wanaoonyesha ushirikina wa kuroga watu ni suala zuri na kujitangaza. Twaomba yasiendelee wahusika wayakabili. Unatoa siri za uganga aliofanya mtu (mfano-Diamond) - hatuelewi kama ni kweli au ni chuki baada ya kukuacha na wewe kukosa hela zake. Kama ulimganga na wewe mganga au mchawi hasa, kwa nini uingie ktk media usimlipizie kisasi kimya kimya akajua nguvu yako mpaka umtangaze ktk media kuwa atakujua wewe nani? Ni sawa na Daktari (medical doctor) kumpima na kumtibu mgonjwa mambo ya siri ambapo ni ethical issue asiseme lakini akigombana naye au akilewa pombe anasema siri za wagonjwa! Au mkunga wa jadi, ngariba atoe siri za maumbile ya watu kutokana na kazi yake. Hii si vema. Tunaomba haki itendeke mtu anapokosa hata kama amefumaniwa; kama adhabu ni wote wamekosea; magazeti yasitangaze uganga wa kienyeji ulio kinyume cha maadili tumeonyesha mifano hapa. Gazeti linaonyesha story yote ya kuvizia na kupanga ili huyo mtu apatikane. Day one alishitukia mpango, day 2 mpango ukafanikiwa (wameshiriki kuipanga-wanajisahau). Mume anasema ukitaka tuishi budi tufanye tumnase nikufumanie (mpango). Picha ya Diamond akisali karibu na maiti ila gazeti linasema alikuwa anachukua nyota ya bahati na kusafisha nyota yake (haya hayafai kimaadili ni kukuza imani potofu za kishirikina. Gazeti na waandishi wake waache haya). Mtu anapotolewa utupu gazetini na watu wanashuhudia au wanapigana uchi gazeti linaziba eneo nyeti kusaidia-hao waliokuwa wanapigana uchi hadharani wakamatwe waadhibiwe. Utaona watoto ndio wamejaa kushuhudia utupu na ngumi hizo. Wote tujali maadili ya taifa. Magazeti yanahitaji hela na ndio tunajua shida na nia ya kuganga njaa. Maana kuna hata matangazo yaliyo kinyume cha maadili ili kugangha njaa. Tunaendelea kutaja na yanajijua- Dawa ya kukuza hips na makalio pia nonino iwe kubwa na urudie tendo zaidi ya mara 7 kwa siku; dawa ya kuwa na akili darasani na kupasi mtihani; kupata ajira; pesa za majini na utajiri wa dangu kwa wachimba madini; hiziri ya jini chuma ulete, utajiri wa biashara kwa yeyote tena wa haraka usio masharti. Dawa ya kuzima kesi (hata ya wizi na meno ya tembo na mauaji?). Haki ipo wapi? Utaifa upo wapi? Maadili hayakiukwi hapa? Kisha daima lawama-serikali ndio inanyima maendeleo! Kwa kutaka kupasi darasani bila ya kusoma bali kula dawa hiyo? Tunaisema serikali lakini hatujisemi sisi media tunavyokuza imani potofu na kuonyesha upungufu wa maadili pia pamoja na kuelimisha jamii katika mazuri. Utovu wa maadili na kukuza imani potofu ndio maana mauaji ya albino, kuwakata viungo, kuchomeana nyumba na mtu kuzikwa akiwa mzima kwa kisingizio cha uchawi yanakua. Nyumba 10-20 kuchomwa kwa siku ni Imani hizi. Tunaomba Guardian, Global Publishers, Kiu investments na wengineo wayaangalie haya matangazo kwa umma. wanaharakati tunawaomba-sio Loliondo, na Ulimboka tu na haya pia yanatuumiza kitaifa. --- On Fri, 3/5/13, denis Matanda <denis.matanda@gmail.com> wrote:
|
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment