Naomba uilete ile ya ulipobadili jina lako. Naisikia tu.
Date: Sat, 11 May 2013 12:47:12 -0700
From: kicheere@yahoo.com
Subject: Re: [wanabidii] Mh Zitto sijakuelewa
To: wanabidii@googlegroups.com
bandugu na hasa mabwana zito kabwe, mngonge, juma abdala na paul; nadhani tatizo siyo bakwata bali tatizo ni waislamu wenyewe. nadhani kukidhi kiu ya kwa nini nasema tatizo ni waislamu wenyewe soma makala yangu hii ya zamani kidogo niliyoandika kwenye mwanahalisi ikiwa na kichwa cha habari rostam aziz anacheza kama pele. Rostam Aziz anacheza kama Pele Rostam bwana, noooma! Na Nyaronyo Kicheere Rostam Aziz, yule mtuhumiwa wa ufisadi aliyejiuzulu nyadhifa zake zote katika CCM kwa sababu hapendi siasa uchwara, anajua kucheza kama Pele na kupanga mipango na mikakati kama Kanisa katoliki. Nimeanza na msemo huo hapo juu kwa kufahamu kwamba tangu dunia imeumbwa hakujatokea mchezaji wa mpira wa miguu aliyevuma na kufunga magoli mengi kama alivyowahi kufanya Edson Arantes dos Nascimento "PELE". Nimeambiwa na wapenzi na washabiki wa mpira wa miguu au soka (soccer) au kabumbu au gozi au futiboli kama wanavyouita wengi mchezo huo kuwa katika uhai wake, Pele, mchezaji mweusi mzaliwa wa Brazil, alifunga zaidi ya magoli 1500, Na rekodi hiyo haijavunjwa hadi leo. Nimeambiwa pia kuwa, Pele alicheza fainali za kombe la dunia mara tatu katika miaka ya sabini akiwa na wataalamu wenzake wa kusakata gozi au kabumbu akina Garincha,…. Na mtu pekee ninayeweza kumlinganisha na Pele hapa nchini lakini yeye akisakanya kutafuta sabuni ya roho, yaani kitu pesa, ni mbunge wa zamani wa Igunga na mweka hazina wa zamani wa CCM na mmiliki wa makampuni zaidi ya kumi nchini, Rostam Aziz. Rostam Aziz anapotafuta pesa, anapowekeza, anapofuatilia noti, hucheza kama Pele! Akikuacha bega tu, utakuta katengeneza milioni wakati wengine hata ndururu hamjapata. Huyo ndiye Rostam, lakini hayo tisa kumi ni jinsi anavyojua kupanga na kupangua, akiweka mikakati ya kupata noti. Katika hili, taasisi pekee tunayoweza kumlinganisha nayo ni Kanisa Katoliki, lile Kanisa alilowahi kuliandikia Paulo Mtume wa Mungu, akiwahubiria Wagalatia, Wakorintho na Warumi. Hapa sikaribishi ubishi, angalia tu mambo yanavyoliendea vizuri Kanisa Katoliki hapa nchini. Na siku zote si kwa kupendelewa , la hasha, ni kutokana na Kanisa hilo kupanga mipango, mikakati na kutabiri vema mwenendo wa uchumi na utawala wa nchi utakavyokuwa. Hakuna Padiri wala Mchungaji kihiyo. Bila digirii nenda kafuge ngurue, hupati Upadiri. Wewe tazama mambo ya Kanisa Katoliki halafu uamue. Wakati Wapagani wanatambika kwenye mapango na mapori ya Nyamongo, Namanyere, Nakapanya na Nyalikungu, Wakatoliki wanajenga makanisa mijini na kuruhusu wote waje kusali misa na rosari takatifu. Wakati Waislamu wananunua maspika, maikrofoni na kukodi magari ya kubeba wahubiri kuwathibitishia waja wa Mwenyezi Mungu subhana wa taala kuwa Yesu yule Mnazareti siyo Mungu wao Wakatoliki wanajenga Chuo Kikuu na kuruhusu wote waje kupata shahada na stashahada pale. Wakati waungwana wanapiga kampeni nchi nzima wakitaka serikali iwaanzishie mahakama yao peke yao kwa ajili ya kuwatatulia migogoro ya mirathi, wakfu na mambo ya talaka wao Wakatoliki wanajenga Hospitali ya Rufani na kuruhusu yeyote atakaye aende kutibiwa pale. Wakati wengine wanalalamikia serikali kwa kutowajengea barabara wao Wakatoliki wanaomba na kupewa maeneo makubwa ya ardhi mbali na barabara huko maporini kwa ajili ya makanisa yao, mashule yao, seminari zao, vyuo vyao, shule zao za chekechea, msingi na sekondari. Narudia huko maporini! Hebu jiulize kuna barabara kuu inapita Mbagala Spiritual Centre? Kuna barabara kuu inapita Kurasini Episcopal Centre? Jiulize tu kama