Wednesday 1 May 2013

Re: : [wanabidii] Kigwangallah na tuhuma za ufisadi

Pole kwa yote,yote naamini ni kwa ajili ya siasa.

----------
Sent via Nokia Email

------Original message------
From: Alphonce <alphoncekalula@yahoo.com>
To: "MUX ALUMNI" <muxalumni@googlegroups.com>,"wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Wednesday, May 1, 2013 5:10:53 PM GMT+0000
Subject: Re: [muXalumni:47408] Fwd: [wanabidii] Kigwangallah na tuhuma za ufisadi

Pole sana Mh.Kigwangalah,
Usijali hizo ni punches za kisiasa. Keep doing the good work you are doing ya kuwaletea maendeleo wana jimbo wako na watanzania kwa ujumla.
Misamaha ya kodi imewekwa na serekali kwa nia njema kabisa kusaidia kusukuma uwekezaji hasa kwa watanzania wenzetu wenye nia njema ya kuleta maendeleo kwa nchi yetu na offcourse in long run kutengeneza ajira kwa watanzania.
Kuna wengi wetu hatufahamu mchakato wa hilo na jinsi ya kuwa wajasiriamali na ku access misamaha ya kodi na mikopo ya mabenki ili tuwekeze.Tunadhani wenye fursa hiyo ni wawekezaji toka nje ya nchi peke yao. Tufunguke na kufikiria outside the box.

Waswahili wanasema mti wenye matunda ndio unaopigwa mawe na si ule wenye miba.

We are with you in spirit. Mungu akupe more strength katika kutekeleza majukumu yako.

Regards,

Alphonce.
Alphonce Kalula

-----Original Message-----
From: "Dr. Hamisi A. Kigwangalla" <hkigwangalla@gmail.com>
Sender: muxalumni@googlegroups.com
Date: Wed, 1 May 2013 19:26:16
To: muXalumni<muXalumni@googlegroups.com>; wanabidii<wanabidii@googlegroupscom>
Reply-To: muxalumni@googlegroups.com
Subject: [muXalumni:47408] Fwd: [wanabidii] Kigwangallah na tuhuma za ufisadi

---------- Forwarded message ----------
From: Dr. Hamisi A. Kigwangalla <hkigwangalla@gmail.com>
Date: 2013/5/1
Subject: Re: [wanabidii] Kigwangallah na tuhuma za ufisadi
To: wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>


Mbunge wa Jimbo la Nzega,
Taarifa kwa vyombo vya habari
Bungeni, Dodoma, Mei 1, 2013.

Nawasalimu kwa heshima na taadhima.
Napenda kutumia fursa hii kutoa taarifa kwa wanahabari na umma kwa ujumla
kufuatia habari iliyotoka leo mapema asubuhi kwenye gazeti la Sauti ya watu
Tanzania Daima, toleo Na.3071 na kuzua mjadala mkubwa na mzito kwenye jamii
pamoja na kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na hadhi, heshima na
uadilifu wangu kwenye jamii nikiwa kama kiongozi wa umma. Niwape pole wale
wote walioguswa na kushughulishwa na jambo hili, haswa familia yangu,
ndugu, marafiki na wananchi wa Nzega; ambao siku zote wanaamini sana katika
uadilifu wangu na namna ninavyosimamia misingi ya haki, sheria na uzalendo.
Nimesikitishwa sana na habari hii hususan kwa kuwa ilichapishwa bila
kunipa fursa ya kueleza kwa mapana uhusika wangu. Niwapongeze gazeti la
Nipashe kwa kupuuza uzushi huu mara baada ya kunipigia na kueleza upande
wangu wa hadithi.
Kumekuwa na wimbi kubwa la baadhi ya watu kwenye baadhi ya vyombo vya
habari kuandika habari za uongo kwa maslahi maovu ya kuwachafua wanasiasa
na watu wengine. Watanzania sote tubadilike na tukatae tabia za kutumika
vibaya namna hii, maana ni hatari kwa ustawi wa weledi, na kwa umoja na
mshkamano wa kitaifa. Ukishaandika jambo ambalo litamchafua mwenziyo, hata
kama utamsafisha kiasi gani ni wazi hautokuwa na uhakika kuwa utawafikia
wale wale waliosoma zile za jana za kumchafua – hivyo ni jambo la kawaida
kabisa kuanza kwanza kwa kuwa na uhakika kabisa na habari kabla ya
kuiandika.
Mfano mwaka 2010 tu mara baada ya kuteuliwa nilizushiwa kashfa ya uongo
kabisa inayohusiana na Uraia wangu na gazeti moja maarufu la kila siku na
mengine yakaweka kwenye ukurasa wa mbele kabisa kwamba Kigwangalla ni
Mrundi; hawakusema ni mrundi wa wapi, toka lini ama kivipi, walisema ni
mrundi tu! Basi hata kusema shaka yao inaanzia wapi hawakusema. Kwa kuwa
vyombo vya dola vilinisafisha na kupelekea kushinda mapingamizi yote
yaliyowekwa na washindani wangu kisiasa, niliamua kudharau na kusema
yatapita tu na yatasahaulika.
Pia gazeti lingine likaandika kwamba kampuni ya Kigwangalla ni miongoni mwa
makampuni yaliyowahi kufaidika na 'stimulus package' baada ya mdororo wa
uchumi mwaka 2008. Gazeti hata halikutaja kampuni ya Kigwangalla ni ipi,
inaitwaje, Kigwangalla ana hisa kiasi gani, anaendesha kampuni hiyo ama la,
na kampuni hiyo imepewa sh ngapi kutoka benki kuu, na je imepewa pesa hizo
kwa nyaraka zipi na zenye namba gani? Na je pesa hizo imepewa kihalali ama
imepitia mlango wa nyuma? Kama imezipata pesa hizo kinyume na utaratibu,
basi kuna ushahidi gani! Kwa kuwa yalikuwa mambo ya uongo na uzushi
niliamua kudharau na kuacha kama ilivyo.
Gazeti lingine la kila siku liliwahi tena kuandika 'Kigwangalla atajwa
kufadhili mgomo wa madaktari' na liliweka hadithi hii kwenye ukurasa wake
wa mbele kabisa. Halikusema amefadhili sh ngapi? Amempa nani? Zimeenda
kufanya nini fedha hizo? Kwa kuwa lilikuwa ni jambo la uongo, pia
nilidharau na kuacha lipite. Mwaka jana Novemba pia gazeti lingine
liliandika habari na kuweka picha yangu na ya Ndg. Hussein Bashe, na
katikati yetu picha ya bastola, na kusema 'Kigwangalla na Bashe na vita ya
bastola Nzega', na humo ndani kueleza kuwa Kigwangalla na Bashe
wanyoosheana bastola wakati wakirudisha fomu za kugombea ujumbe wa NEC. Na
kuna mengine mengi: yale ya rushwa ya vitumbua n.k.
Yote haya kwa ujumla wake yalikuwa ni mambo ya uongo na yasiyo na chembe ya
ukweli hata kidogo. Mara zote nimekuwa nikiyadharau na kuongea na wahariri
wa vyombo husika vya habari kwa namna inayoashiria urafiki na weledi wa
kushirikiana na kufanya kazi pamoja na si vinginevyo; ushauri ambao
niliupata mwaka 2009 kutoka kwa moja ya wanasheria wa kampuni yangu (wa
kampuni ya Marando, Mnyele & Co. Advocates), wakili nguli Mzee Mabere
Nyaucho Marando, ambaye alisema 'wasamehe tu hawa gazeti la Sauti Huru
maana ni vema kujenga marafiki wengi zaidi na media kwa kuwa wewe ni
kijana, kuliko kujenga maadui – na niliwasamehe bila gharama yoyote ile'.
Mzee Marando hakukosea, ila ukweli ni kwamba ukifanya hivyo utaona
patatulia kwa muda na baada ya hapo pataibuka tena jambo lingine la ukurasa
wa mbele linaloandikwa bila ukweli wowote ule! Imekuwa wimbo wa kawaida
kwenye baadhi ya media houses! Kufanya kazi kwa maslahi ya watu fulani ama
chama fulani, misingi ya weledi ya uandishi haipo! Cha muhimu ni maelekezo
ama utashi wa anayetoa chochote.
Jambo moja kubwa nililojifunza kutokana na yote haya ni kwamba, jambo
likiishaandikwa kwenye media halifutiki kwenye bongo za watu, hata muda
ukipita namna gani! Leo hii kila siku haya mambo yamekuwa yakirudiwa rudiwa
kwenye mitandao ya kijamii hata baada ya kuyatolea ufafanuzi wa kina.
Nimefika mahali nimeona niachane na passive ways za kushughulika na media
ili kuweka sawa kumbukumbu zangu mbele ya umma wa watanzania.
Ya ukweli: ni kweli kwamba ninamiliki hisa kwenye kampuni ya Emergent
Africa Ltd. Nina hisa 40% na mke wangu Dr. Bayoum Kigwangalla anamiliki
hisa 11%. Sijihusishi na kuendesha biashara hii kama mtendaji wa kila siku
– kampuni ina watumishi wake sehemu mbalimbali. Ni kweli kwamba kampuni ina
mradi wa kujenga chuo cha afya Nzega (International Institute for Health
Tabora), eneo la uchama, na ni kweli imepewa orodha ndefu ya vitu
ilivyosamehewa kodi na serikali kwa kuwa ni vitu/vifaa vya mtaji (deemed
capital goods). Ni kweli kwamba kampuni imewahi kuingiza nchini kontena
moja lenye vifaa vichache sana katika vinavyotajwa kwenye habari ile, na
vingi kati ya hivyo vipo aidha kwenye stoo ya kampuni iliyopo Nzega ama ya
Dar es salaam, Kigamboni. Kwa kuwa vipo, wanahabari wanakaribishwa kwenda
kuvitazama vitu hivi kama wanapenda.
Ya uongo: Si kweli kwamba nina hisa 78% na mke wangu Dr. Bayoum Kigwangalla
ana hisa 22% - ni uongo. Si kweli kwamba kampuni imeagiza vitu na
kuvipitisha bandarini na forodhani kwa msamaha kwa nia ya kuuza na hivyo
kuiibia serikali kwa njia ya kukwepa kodi. Si kweli kwamba kampuni ya
Emergent Africa Ltd imeingiza vifaa vyote ambavyo imepewa msamaha, kama
habari inavyotaka kuwaaminisha waTanzania. Sijawahi kuuza bidhaa zozote
zile za kampuni hii zilizoingizwa nchini kwa njia ya msamaha wa kodi.
Kampuni ya Emergent Africa Ltd haina mradi wa kuuza tiles na hivyo
haijawahi kufanya biashara hiyo.
Ingekuwa ni dhambi kubwa kama kweli ningekuwa naviuza vifaa hivi bila
kuvilipia kodi. Na kama ningekuwa sina mradi genuine wa ujenzi wa chuo na
labda nimetumia vibaya nafasi yangu ya ubunge kujipatia msamaha ili
kurahisisha biashara zangu basi ningeanza kwa kuuza cement (ambayo ni
bidhaa inayokimbia sana sokoni na kampuni yangu imepewa msamaha wa karibu
tani 5000 – lakini sijawahi kuutumia msamaha huu kununua hata mfuko mmoja
wa cement!). Ama ningeingiza mabati/vigae vya kuezekea (ambavyo pia
vinakimbia sana sokoni kwa kuwa watu wengi wanajenga – lakini sijaingiza
hata kigae kimoja!), ama ningeingiza malori 4, Nissan Navara pick up 4,
Mitsubishi Canter 2, Landcruiser Hardtop 4( ambazo zinatumika sana kwenye
utalii na hata kwenye barabara za vumbi) kwa msamaha – lakini sijaingiza
hata gari moja kati ya haya, kinyume na habari hii ya Tanzania Daima
inavyotaka kuuaminisha umma! Kuonesha uadilifu nitaeleza hapa mfano mmoja
kwamba mnamo Novemba mwaka jana nilinunua gari moja SUV aina ya Nissan
Patrol (T934 CDB) na nimeilipia kodi zote bila msamaha japokuwa ningeweza
kutumia msamaha wa kodi kununua na kuingiza moja ya magari yaliyopo kwenye
msamaha huu wa kampuni ambayo mimi ni major shareholder. Pia nina ujenzi wa
nyumba ya kuishi Nzega, Tabora na Dar es salaam katika hatua mbalimbali:
ningeweza kutumia msamaha huu wa kodi wa kampuni yangu ili kujipatia unafuu
kwenye manunuzi ya vifaa mbalimbali vya ujenzi kama cement, vigae ama
mabati, lakini sijawahi kufanya hivyo hata siku moja!
Kuwa na hisa kwenye kampuni inayofanya biashara halali siyo dhambi. Kupata
msamaha wa kodi siyo dhambi. Dhambi ingekuwa kuviuza baada ya kupata
msamaha. Kama kuna mtu anaamini kuwa kuna vifaa vimeuzwa na kampuni yangu,
kati ya hivi vilivyoingizwa nchini kwa msamaha, anakaribishwa kuleta
uthibitisho wa nyaraka za mauzo (cash sale receipts, tax invoice ya mauzo,
pay-in slip ya benki ya malipo, delivery note, ama receipt yoyote ile ya
kampuni hii inayoashiria kuwa mauzo yamefanyika) ili niweze kufuatilia
kujua ni nani aliyeuza na kwa nini alifanya hivyo ili niweze kuchukua hatua
za kinidhamu dhidi yake ikiwa ni pamoja na kumpeleka mbele ya vyombo vya
sheria.
Msamaha wa vifaa hivi ni kwa ajili ya Ujenzi wa Chuo Cha Afya Nzega
(kitakachoitwa International Institute for Health Tabora), ambacho
nilikianza kwa fedha zangu mpaka pale kilipofikia na sasa tunasubiria
majibu ya benki ya maombi yetu ya mkopo ndipo tuendelee. Na msamaha huo upo
na hautotumika kwa mambo mengine ya binafsi kama nilivyoeleza hapo juu
kwenye ununuzi wa gari langu binafsi la kutembelea na ujenzi wa nyumba
yangu binafsi ya kuishi Nzega, Tabora ama Dar es salaam (ambako ninajenga).
Watanzania tuache kushabikia uongo. Kufanya hivyo kunaziba mianya ya ukweli
kutamalaki. Tuache kutazama mambo kwa macho ya wivu, husda na majungu.
Tusimame kwenye misingi ya ukweli daima. Nchi hii itaendelezwa na watu
wenye kuchukua maamuzi thabiti na hatua za maksudi za kuleta mabadiliko –
kama miradi ya namna hii (ya chuo cha afya Nzega kule!). Nchi yetu bado ina
watu waaminifu na waadilifu na tunaamini tutafanikiwa kuwadhibiti walio
waovu. Hata siku moja kweli haijawahi kushindwa vita na uongo. Si kila mtu
aliyeko kwenye uongozi ndani ya CCM basi ni fisadi, watu wazuri na wasafi
wapo pia. Tusimuangalie kila mtu kwa sura ya 'ufisadi' na 'ubadhirifu' tu!
Tuaminiane jamani. Tusifedheheshane na kukatishana tamaa. Safari kuelekea
mapinduzi ya maisha ya watanzania kiuchumi na kijamii bado ni ndefu lakini
tutafika. Tufanyeni kazi.
Taarifa hii nimeiandika na kuitoa mimi mwenyewe, Hamisi Andrea Kigwangalla,
M.D., Mbunge, Jimbo la Nzega. (simu yangu ya kiganjani ni 0782636963 na
email yangu ni hkigwangalla@gmail.com, website: www.hamisikigwangalla.com )




2013/5/1 paul lawala <pasamila292000@gmail.com>

> Mrema
>
> Hiyo ndiyo hoja,udhaifu wa kimfumo,kisheria nk
>
> Kama fursa za bwerere zinapatikana binadamu ni rahisi kuitumia,ndiyo maana
> tunatakiwa tuanze kufaya kazi Ki-Kagame
>
>
> 2013/5/1 Herment Mrema <hmrema11@hotmail.com>
>
>> Ukweli uko pale pale. TRA wameishauri serikali kupunguza msamaha wa kodi
>> lakini baada ya msamaha kupungua unaongezeka kila mwaka. Repoti ya
>> Mthibiti Mkuu wa Serikali inasema misamaha inayotolewa haina uwiano na
>> manufaa kwa nchi. Nyinyi mnafikiri ni wanani hao ambao wanafaidika na
>> misamaha hii ya kodi?. Ni wanasiasa ambao wamekuwa wafanyabiashara
>> wababaishaji kwani biashara hawazijui na wafanyabiashara walioamua kuwa
>> wanasiasa uchwara kwani siasa hawazijui kisa kupata fedha za bwerere kama
>> hizi alizopata Mhechimiwa Dr. H.K.. Uzuri hayuko peke yake wako wengi sana
>> na ndio wala nchi.
>>
>> Kazi kwetu
>>
>> Ahsante
>>
>> Herment
>>
>> ------------------------------
>> Date: Wed, 1 May 2013 12:29:15 +0300
>> Subject: Re: [wanabidii] Kigwangallah na tuhuma za ufisadi
>> From: semkiwas@gmail.com
>> To: wanabidii@googlegroups.com
>>
>>
>> Maurice, Hamisi mwenyewe mpaka sasa yuko kimya labda anaandaa ufafanuzi
>> wa jambo hili tuvute subira
>> Swalehe,
>> 2013/5/1 Maurice Oduor <mauricejoduor@gmail.com>
>>
>> Hamisi mwenyewe asemaje about this accusation?
>>
>> Courage
>>
>>
>> 2013/5/1 Selemani Swalehe <semkiwas@gmail.com>
>>
>> Kwa kweli inabidi muheshimiwa Kigwa atueleze kwa kina wana Nzega
>> kuhusu tuhuma hizi maana ni nzito hadi zimepitiliza .Amejenga jengo pale
>> Uchama sambamba na Petrol Station ya msomali kumbe ni kiini macho
>> tena halijamalizika kujengwa ametudanganya kuwa anajenga chuo, kumbe ndio
>> ile wanayosema Kalaga baho na ubozi wako. Bila ufafanuzi wa kina kwa
>> tuhuma hii hatukubali wana Nzega tutahamasishana tuandamane. Kama hii ni
>> kweli ni afadhali Seleli arudi.
>> Swalehe,
>>
>> 2013/5/1 Emmanuel Muganda <emuganda@gmail.com>
>>
>> Kigwangallah matatani kwa tuhuma za ufisadi
>>
>>
>> na Josephat Isango
>>
>> MBUNGE wa Nzega, Dk. Hamisi Kigwangalla (CCM), anadaiwa kuliibia
>> taifa kwa kutumia vibaya misamaha ya kodi ya mamilioni ya shilingi kwa
>> ajili ya ujenzi wa chuo cha afya eneo la Uchama, wilaya ya Nzega.
>> Kwa mujibu wa nyaraka ambazo Tanzania Daima Jumatano imezipata, Dk.
>> Kigwangallah amejipatia misamaha ya kodi ya ongezeko la thamani na ushuru
>> wake kupitia kampuni ya Emergent Africa Limited, anayoimiliki kwa asilimia
>> 78 na Bayoun Kigwangallah ana asilimia 22.
>> Kupitia kampuni hiyo, mbunge huyo ameingiza nchini bidhaa mbalimbali
>> ambazo badala ya kuzielekeza katika ujenzi, amefungua duka la kuuza vifaa
>> vya ujenzi eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam na nyingine anaziuza kwa
>> wafanyabiashara wengine.
>> Nyaraka hizo zinaonyesha kuwa kampuni ya Emergent Africa Ltd, ilisajiliwa
>> katika Kituo cha Taifa cha Uwekezaji (TIC) Septemba 27, 2011 na iliruhusiwa
>> kupata misamaha hiyo kuanzia Septemba 2011 hadi Agosti 2014.
>> Kwa mujibu wa makubaliano kati ya kampuni ya Emergent Afica Ltd na TIC,
>> Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) iliombwa kuisamehe kodi kampuni hiyo ya
>> Dk. Kigwangallah vitu mbalimbali vyenye orodha toka namba 1 hadi 390.
>> Bidhaa hizo kwa uchache ni kompyuta 1042, mashine za kutolea kopi 12,
>> printa 12, 'binding machines' 12, vikokotozi (calculator) 640, projekta 12,
>> video kamera 12, feni 30, vifaa vya simu masanduku 28, jenereta moja,
>> magari aina ya Toyota 13, lori 3, Nissan Navarra Pik up 4, Mitsubishi
>> Canter 2 na mabasi madogo manane.
>> Pamoja na msahama huo, Dk. Kigwangallah kupitia kampuni hiyo, aliingiza
>> nchini vitu bidhaa mbalimbali vikiwemo vigae vya sakafuni 2500 vyenye
>> ukubwa wa 600X600 na 1000 vyenye ukubwa wa 400 X 400 pamoja na vigae vya
>> ukutani.
>> Katika orodha hiyo viko viti na meza za kulia, hema la bustanini, sofa,
>> kabati za kuwekea nguo, mazulia, vitanda na magodoro, televisheni na
>> vingine.
>> Aidha nyaraka hizo zinaonyesha baada ya kupokea bidhaa hizo kutoka nchini
>> China, ziliuzwa katika maduka mbalimbali ya Kariakoo na vigae vingine
>> kuuzwa kwa mkuu wa wilaya moja mkoani Tanga (hatukumtaja) kwa kuwa
>> hakupatikana kujitetea.
>> Hata hivyo, kumeonekana utata katika nyakara hizo kwani kampuni ya Delmas
>> iliyosafirisha kontena la bidhaa hizo kuja kwa Dk. Kigwangallah, ziko
>> tofauti na ankara za malipo.
>> Ankara hizo zinaonyesha kuwa zilitolewa na makampuni ya Louis Valentino
>> Investment and Development Co. Ltd iliyopo Na. 19 Ji Hua 3 Road Foshan na
>> Sharpeye Furniture.
>> Wakati manunuzi yakionekana kufanyika China Oktoba mosi, 2012, nyaraka
>> nyingine zinaonyesha kuwa mali zilishaingizwa nchini tangu Aprili 14 mwaka
>> huo, kupitia kampuni ya Innovative Freight yenye TIN 100-145-596, risiti
>> namba 2012/0000002986.
>> Na nyaraka za mamlaka ya mapato zinaonyesha bidhaa hizo ziliingia nchini
>> Aprili 3 mwaka jana, hali inayoonyesha kupishana katika tarehe za kununua
>> na kuingiza bidhaa hizo.
>> Pia utata huohuo unaonekana katika taarifa za Shirika la Viwango Tanzania
>> (TBS) ambazo zinaonyesha bidhaa hizo zilikaguliwa Machi 28, 2012.
>> Huku kukiwa na orodha zinazotofautiana za makampuni mawili ya kibiashara
>> wakati ankara ya malipo ilikuwa moja.
>> Taarifa zaidi zinaonyesha kuwa kontena hilo lilipofika nchini lilionekana
>> kuwa na vitu tofauti na vile vilivyoorodheshwa, hivyo kusababisha kontena
>> hilo kufanyiwa uchunguzi usio wa kawaida kwa kupekua mzigo mmoja mmoja.
>> Dk. Kigwangallah alipotafutwa kwa simu kufafanua tuhuma hizo, alisema
>> amebanwa na kazi. Na alipoambiwa ametumiwa maswali kwenye barua pepe yake,
>> aliahadi kujibu lakini hakufanya hivyo.
>> Alipopigiwa tena jioni, alisema, "Sema haraka unataka nini?" Alipoulizwa
>> juu ya tuhuma hizo alikata simu.
>> Lakini baadaye aliandika ujumbe kwa simu: "Nitakupigia jioni nikitoka
>> bungeni."
>> Alipoambiwa inaandikwa habari gazetini, alijibu kwa ujumbe mfupi kuwa
>> tuhuma zilikuwa za uongo bila kufafanua.
>>
>> --
>> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>>
>> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
>> ukishatuma
>>
>> Disclaimer:
>> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any
>> legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts
>> must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you
>> agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>> ---
>> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
>> "Wanabidii" group.
>> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
>> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>>
>>
>>
>>
>>
>> --
>> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>>
>> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
>> ukishatuma
>>
>> Disclaimer:
>> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any
>> legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts
>> must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you
>> agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>> ---
>> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
>> "Wanabidii" group.
>> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
>> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>>
>>
>>
>>
>>
>> --
>> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>>
>> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
>> ukishatuma
>>
>> Disclaimer:
>> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any
>> legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts
>> must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you
>> agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>> ---
>> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
>> "Wanabidii" group.
>> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
>> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>>
>>
>>
>>
>>
>> --
>> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>>
>> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
>> ukishatuma
>>
>> Disclaimer:
>> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any
>> legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts
>> must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you
>> agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>> ---
>> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
>> "Wanabidii" group.
>> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
>> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>>
>>
>>
>> --
>> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>>
>> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
>> ukishatuma
>>
>> Disclaimer:
>> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any
>> legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts
>> must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you
>> agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>> ---
>> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
>> "Wanabidii" group.
>> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
>> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>>
>>
>>
>
> --
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree
> to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>
>
>



--
"Vision is the ability to see the invisible!"
Hamisi A. Kigwangalla, MD, MPH, MBA
P.O.Box 22499,
Dar es salaam.
Tanzania.
Phone No: +255 754 636963
+255 782 636963
website: www.peercorpstrust.org or www.hamisikigwangalla.com
Email: hamisi.kigwangalla@peercorpstrust.org or info@hamisikigwangalla.com
Skype ID: hkigwangalla
Blog: blog.hamisikigwangalla.com




--
"Vision is the ability to see the invisible!"
Hamisi A. Kigwangalla, MD, MPH, MBA
P.O.Box 22499,
Dar es salaam.
Tanzania.
Phone No: +255 754 636963
+255 782 636963
website: www.peercorpstrust.org or www.hamisikigwangalla.com
Email: hamisi.kigwangalla@peercorpstrust.org or info@hamisikigwangalla.com
Skype ID: hkigwangalla
Blog: blog.hamisikigwangalla.com

--
-- -~--
muXalumni | Discuss, Share, Inform
Online: http://groups.google.com/group/muXalumni?hl=en
Facebook: Search for muXalumni
Twitter: @muXalumni
Blog: http://muhimbili.blogspot.com/


---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "muXalumni" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to muxalumni+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.



--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.



--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment