Thursday 9 May 2013

Re: [wanabidii] Mbunge anapojibu hoja za mbunge mwenzake waziri afanye nini?

Inashangaza sana Gloria,
Hii inaashiria kuishiwa nguvu kwa CCM. Waziri peke yake hatoshi kujibu hoja za wabunge wa upinzani, hii inanikumbusha wakati wa utoto  ndugu yako akichokozwa na mtu na unajuwa hana nguvu za kupambana nae, basi mnakuja wote kumchangia yule mtu mmoja mwenye nguvu anaempiga ndugu yenu. Nawataka muache tabia hiyo mara moja mbunge aseme matatizo ya jimbo lake yaliyomleta Bungeni. Ndio maana maendeleo yanachelewa nchi nzima, maana muda mwingi wabunge wa CCM mnajibu hoja za wenzenu mnasahau kutoa shida zinazotafuna majimbo yenu. Mfano juzi Tundu Lisu alisema jeshi la polisi linatumika vibaya na wanasiasa, kila aliesimama alitetea sio kweli sio kweli hadi jioni muda wa kikao unaisha. Ni saa ngapi mtatetea majimbo yenu? Acheni kufanya kazi za Mawaziri tafadhali fanyeni kazi zenu kama wabumge.
Swalehe. 
 
2013/5/9 Gloria Mazoko <mazokogloria@yahoo.com>
Swalehe,

Ukistaajabu ya Musa utayaona ya firauni!!!!!!!!!!!!!!!!
Si ndio maana watu siku hizi tumegeuza kipindi cha bunge kama sehemu ya starehe maana ni vituko kwenda mbele. Mi hilo nilikuwa nilishangaa kila siku ila kwa kuwa sijui kanunui za bunge nikahisi wako sahihi. Ila shortly inachekesha sijui nikujishau au ni kunogewa hata sielewi???Maana wabunge wa CCM ni kama wote ni Ma- Rais, , Makamu wa Rais ,Mawaziri, Makatibu wakuu, wakuu wa mikoa, wilaya, wakurugenzi wa mikoa na taasisi mbalimbali.

Utakuta mtu anajibu hoja ya Mbunge mwenzake utafikiri kakaimishwa Uwaziri wa Wizara fulani. Kichekesho kweli kweli!!!!. Sijui ni kuganga njaa au ni kuona kama watakumbukwa wakati mwingine wapewe hizo Wizara hata sielewi. Mi huwa wakati mwingine naona aibu mpaka nainama chini watu wanbaki kucheka. Yaani wangekuwa wanajua wakiwa wanafanya hivyo watazamaji wanvyokuwa wanakasirika wasingedhubutu kufanya hivyo maana huwa wanaporomoshewa maneno mpaka unasema wangeyasikia haya wasingetamani hata na huo ubunge. Sijui hawana watu wa kuwashauri maskini. Utakuta mtu macho yamemtoka badala yakueleza matatizo ya wananchi wake yaliyomleta bungeni na aliyoapa kuyatafutia ufumbuzi ambao hata robo hajafanya anadandia kazi zingine za mawaziri, jamani Tanzania ni zaidi ya tuijuavyo.

Kuna mwingine Juzi alitoa mpya, eti mtu akitaka kufukuza mawaziri agombee u-Rais. Hivi hao mawaziri wengine waliopigiwa debe hapo nyuma wafukuzwe na kweli wakafukuzwa, wao walimkosea nini Mungu? Double standard zitatumaliza.

Anyway ngoja tuendelee tutaona mwisho wake.

Gloria A Mazoko,
Education and Publicity Manager,
Tanzania Federation of Cooperatives Ltd, 9th Floor, Ushirika Building Lumumba Street ,
P. O. Box 2567 Dar es Salaam - Tanzania. Tel: +255 222 2184 084, Fax: +255 222 2184 081,
Mob: +255 754 699 770,
Email: mazokogloria@yahoo.com, ushirika@ushirika.co.tz
web: www.ushirika.coop.

From: isack mchungu <isackmn1965@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Thursday, May 9, 2013 3:43 PM
Subject: Re: [wanabidii] Mbunge anapojibu hoja za mbunge mwenzake waziri afanye nini?

SWALEHE,
 
hiyo ndo ile aliyosema mbunge wa iringa mjini mch. Msigwa kuwa AKILI NDOGO ZIMERUHUSIWA KUTAWALA VICHWA VIKUBWA, mh msigwa hakukosea na ndicho walichonacho wabunge wengi wa CCM, kuna siku nilisema hapa kuwa siku bajeti ya wizara ya maji inapitishwa nilishindwa kumwelewa Mh. christopher ole sendeka , mbunge wa simanjiro CCM,alitangulia kuchangia mbunge wa chadema kuhusu maji aliefuata alikuwa ole sendeka cha kushangaza jamaa badala ya kuzungumzia tatizo la maji lilivyokubwa kule umasaini akaanza kumsaidia waziri maghembe kujibu hoja za mbunge wa chadema, akatumia muda mwingi kujibu hoja ya maji alipokuja kuanza kuongelea suala la tatizo la maji kule kwa wananchi wake tena akaanza kulaumu yaleyale aliyokuwa anatetea! yaani jamani nyie acheni,KWELI VIONGOZI WAMEPATA NCHI. BADALA YA NCHI KUPATA VIONGOZI

2013/5/9 Selemani Swalehe <semkiwas@gmail.com>
Wana mabadiliko ninapotazama Bunge napata tabu sana. Mara nyingi mbunge yeyote yule anapotoa hoja katika kuchangia tunategemea Waziri wa wizara husika ndie atakaejibu hoja za wabunge wote wakati atakaposimama kutoa  majumuisho na kuwasilisha hoja rasmi.Lakini cha ajabu wakati mbunge kutoka kambi ya upinzani anapochangia na  kutoa hoja alizotumwa na wananchi wa jimbo lake, akimaliza kama anaefuatia kuchangia ni mbunge kutoka CCM  badala ya kutoa hoja zake alizotumwa na wananchi wa jimbo lake  anaanza kujibu hoja za mbunge mwenzake alizotoa na kukanusha yale aliyosema mbunge wa upinzani wakati hiyo ni kazi ya waziri na sio kazi ya mbunge.Sasa waziri yeye atafanya kazi gani? Hii imekaaje? ni kutetea chama au ni kuonyesha umahiri wa kuwakandamiza wapinzani ili pengine mbunge huyo aonekane anafaa na hatimae kupata cheo au ni nini? Sijui kama comrades mmeliona hilo.
Suleiman Swalehe
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
0 comments:

Post a Comment