kuna mgogoro wa eneo la kanisa barabara kuu za Kilwa, Nyerere, Morogoro, Bagamoyo au Kawawa, Mandela na Sam Nujoma jijini Dar es Salaam? Nasema Kanisa Katoliki siyo vikanisa! Hilo ndilo Kanisa Katoliki. Kila mwaka wanakutana mara moja wale maaskofu wakubwa wa kanisa hilo na kupanga mipango, mikakati na kutoa maelekezo kwa mapadiri wao. Na mikutano yao hakuna wandishi wa habari na hayatangazwi maazimio yao. Mtaona tu katika pori fulani wameomba eneo jirani na kijiji, mji au manispaa. Wakilipata eneo hilo wanaanza kujenga kanisa, linafuatiwa na zahanati, inafuatiwa na shule ya watoto wadogo (chekechea), inafuatiwa na shule ya msingi, inafuatiwa na shule ya sekondari ambayo inafuatiwa na chuo cha ufundi. Haujapita muda mnashangaa kijiji, mji au manispaa inakua kuelekea walipo Makatoliki wale kwa sababu wamewekeza katika vitu vinavyotakiwa na jamii. Mnapozinduka kuwa Yesu awe Mungu au asiwe Mungu ni hoja inayowahusu wanaoamini hivyo tayari Makatoliki wamefikisha vyuo vikuu saba. Mtakapogundua kwamba dini na maamrisho yake yapasa kutekelezwa na wale wanaoifuata dini hiyo na kwamba mahakama ya kidini yapasa kuanzishwa na wafuasi wa dini hiyo mtakuta tayari Makatoliki wamejenga hospitali 20 au zaidi zinazotumiwa na serikali kama hospitali za wilaya. Ukiugua unataka utakwenda hutaki utapelekwa na nduguzo ukatibiwe huko. Narudia, mtu pekee nchini anayeweza kucheza kama Pele na kupanga mipango ikapangika na mikakati ikatekelezeka kama Kanisa Katoliki ni mfanyabiashara maarufu Rostam Aziz. Mimi simsifii hivi hivi tu, hebu fuatilia mafanikio yake. Waziri wa sasa wa Nishati na Madini, Mheshimiwa sana, William Ngeleja, aliwahi kuwa mwajiriwa wa Rostam Aziz. Yaani hapo mwanzo, Ngeleja alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Sheria katika Kampuni ya Vodacom ambayo mmojawapo wa wamiliki wake ni Rostam Aziz. Upo? Kabla ya Rostam kuanza kuwekeza kwenye nishati na madini, alimsaidia William Ngeleja, kugombea ubunge wa kwao sengerema na kushinda. Mimi nasema alishawishiwa kugombea na wale waliomhitaji na Ngeleja aliposhinda ubunge akapewa Uwaziri wa Nishati na Madini. Na sasa kampuni ya Richmond/Dowans imeshinda tuzo kwenye mahakama ya kimataifa na inatakiwa kulipwa fidia na Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco), nasikia mabilioni ya shilingi lakini kabla pesa hizo hazijalipwa mkuu wa kitengo cha sheria cha Tanesco aitwaye Subira kaondolewa! Hebu bashiri nani kaletwa kuchukua nafasi ya Subira kama Mkuu wa kitengo cha Sheria cha Tanesco wakati huu ambapo Tanesco inatakiwa kumlipa mmiliki wa Richmond/Dowans ambaye mimi nimedokezwa na wanoko wa mjini kuwa ni Rostam Aziz? Ndiyo umebashiri vizuri. Ni mwanasheria mwingine kutoka Vodacom, ile kampuni ya Rostam Aziz! Kumbe atoke wapi? Kudadeki, Mzaramo kalonga au kasema: kalaga baho na ubozi wako! Nanachokiona hapa ni msomi mtaalamu wa sheria wa Rostam kapelekwa Tanesco ya serikali chini ya mwanasheria mwingine wa Rostam (Ngeleja) kusaidiana kuhakikisha sheria, kanuni na taratibu zinafuatwa kumlipa haraka iwezekanavyo mmiliki wa Richmond/dowans ambaye ni Rostam. Tena mengi hapa sikuyasema, nimeambiwa hata wanasheria walioendesha kesi ya Richmond/dowans walikuwa wapangaji wake Rostam Aziz hapo zamani! Nyie mnaona watu wanashinda tu. Mmeula wa chuya. Ni mipango, mikakati na uwezo wa kuona mbali. Cheza kama Pele na panga mipango kama Kanisa Katoliki. Usichezee shilingi chooni, usimrudishie mpira golikipa mbele ya adui. Wenye kujua wanachukua viwanja visivyo na migogoro mbali kabisa maporini, faida yake itakuja kujulikana miaka 20 baadaye. --- On Sat, 5/11/13, mngonge <mngonge@gmail.com> wrote:
|
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment