Friday 3 May 2013

Re: [wanabidii] HAYA NDIO YANAYOUWA MAKANISA YA KILOKOLE

Poleni, ibada ndefu bila uwepo wa Roho Mtakatifu ni sawa na makelele na husababisha watu kuchoka, au pia uchovu husababishwa na mtu mwenyewe kutokua konnected na vitu vya juu, ibada hupaswa kufanywa na mtu kila iitwapo leo, na ana heri anayeweza kufanya ibada na kuwa karibu na uwepo wa Mungu muda mrefu, maana hata Yesu aliwaambia hamkuweza kuwa nami hata lisaa limoja? kwa maisha ya sasa unakuta lisaa limoja kwa watu wengi ni shughuli, na sio rahisi
kuwepo kwenye uwepo wa Mungu na watakatifu wengine ni jambo jema na hasa ukizingatia kwamba watu wengi hufanya ibada mara moja kwa wiki, sasa kama ibada ya wiki na yenyewe ikiwa fupi mara nyingi haitoshi kumtoa mtu katika hali ya kimwili na kumsaidia kumweka katika hali ya kiroho,  na haitoshi kumbadilisha mtu ili aendelee kufanana na Yesu siku hadi siku. ndio maana wengine wanafanya ibada ndefu, lakini ibada ndefu bila Roho wa Mungu kuwepo ni uchovu na mara nyingi hazina faida kwa mtu wala kumsaidia kubadilika.

Na ni msingi sana kukaa kwenye neno la Mungu, kuna watu wengi wametolewa kwenye imani kutokana na kukwazwa na vitu vidogo vidogo, kama utajiri wa wachungaji, either kuwa na pesa, nyumba na  hata magari, hayo yamewasababishia kuwa na uchungu moyoni, na hivyo kuwatoa kwenye mstari wa neno la Mungu.  Kama mahali panakukwaza si utafute panapokufaa? maana mwisho wa siku usijekosa mbingu kwa ajili ya makwazo madogo madogo.  Mchungaji ni binadamu kama binadamu mwingine mwenye dhamana kama amepewa na Mungu haya, kama na viongozi au yeye mwenyewe hatujui ni siri ya kila mtu nao wana mapungufu yao.  Ingekua Yesu yupo hapa ndio mhubiri ni kweli, lakini anatumia hao hao ambao hawajakamilika ili  kupitisha ujumbe wake. 
Maana hakuna aliyekamilika akafanana na Yesu, kuna wengine wameokoka tena wanapanda mpaka madhabahuni lakini matendo yao ya sirini ni siri zao wenyewe na hao utasemaje?, wote tunasubiri neema ya Yesu ituponye na kutusogeza kutoka utukufu hadi utukufu.

Asante





2013/5/2 Tracy John <tracykwetu@gmail.com>
TUSIPOKUWA MAKINI NA TUSIPOANGALIA MAKANISA YA KIPENTEKOSTE YATAKUWA HAYAVUTII KABISA RIKA FULANI LA WATU MAANA KUNA MAMBO MENGI AMBAYO TUNADAI NI MUNGU AU ROHO MTAKATIFU AMBAYO HAYANA UHUSIANO KABISA NA MUNGU NA ROHO MTAKATIFU. RIKA LA WASOMI NA WATU MASHUHURI KATIKA JAMII TUTASHINDWA KABISA KUWAVUTA KWA BWANA MAANA KUNA UPUUZI MWINGI AMBAO TUNAUFANYA KWA JINA LA ROHO MTAKATIFU AMBAYO HAYANA UHUSIANO WOWOTE NA ROHO MTAKATIFU.

IBADA NDEFU KULIKO KAWAIDA KWA KUDAI KUWA NI ROHO MTAKATIFU ANATEMBEA ZINAWAKWAZA SANA WATU HASA WATU WA MIJINI NA MAJIJINI AMBAO WANA MAMBO TELE YA KUFANYA KUKIMBIZANA NA HALI YA MAISHA INAVYOKWENDA. JE, WAPENTEKOSTE WENZANGU HATUWEZI KUFANYA IBADA FUPI ZAIDI ILI MTU AJUE ANAKUJA KUABUDU NA BAADA YA HAPO ANAENDA KWENYE SHUGHULI ZAKE?

IBADA ZA KILA SIKU. HIVI KWELI WATU HAWANA KITU KINGINE CHA KUFANYA ZAIDI YA KUJA KWENYE IBADA KILA SIKU?

KUHUBIRI JUMBE AMBAZO HAZIJAANDALIWA VIZURI VYA KUTOSHA AMBAZO HAZINA NYAMA ZA MAARIFA YA KIMUNGU NA AMBAZO HAZINA UWEZO WA KUWASAIDIA WATU KUMWAMINI MUNGU KUTATUA CHANGAMOTO MBALI MBALI WANAZOKUTANA NAZO KATIKA MAISHA. JUMBE ZETU ZINA HALELUYAH, BWANA ASIFIWE, MPE BWANA MAKOFI, SHANGILIA, KULIKO KUWA NA NYAMA ZA KUSAIDIA WATU KUMJUA MUNGU ZAIDI.

KUWAFANYA WATU KAMA WATOTO WA CHEKECHEA WAKATI WANA HESHIMA ZAO. SEMA HALELUYAH MARA SABA ALAFU YA SABA ISEME KWA MUDA MREEEEEEEFUUUUUUU. DUH! AIBU. NDO MAANA WATU WENYE AKILI TIMAMU WANAYAKIMBIA MAKANISA YETU.

MAKANISA YETU MENGI TUNAJIINUA SISI WENYEWE KATIKA MAZUNGUMZO YETU NA KUWASHUSHA WATUMISHI WENZETU WAKATI TULITAKIWA KUMWINUA YESU NA KUMSHUSHA SHETANI. KUINUA BARAKA NA KUSHUSHA LAANA. KUZIINUA NGUVU ZA MUNGU NA KUSHUSHA ZA SHETANI.

YAPO MENGI SANA YANAYOKERA. TUSIPOBADILIKA TUTAENDELEA KUTOFAA KWA KIZAZI HIKI.

JIULIZE SWALA MPENDWA HIVI UKIONDOA KWENYE IBADA YAKO KILA KISICHO MUNGU AU KISICHO SAWA NA MAANDIKO UTABAKI NA IBADA?

KAMA UMEGUSWA NA UJUMBE HUU UWEKE KATIKA COMMENT KILE AMBACHO WEWE UNAONA I KERO KATIKA NAMNA TUNAVYOIENDESHA KAZI KAMA MAKANISA YANAYOAMINI KATIKA NGUVU YA ROHO MTAKATIFU.

BILA KUSAHAU SWALA LA KUTOZA SADAKA, MAANA ILE SIO KUTOA SADAKA NI KUTOZA SADAKA KWA KILA KITU AMBACHO WATU WANAMWAMINI MUNGU KWACHO. ACHA KUWACHOCHEA WATU KUTOA, WAFUNDISHE KANUNI ZA MUNGU ZAUTOAJI KIBIBILIA NA KAMA HAIPO KWENYE BIBILIA ACHANA NAYO ALAFU WAACHIE WATU MAAMUZI YA WATATOA AU HAWATATOA, WATATOA NINI NA KWA KIWANGO GANI. ACHA KUFANYIA WATU MAAMUZI ENEO HILO.

NGOJA NIACHIE WENGINE WAONGEZE.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 



--
Doroles Msimbira,
P.O Box 3454,
Dodoma.
Tel: +255787572392, +255754572392
Jesus Loves You, he asks you to surrender your life to him

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment