Thursday 23 May 2013

Re: Re: [wanabidii] VURUGU MTWARA BAADA YA SERIKALI TAMKO LA SERIKALI KUHUSU GESI

Nimeikumbuka hutuba ya M. Robespierre ya tarehe 6-02-1794. Hii hapa ni tafsiri (kutoka lugha ya kifaransa) ya kisehemu tu cha hutuba hiyo.

We wish that order of things where all low and cruel passions are enchained, all the beneficent and generous passions awakened by the laws; where ambition subsists in a desire to deserve glory and serve the country; where distinctions grow out of system of equality, where the citizen submits to the authority of the magistrate, and where the magistrate obeys that of the people, and the people are governed by a love of justice; where the country secures the comfort of each individual, and where each individual prides himself on the prosperity and glory of his country; where every soul expands by a free communication of republican sentiments, and by the necessity of deserving the esteem of a great people: where the arts serve to embellish that liberty which gives them value and support, and commerce is a source of public wealth and not merely of immense riches to a few individuals...

The wisdom of government should guide its operations according to circumstances, it should time its measures, choose its means; for the manner of bringing about great things is an essential part of the talent of producing them, just as wisdom is an essential attribute of virtue...

Happily virtue is natural in the people, despite aristocratic prejudices. A nation is truly corrupt when, after having by degrees lost its character and liberty, it slides from democracy into aristocracy; this is the death of the political body by decrepitude...

The law of self-preservation with every being, whether physical or moral, is the first law of nature. Crime butchers innocence to secure a throne, and innocence struggles with all its might against the attempts of crime. If tyranny reigned one sigle day not a patriot would survive it. How long yet will the madness of despots be called justice, and the justice of the people be called barbarity or rebellion? How tenderly oppressors and how severely the oppressed  are treated! Nothing more natural; whoever does not abhor crime (by state) cannot love virtue. Yet one or the other must be crushed... This is a dreadful contest, which liberty maintains against tyranny; ....

To punish the oppressors of humanity is clemency; to forgive them is barbarity.



Da: Gikaro Ryoba <gikaroryoba@yahoo.com>
A: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>; "fkyembe@gmail.com" <fkyembe@gmail.com>
Inviato: Giovedì 23 Maggio 2013 12:08
Oggetto: Re: Re: [wanabidii] VURUGU MTWARA BAADA YA SERIKALI TAMKO LA SERIKALI KUHUSU GESI

Kwa yanayoendelea kutokea Mtwara watanzania hawapaswi kuwalaumu wakazi wa mtwara kwa sasbabu wanaleta fikra chanya kwa watanzania wengine juu ya kutetea rasilimali zetu ambazo zinatafunwa na viongozi wachache, wakishirikiana na wale wa nchi za magharibi.
 
Kwa muda mrefu sasa, nchi nyingi za kiafrica, Tanzania ikiwemo, zimekuwa nyuma kimaendeleo na wananchi wake wanaishi katika umaskini wa kutupwa wakati wamezungukwa na rasilimali nyingi. Mfano, mererani kuna mgodi mkubwa wa madini lakini ukitoka nje ya mgodi unakutana na kundi la watanzania wanaishi maisha ya taabu na umaskini wa kutupwa.
 
Hii yote ni kwa sababu viongozi wetu, chini ya CCM, wamekuwa hawajali shida za wananchi; badala yake wanajali matumbo yao na familia zao. Wanamtwara hawasemi kama gesi ni yao pekee bali wanataka serikali ifanye utaratibu wowote wa kujenga plant ya umeme mtwara halafu uingizwe kwenye gridi ya taifa. Wameona mbali kwamba gesi ikisafirishwa itaingia mikononi mwa mafisadi na kuiacha nchi inaendelea kuwa gizani kwani wanataka kuisafirisha hadi Dar ili kujinufaisha kibinafsi na viongozi waonekane wa maana mbele ya wachina, wazungu na wamarekani.
 
Watanzania wote tuzinduke na kudai mgawanyo sawa wa rasilimali zetu sio kila siku zinaporwa na wageni na kuachiwa mashimo. Kwa nini kila kitu Dar na tayari mji ushajaa? Tufikiri sana faida ya maamuzi ya wanamtwara kwani inawafumbua masikio na macho watanzania wote wenye uchungu na rasilimali zetu zinazoporwa kila kukicha na wageni huku wazawa tukiendelea kuwa maskini wa kutupwa. Tafakari, chukua hatua!

----- Original Message -----
From: ELISA MUHINGO <elisamuhingo@yahoo.com>
To: fkyembe@gmail.com; wanabidii@googlegroups.com
Cc:
Sent: Thursday, May 23, 2013 11:30 AM
Subject: Re: Re: [wanabidii] VURUGU MTWARA BAADA YA SERIKALI TAMKO LA SERIKALI KUHUSU GESI

Felix kwa sentenso yako ya mwisho ili tusigombane sisi kwa sisi huo uongozi dhaifu ujikakamue utuelekeze kujadiliana na wana Mtwala. Ukithubutu kutumia nguvu basi darfur. Na waliowashawishi wanataka hilo. Jingine. Tujadili wanalotamka watu wa Mtwara. Hawasemi wanataka gesi iishie huko. Ni upumbavu kupotosha hapo maana hatutakuwa na la kujadili.

----------
Sent from my Nokia Phone

------Original message------
From: Felix Mwakyembe <fkyembe@gmail.com>
To: <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Thursday, May 23, 2013 9:52:40 AM GMT+0300
Subject: Re: [wanabidii] VURUGU MTWARA BAADA YA SERIKALI TAMKO LA SERIKALI KUHUSU GESI

Ezekiel,

Hatuwezi kuhalalisha yanayotekea Mtwara kwa sababu ya kusahauliwa. Ni
Watanganyika wangapi waliokumbukwa na hiyo serikali, vipi kuhusu Rukwa
ambao pamoja na kutekezwa lakini ndio wenye kuwalisha hata hao wa Mtwara,
vipi kuhusu Tabora, Kigoma, Mbeya, Iringa, Ruvuma, Katavi, Kagera, nk.

Tatizo la umasikini linawakaba Watanzania wote, watu wameingia Mtwara
wakatumia udhaufu wa umasikini wetu na kuchochea vurugu, hapana lazima
tukatae vurugu.

Tukumbuke hizi vurugu zimeanza baada ya taarifa za kuwepo kwa hizo
rasilimali, ni mazingira hayo hayo yanayozifanya nchi kama DRC, Somalia,
Sudan, na nyinginezo kuwa katika machafuko miaka yote.

Tanzania tuna matatizo  ya kiuogozi kama taifa, lakini pia tuelewe kuna
nguvu kutoka nje zenye lengo la kutugonganisha ili wajichotee rasilimali
hizo bila bughudha wakati sisi akili iko kwenye kupigana wenyewe kwa
wenyewe.

Felix


2013/5/23 Ezekiel Massanja <ezekielmassanja@gmail.com>

> Maelezo yako dada Hilda mazuri sana lakini yana kasoro za msingi. Baadhi
> ya sababu ulizozitoa unaweza kuzitafiti tena kuona ukweli wake. Watu wa
> Mtwara wanalilia maendeleo Yao baada ya kusahauliwa kwa MUDA mrefu. Kwa
> MUDA mrefu pato la taifa halikugawiwa kwa Haki. Naweza kukupa mifano
> michache tu: Angelia barabara zinazoenda kusini na zile zinazoenda
> kaskazini, kwa nini miundombinu  Hii muhimu itofautiane kiasi hicho wakati
> nchi ni moja hii hii. Ni kweli Kwamba hata watu wa Maganzo kwenye almasi
> maendeleo Yao hayalingani na utajiri ulio jirani hapo. Ni kweli Kwamba
> tujikita kwenye majimbo wengine ambao hawana HAYO madini na gesi
> watafanyaje? Basi kile kinachopatikana kigawiwe kwa haki, wote wapate,
> ndipo hiyo amani iwe ya kudumu.
>
>
>
> wasalaam
>
>
>
> On Wednesday, May 22, 2013, Hildegarda Kiwasila wrote:
>
>>
>> Radio zimeongea vizuri zaidi zimetoa maelezo makini ya kinachoendelea na
>> uharibifu unaofanyika na waandishi wa habari kuwindwa eti wakiongea
>> wanaipendelea serikali. Kwa hali ilivyo Mtwara sasa, wageni ni wengi sana
>> wanaohusika na utafiti na shughuli za miradi ya maendeleo funded by
>> international devemopment organizations. Ni hatari sana kama watawavamia
>> hawa na kuwadhuru.
>>
>> Ikiwa suala ni Gas ibaki kwao, basi watu wa Kihansi na huko Ruaha-Mikumi
>> Kilombero, Pangani 1 and 2 Tanga; Mtera, Nyumba ya Mungu dam ambao hata
>> kuvua huzuiwa nao waanzae kukata milingoti ya Miti kuzuia umeme Usije Dar
>> na Maeneo mengine? Mungu atusaidie. Mbona mafao ya National park, Madini
>> tunatumia nchi nzima kama sources za hela za nchi ambapo hata wafugaji na
>> wakulima kando ya mbuga hizo kuingia protected areas wanaadhibiwa?
>>
>> Kwao hao vijiji vingine vyenye vyanzo vya umeme umeme unapita juu angani
>> ya waya za umeme wao wanamulikia mienge ya moto. Hawana benefits na benefit
>> sharing ni mkakati mpya wa sasa kimataifa kuanzia RIO Summit 1992.
>>
>> Maji yanatoka Ruvu, wami yananywewa mijini kuko vijijini misitu ni
>> protected wasitumie ili maji ya mto yapatikane kwenye intakes yafike e.g.
>> DSM. Tukifanya hivi kwamba kila mwenye ambako resource ipo azuie hatutofika
>> mbali. Issue ni planning for benefit sharing. Wao watafaidikaje? Kuwe na
>> mpango katika aina zote za resources ambazo zinatambulika kama mali ya umma
>> sio binafsi. Hatutatatua matatizo kwa kuharibu miundo mbinu. Kubomoa daraja
>> na mwenye mimba sasa na hofu ya mapambano uchungu utakuja haraka. Jee,
>> utamsafirishaje unapokataza wasitoke nje na kuharibu miundo mbinu? Kweli
>> tunafurahia haya na wengine kuona kuwa ndio faida ya utawala ni wa kifisadi
>> ambapo mafisadi ni waume na ndugu zetu. Wakishitakiwa-tunaweka mawakili
>> wazito. Na wakirudi home hao mafisadi tunawapigia KURA sisi wenyewe
>> wanashinda tena. Jamani tumrudie Mungu.
>>
>> --- On *Wed, 22/5/13, Juma Mzuri <jumamzuri@gmail.com>* wrote:
>>
>>
>> From: Juma Mzuri <jumamzuri@gmail.com>
>> Subject: Re: [wanabidii] VURUGU MTWARA BAADA YA SERIKALI TAMKO LA
>> SERIKALI KUHUSU GESI
>> To: "Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
>> Date: Wednesday, 22 May, 2013, 12:25
>>
>> Huko MIKINDANI ofisi zote za serikali zavamiwa na kuchomwa na mpaka
>> daraja la Mikindani nalo limevunjwa kwa maana hauwezi kutoka wala kuingia
>> MTWARA
>>
>> Kuna madai kwamba silaha zimeibiwa (Haijathibitishwa)
>>
>> Maaskari wanafanya msako wa nyumba hadi nyumba maeneo ya Magomeni na
>> Mangowela
>>
>> Askari achomwa mshale. Haijulikani hali yake
>>
>> Ni mapambano baina ya vijana na maaskari. Vijana hawaogopi tena risasi
>> wala mabomu .
>>
>> Kundi limeelekea Shangani kwenye nyumba za vigogo.
>>
>>  Nyumba ya kupumzikia wageni inayoitwa Shengena Lodge imechomwa moto kwa
>> kile kinachoelezwa kwamba iliwapokea askari Polisi.
>>
>> Ofisi ya CCM saba saba imechomwa moto, na baadhi ya waandishi
>> wamezingirwa maeneo ya Sokoni, sasa ni milio ya risasi na mabomu.
>>
>> Matairi  kila  kona  ya mji  yamechomwa  barabarani  polisi  na  zimamoto
>>  wanafanya kazi ya kuzima na kufukuza wananchi. Kauli mbiu "Gesi haitoki
>> hata kwa bomba la peni"
>>
>> Kambi ya Upinzani yaukataa mpango wa serikali wa ujenzi wa bomba la gesi
>>
>> Nyumba kadhaa  za watumishi  wa Serikali  zimechomwa  maeneo ya
>> Shangani.(habari haijathibitishwa rasmi)
>>
>> Ni magari ya FFU tu ndio yapo barabarani nayo hupata wakati mgumu kupita
>> kwasababu ya mawe na magogo yaliyowekwa na vijana,baadhi ya watu kadhaa
>> wamechukuliwa na askari eti kwakuwa walipita jirani na gari yao,askari
>> wengi waliokuja si wa hapa Mtwara wengi wametoka Masasi na Lindi. Ving'ora
>> vinalia ovyo ovyo.
>>
>> watoto wamefungiwa mashuleni walimu wamekimbia
>>
>> Vituo vya Redio vya Mtwara havizungumzii hali hii ya hatari. Vinapiga
>> Muziki pengine vinakusanya matukio na habari ya majanga haya. Ili Wananchi
>> wayapate .
>>
>>  Mabomu yanapigwa mfululizo maeneo ya Magomeni-Mtwara . Takriban mabomu
>> 20 na ushee mpaka sasa. Na wanaendelea kupiga mabomu.
>>
>> Sasa hali si shwari kila eneo, wakionekana watu watatu wanaongea maongezi
>> maaskari wanapiga mabomu. Mabavu yamechukua mkondo wake. Wananchi
>> wamejifungia majumbani mwao. Chuki dhidi ya Polisi yaimarika. Polisi
>> wanapiga mabomu bila mwelekeo.
>>
>> Magomeni na sokoni kimenuka, mabomu yanarushwa na wananchi wanakimbia
>> ovyo.
>>
>> Kituo  kimoja  cha habari  kinachorusha habari za bunge chazuia mawimbi
>> yake kwa Mkoa wa Mtwara hivyo hakisikiki(Redio na TV). Na kimewanyima haki
>> wananchi wa Mtwara ya kupata taarifa.(Hatimaye wamerejesha matangazo yao)
>>
>> Waziri wa Nishati amesoma hotuba yake kwa hisia kali na mbwembwe.
>> Mwishoni amesema bomba la gesi linajengwa kutoka Mtwara kwenda Dar.
>>
>>
>> Maduka yote yamefungwa, baa zimefungwa, hakuna huduma za usafiri, ofisi
>> za serikali zimepwaya kimsingi hakuna lolote linalofanyika
>>
>> Boda boda zinazoonekana maeneo ya Nkanaledi na abiria zinapigwa mawe.
>>
>> Makachero nao wanajifanya madereva wa boda boda na Bajaji, Tax wengine
>> wanatembea na magari ya Serikali.
>>
>>
>>
>> 2013/5/22 Juma Mzuri <jumamzuri@gmail.com<http://mc/compose?to=jumamzuri@gmail.com>
>> >
>>
>> Askari mmoja na raia mmoja amefariki na ofisi ya ccm na kituo cha mafuta
>> vimechomwa moto
>>
>>
>> 2013/5/22 ezekiel kunyaranyara <ekunyaranyara@yahoo.co.uk<http://mc/compose?to=ekunyaranyara@yahoo.co.uk>
>> >
>>
>> Nasikia hata Guest Houses walizowahi kufikia askari wakati wa vurugu za
>> mwanzo zinachomwa moto (Not sure).
>>
>> Hali kama hii haifai kabisa kwa Taifa huru kama hili. Wahalifu lazima
>> wasakwe na wakamatwe na wafikishwe mbele ya mkono wa sheria.
>>
>> Naona hii sio gesi tu kuna kitu cha ziada hapa.
>>
>> Tutajua tu.
>>
>> K.E.M.S.
>>
>>  --
>> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>>
>> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
>> ukishatuma
>>
>> Disclaimer:
>> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any
>> legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts
>> must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you
>> agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>> ---
>> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
>> "Wanabidii" group.
>> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
>> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>>
>>
>>
>  --
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree
> to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>
>
>

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.



--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 


0 comments:

Post a Comment