Wednesday 8 May 2013

Re: [wanabidii] HAYA NDIO YANAYOUWA MAKANISA YA KILOKOLE

Ibada ambayo nahudhuria mimi Jumapili inachukua takriban saa moja tu. Si tatizo kwangu. Ila ninakwazika pale matangazo yanaposhukua muda mrefu kuliko ibada yenyewe. Kwa kweli matangazo yangetakiwa yawe brief na yasiondoe maana ya ibada. Matangazo yangekuwa yanatolewa kwa ufupi na yabandikwe kwenye sehemu za matangazo ili wale wenye kutaka kujua details waende. Kwa maisha ya mijini muda ni tatizo sana. Kuna wengine wana majukumu ya kazi hata siku za jumapili hususan wafanya biashara. Kuna siku maalum kama wiki ya pasaka ambapo kila mtu anakuwa amekaa kwa nia ya ibada tu na maofisi yanakuwa yamefungwa, hapo hakuna mwenye haraka hata kama ibada ingechukua siku nzima. Ukiangalia ibada zetu baada ya kukomunika baadhi wa watu wanaanza kutoka kwa kuwa wanajua kipindi cha matangazo kitawakwaza. Hawa wanakosa baraka za mwisho. Tujaribu kuwa accomodate hawa pia. Nakumbuka kanisa fulani Arusha kama sikosei (Ngarenaro) kuna ibada ya kwanza saa moja tu kwa ajili ya wafanya biashara. Ibada hii inapedwa na inajaa kweli kweli.
Kutoa sadaka ni wajibu wa kila muumini, sasa kama ukitoa huku unalingalisha maisha yako na ya watumishi si sawa. Kweli kuna watumishi wanatia kufuru na bila shaka watumishi na wafanyabiashara wanafahamika. Kama unaona umeenda kwa mfanya biashara ambaye ndiye mmiliki wa kanisa, anakumiliki na wewe pia. Si sawa.
Ukienda kwa kanisa la fulani, ukamwabudu mungu wa fulani....... si sawa. Mungu hahodhiwi na mtumishi.

2013/5/8 Kilasara Fratern <kilasara.fratern@gmail.com>
"Mpeni Mungu yaliyo yake Mungu na Kaisari yaliyo yake Kaisari." Tena duniani humu, kila kitu ni kwa wakati. Mwanadamu inakupasa upange muda wako wa kufanya mambo yako (utumishi kwa Kaisari), na muda wa kumtumikia Mungu, na muda wa huo wa kumtumikia Mungu, ndio muda wa ibada, kusali, na kuimba. Tumezoea kumpunja Mungu muda. Ni wangapi kati yetu, wana muda wa nusu saa wa kumwomba na kumwabudu Mungu kila siku? Sidhani! Kwanini basi, kwa wiki, tusipate muda wa kutosha kwa ajili ya Mungu anayetupa, na aliye uhai wetu, angalau siku moja kwa wiki!

Kazi, japo fedha naipenda, lakini, kuna leo na kesho, kazi haziishi! Je, nitasema, utasema, nini mbele ya Mola wako? Wakati ukiwa hai, ulifanya nini, maana, kwa walio wakristu tumefundishwa kwenye mafundisho ya awali ya dini kuwa "Mungu ametuumba ili tumtumikie." Na kumtumikia kwetu ni kwa kuomba, tena kwa kuwaombea wengine wenye shida na mateso. Sasa, ni wangapi kati yetu tuna muda au huwa tunatenga muda kwa ajili ya ibida, na kama ni ibada tunaifanya kwa moyo na kwa uaminifu kama vile tunavyofanya kwenye kazi zetu za kuajiriwa?

Japo, nimemwelewa mtoa mada, lakini ukizingatia maana ya "Kwa nini inambidi binadamu kuomba? Kuwa, kuomba sio hiari yetu, bali ni wajibu, na ni lazima, kama kweli unategemea kumrudia Muumba wako, "MINI NIKO AMBAYE NIKO; si ungi mkono hoja hii." Kufanya hivyo ni sawa na kuendekeza ubinafsi wetu wanadamu. Tukubali, kama ni muda, kazi zetu, ambazo Mungu ametupa ili tupate riziki yetu, tule na kunywa, ili tusife njaa; lakini, kwa hali ilivyo na mwenendo wa maisha yetu ulivyo, tunazitumia kuwa bakora kwa Mungu wetu kwa kumnyima muda muda wa maombi! Muda wa maombi ndio muda pekee ambao Mungu anategemea akusikie wewe kwa kinywa chako ukimsifu na kumwabudu. Masifu yako na sala yako ndiyo sala na sadaka pekee anayoifurahia mungu wako kuliko fedha (sadaka). Sema, kikwazo kingine tunachokumbana nacho wakati mwingine ni kutokujua kuomba. Hili ndio wachungaji na mapadre wanatakiwa wawafundishe waumini wao kuomba, hasa, sala binafsi-rohoni kuliko kukariri sala za kwenye vitabu. Hata hivyo hii ni mada ambayo inaweza kujadiliwa panapo nafasi, lakini kwa mada hii, tunahitaji kwenye maisha yetu tuwe na muda wa kumwabudu Mungu.

Nawasifu sana wenzetu Waislamu, maana wao kwa siku, yapo masaa ambayo kwa wale walio waaminifu katika imani yao, inawapasa kwenda kusali. Hawajakosea kufanya hivi. Hata sisi Wakrsitu, tunapaswa kufanya hivi maana wengine wenzetu Wayahudi na Orthodox bado wanashikilia utaratibu huu na kwa Wakatoliki, utaratibu huu umebakia kwa Watawa (Mapadre na Masista). Haikupaswa kuwa hivi, bali ilipaswa ifuatwe na watu wote waumini.

2013/5/3 Kenneth Masuki <kennymasuki@gmail.com>
Wapendwa

Ushauri wangu ni huu kwa wote na hasa aloleta mada hii hapa jukwaani. Kama unaona hizo taratibu hazikufai basi wewe huna ushirika na kundi hilo la watu hivyo waache wao wanaofurahia mfumo huo waendelee kuliko kuanza kutoa kasoro kibao amabzo kwa mantiki hazikusaidii chochote. Masuala ya kiroho ni ya kiimani na wala hayahitaji kuvutia wala kuvutiwa, kama mtu huamini kinachofanyika huko kwanini unataka kuvutiwa kuingia huko, ili iweje? Imani siyo social club ambako wanawavutia wateja kwa kufanya mambo yanayo-appeal kwa kundi wanalolitarget. 

Tracy, unaposema kuwa [nanukuu] "RIKA LA WASOMI NA WATU MASHUHURI KATIKA JAMII TUTASHINDWA KABISA KUWAVUTA KWA BWANA MAANA KUNA UPUUZI MWINGI AMBAO TUNAUFANYA KWA JINA LA ROHO MTAKATIFU AMBAYO HAYANA UHUSIANO WOWOTE NA ROHO MTAKATIFU." Hao wasomi hao ni wapi tena maana kuna wasomi wengi tu waliobobea na hata watu mashuhuri ambao wamo makanisani na wameokoka. Mimi nafikiri kama mtu unachuki binafsi na mfumo fulani basi usijaribu kutafuta wafuasi ili kujijengea uhalali wa wewe kutoenda kujumuika na fulani kwa sababu zako binafsi. Pia napenda kukutaarifu kuwa Biblia inasema kuwa "Neno la Msalaba kwao wanaopotea ni UPUUZI lakini kwa waliokolewa ni nguvu ya MUNGU." 

Kuhusu suala la ibada ndefu mie sioni mgogoro wowoe hapo maana kwa tabia ya asili binadamu anapenda kutumia muda mwingi pale anapoona ana maslahi napo. Mfano utakuta wapenzi wanatumia muda mwingi pamoja ikiwa ni beach, au sinema au popote pale watakapoamua kuwepo. Naamini hata wewe Tracy, kama umeolewa au una mpenzi utakuwa unatumia masaa mengi kuwa naye kuonyesha mapenzi yenu kwa kila mmoja na siyo kukutana na kuongea mara moja kwa wiki kwa nusu saa tu. Je si halali kwa wale wanaompenda Mungu wao kutumia muda wao mwingi katika ibada? Pia kuwa na ibada hizo kila siku au mara kadhaa katika week?

Well nilikuwa napita tu nikaweka kituo kwa kitambo kidogo...Mbarikiwe

Ken

2013/5/3 Doroles Msimbira <dmsimbira@googlemail.com>
Poleni, ibada ndefu bila uwepo wa Roho Mtakatifu ni sawa na makelele na husababisha watu kuchoka, au pia uchovu husababishwa na mtu mwenyewe kutokua konnected na vitu vya juu, ibada hupaswa kufanywa na mtu kila iitwapo leo, na ana heri anayeweza kufanya ibada na kuwa karibu na uwepo wa Mungu muda mrefu, maana hata Yesu aliwaambia hamkuweza kuwa nami hata lisaa limoja? kwa maisha ya sasa unakuta lisaa limoja kwa watu wengi ni shughuli, na sio rahisi
kuwepo kwenye uwepo wa Mungu na watakatifu wengine ni jambo jema na hasa ukizingatia kwamba watu wengi hufanya ibada mara moja kwa wiki, sasa kama ibada ya wiki na yenyewe ikiwa fupi mara nyingi haitoshi kumtoa mtu katika hali ya kimwili na kumsaidia kumweka katika hali ya kiroho,  na haitoshi kumbadilisha mtu ili aendelee kufanana na Yesu siku hadi siku. ndio maana wengine wanafanya ibada ndefu, lakini ibada ndefu bila Roho wa Mungu kuwepo ni uchovu na mara nyingi hazina faida kwa mtu wala kumsaidia kubadilika.

Na ni msingi sana kukaa kwenye neno la Mungu, kuna watu wengi wametolewa kwenye imani kutokana na kukwazwa na vitu vidogo vidogo, kama utajiri wa wachungaji, either kuwa na pesa, nyumba na  hata magari, hayo yamewasababishia kuwa na uchungu moyoni, na hivyo kuwatoa kwenye mstari wa neno la Mungu.  Kama mahali panakukwaza si utafute panapokufaa? maana mwisho wa siku usijekosa mbingu kwa ajili ya makwazo madogo madogo.  Mchungaji ni binadamu kama binadamu mwingine mwenye dhamana kama amepewa na Mungu haya, kama na viongozi au yeye mwenyewe hatujui ni siri ya kila mtu nao wana mapungufu yao.  Ingekua Yesu yupo hapa ndio mhubiri ni kweli, lakini anatumia hao hao ambao hawajakamilika ili  kupitisha ujumbe wake. 
Maana hakuna aliyekamilika akafanana na Yesu, kuna wengine wameokoka tena wanapanda mpaka madhabahuni lakini matendo yao ya sirini ni siri zao wenyewe na hao utasemaje?, wote tunasubiri neema ya Yesu ituponye na kutusogeza kutoka utukufu hadi utukufu.

Asante

2013/5/2 Tracy John <tracykwetu@gmail.com>
TUSIPOKUWA MAKINI NA TUSIPOANGALIA MAKANISA YA KIPENTEKOSTE YATAKUWA HAYAVUTII KABISA RIKA FULANI LA WATU MAANA KUNA MAMBO MENGI AMBAYO TUNADAI NI MUNGU AU ROHO MTAKATIFU AMBAYO HAYANA UHUSIANO KABISA NA MUNGU NA ROHO MTAKATIFU. RIKA LA WASOMI NA WATU MASHUHURI KATIKA JAMII TUTASHINDWA KABISA KUWAVUTA KWA BWANA MAANA KUNA UPUUZI MWINGI AMBAO TUNAUFANYA KWA JINA LA ROHO MTAKATIFU AMBAYO HAYANA UHUSIANO WOWOTE NA ROHO MTAKATIFU.

IBADA NDEFU KULIKO KAWAIDA KWA KUDAI KUWA NI ROHO MTAKATIFU ANATEMBEA ZINAWAKWAZA SANA WATU HASA WATU WA MIJINI NA MAJIJINI AMBAO WANA MAMBO TELE YA KUFANYA KUKIMBIZANA NA HALI YA MAISHA INAVYOKWENDA. JE, WAPENTEKOSTE WENZANGU HATUWEZI KUFANYA IBADA FUPI ZAIDI ILI MTU AJUE ANAKUJA KUABUDU NA BAADA YA HAPO ANAENDA KWENYE SHUGHULI ZAKE?

IBADA ZA KILA SIKU. HIVI KWELI WATU HAWANA KITU KINGINE CHA KUFANYA ZAIDI YA KUJA KWENYE IBADA KILA SIKU?

KUHUBIRI JUMBE AMBAZO HAZIJAANDALIWA VIZURI VYA KUTOSHA AMBAZO HAZINA NYAMA ZA MAARIFA YA KIMUNGU NA AMBAZO HAZINA UWEZO WA KUWASAIDIA WATU KUMWAMINI MUNGU KUTATUA CHANGAMOTO MBALI MBALI WANAZOKUTANA NAZO KATIKA MAISHA. JUMBE ZETU ZINA HALELUYAH, BWANA ASIFIWE, MPE BWANA MAKOFI, SHANGILIA, KULIKO KUWA NA NYAMA ZA KUSAIDIA WATU KUMJUA MUNGU ZAIDI.

KUWAFANYA WATU KAMA WATOTO WA CHEKECHEA WAKATI WANA HESHIMA ZAO. SEMA HALELUYAH MARA SABA ALAFU YA SABA ISEME KWA MUDA MREEEEEEEFUUUUUUU. DUH! AIBU. NDO MAANA WATU WENYE AKILI TIMAMU WANAYAKIMBIA MAKANISA YETU.

MAKANISA YETU MENGI TUNAJIINUA SISI WENYEWE KATIKA MAZUNGUMZO YETU NA KUWASHUSHA WATUMISHI WENZETU WAKATI TULITAKIWA KUMWINUA YESU NA KUMSHUSHA SHETANI. KUINUA BARAKA NA KUSHUSHA LAANA. KUZIINUA NGUVU ZA MUNGU NA KUSHUSHA ZA SHETANI.

YAPO MENGI SANA YANAYOKERA. TUSIPOBADILIKA TUTAENDELEA KUTOFAA KWA KIZAZI HIKI.

JIULIZE SWALA MPENDWA HIVI UKIONDOA KWENYE IBADA YAKO KILA KISICHO MUNGU AU KISICHO SAWA NA MAANDIKO UTABAKI NA IBADA?

KAMA UMEGUSWA NA UJUMBE HUU UWEKE KATIKA COMMENT KILE AMBACHO WEWE UNAONA I KERO KATIKA NAMNA TUNAVYOIENDESHA KAZI KAMA MAKANISA YANAYOAMINI KATIKA NGUVU YA ROHO MTAKATIFU.

BILA KUSAHAU SWALA LA KUTOZA SADAKA, MAANA ILE SIO KUTOA SADAKA NI KUTOZA SADAKA KWA KILA KITU AMBACHO WATU WANAMWAMINI MUNGU KWACHO. ACHA KUWACHOCHEA WATU KUTOA, WAFUNDISHE KANUNI ZA MUNGU ZAUTOAJI KIBIBILIA NA KAMA HAIPO KWENYE BIBILIA ACHANA NAYO ALAFU WAACHIE WATU MAAMUZI YA WATATOA AU HAWATATOA, WATATOA NINI NA KWA KIWANGO GANI. ACHA KUFANYIA WATU MAAMUZI ENEO HILO.

NGOJA NIACHIE WENGINE WAONGEZE.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
--
Doroles Msimbira,
P.O Box 3454,
Dodoma.
Tel: +255787572392, +255754572392
Jesus Loves You, he asks you to surrender your life to him

-----------------------
Fratern Kilasara
,

P. O. Box - (Home): 62810; or (Office): 65300
Dar es Salaam - Tanzania.
Telephone (Office): +255 (0)22 2700021/4 Ext No. 239; Fax: +255 (0)22 2775591
Mobile (Personal): +255 (0)715 40 41 53 or +255 (0)754 40 41 53
Emails: kilasara.fratern@gmail.com or kilasara.fratern@yahoo.com

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
0 comments:

Post a Comment