Neville Unajua mengi, hapa ni kama unazunguka mbuyu tu. Mwaga hapa tusikie, tusome kisha tupime halafu tushauri. Sent from Yahoo! Mail on Android |
From: Neville Meena <nevilletz@gmail.com>;
To: <wanabidii@googlegroups.com>;
Subject: Re: [wanabidii] Charles Mullinda ajitoa kwenye Jukwaa la Wahariri Tanzania
Sent: Tue, May 21, 2013 4:55:16 AM
Felix, Demokrasia inakuruhusu kuwaza na kutegemea mengi kama unavyosema. Ila Mulinda aliandika Mtandao Hatari, kwa mtazamo wa hao wahariri aliocheka nao, kula nao na kusafiri nao wakasema kuna kasoro. Yeye akasema anafahamu mengi na ana ushahidi wa kile alichokiandika, kama akipewa nafasi basi ataweka wazi mengi kuhusu madai yake. Akapewa nafasi tena mkutano wa wahariri uliounda kamati yeye alikuwapo. Kamati ikamsikiliza yeye na wengine, taarifa ikaandikwa na ikasomwa yeye akiwapo. Akatoa utetezi wake, wahariri wakapima huo utetezi wakamkuta na hatia, wakamsimamisha. Kwa maana hiyo taratibu za kidemokrasia zilifuatwa yeye akiwa mshiriki kamili wa vikao vya TEF. Inawezekana hakuridhika, hilo ni jambo jingine. Kama kuna mambo mengine zaidi anaweza kuendelea kuandika maana sisi hatukumfukuza kazi, bado ni Mhariri wa Mtanzania Jumatano ila siyo sehemu ya TEF maana amekosa sifa kwa mujibu wa jukwaa letu. Maana ya kumsimamisha uanachama ni kumpa fursa ya kutafakari conducts zake na kama akiona anaweza atarejea. Lakini baada ya kumsimamisha yeye alitangaza kujitoa kwenye TEF, huo ni uamuzi wake ambao mimi binafsi ninauheshimu. Suala la waandishi wa habari kulalamikia wahariri ni sehemu ya demokrasia pia. Wanalalamikia uhuru wa wahariri kuwa na chama chao au umoja wao wa kukutana na kufanya mambo yao! Hili ni tatizo nchini mwetu kwamba vyama vingi vya waandishi wa habari vilianzishwa na kufa. Taja, AJM na vingine kadha wa kadha. Hivi leo tuna Press Clubs karibu katika mikoa yote nchini, lakini waandishi wa habari hawako tayari kuwa wanachama wa klabu hizo kwa sababu zao zao binafsi. Kigezo ni kwamba wanataka kuwa huru, ukijiuliza uhuru dhidi ya nani? Katika mazingira ya sasa ni ujinga na upuuzi kufikiri kwamba ,mwandishi wa habari anaweza kusimama peke yake. Nchi yetu na mazingira ya sasa ambako mtu kama Kibanda anaweza kufanyiwa alivyofanyiwa, vifo vya waandidhsi wa habari na mengine mengi ni utumwa kufikiri kwamba mnaweza kuishi katika tasnia ya habari bila kuwa na umoja. TEF kama taasisi inayokua lazima ikosolewe kama inakosea, lakini kasoro hizo haziondoi umuhimu wa kuwapo kwake. TEF imeonyesha njia kwamba waandishi wa habari wanaweza kuwa na umoja wao na ukafanya kazi na kujisimamia wenyewe. Msipoweza kujisimamia wajuzi kutoka nje ya tasnia watakuja kuwasimamia. Tuache kutukuza vya wengine, tukuzeni na kuheshimu kile kilicho chenu. 2013/5/20 Felix Mwakyembe <fkyembe@gmail.com>
-- Neville C. Meena, Secretary General, Tanzania Editors Forum - TEF, Dar es Salaam - Tanzania. Cell: +255 - 787 - 675555 +255 - 753 - 555556 Send Emails to wanabidii@googlegroups.com Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines. --- You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group. To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com. For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out. |
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment