Saturday 6 April 2013

[wanabidii] Taarifa ya CUFkuhusu Msaada kutoka Denmark na Ratiba ya Town Hall Meetings

Chama  cha The Civic United Fronf (CUF-Chama Cha Wananchi) kinapenda kuwajulisha wanachama wake  na Watanzania kwa ujumla kuwa Chama  cha CUF kimepata msaada wa ujenzi wa chama kupitia mafunzo na kufanya mikutano ya ndani 'Town Hall Meetings' ya kushirikisha wananchi katika kutoa maoni ya sera za Maendeleo kwa Wote (Inclusive Development) katika mikoa ya Tanzania katika dhana ya KUIMARISHA MFUMO WA DEMOKRASIA NDANI YA VYAMA VYA SIASA NA KUKUZA MIJADALA BAINA  YA VYAMA, WAPIGA KURA NA TAASISI MBALIMBALI ZA KIJAMII.  (Strengthening the democratic structure in political parties and dialogue between parties, voters and NGOs). 

Lakini pia kuwapatia mafunzo maalumu yenye madhumuni ya kuwajengea uwezo zaidi wanachama na viongozi wakekuhusiana na Namna ya kuandaa Sera/Manifesto na kuzitumia kwa wananchi(how to fomulate local policy agendas and Communicate it to the public), upangaji wa mikakati, masuala yanayohusiana na uratibu wa kampeni za uchaguzi (Strategic planning and effective elections management cycle and campaign) uongozi na uendeshaji wa oganaizesheni ya chama (Creating effective organizational structure) pia kutafanyika ziara za mafunzo Denmark kwa ajili ya kubadilishana uzoefu na kujifunza zaidi. 

Chama cha Radikale vestre cha Denmark kilifanya uchambuzi wa mapendekezo ya CUF kwa kuwa CUF-RV ni vyama vinavyoshabiiana kisera na itikadi na wote ni wanachama wa Liberal International na kuyaafiki. Mapendekezo ya Ushirikiano wa CUF na RV yalifikishwa Danish Institute for Parties and Democracy (DIPD) ambayo imekubali kutoa kiasi cha Danish krones (DKK)1.291.823 ambazo ni sawa na Tshs. 363 milioni kugharamia mradi huu wa ushirikiano.

Awamu ya kwanza ya mradi huu wa ushirikiano ni kufanyika kwa mikutano ya ndani ('Town hall Meetings') katika 
mikoa 5. Mikutano hii itawashirikisha wananchi 125 – 150 wa vyama vyote vya siasa, vyama vya kijamii na viongozi wa kiserikali kujadili mustakbali wa Maendeleo ya wananchi wote – Inclusive Development katika mkoa wao na hasa wilaya ambapo mkutano unafanyika.

Dhana ya Maendeleo kwa wote inasisitiza kila mtu ashiriki na ama ashirikishwe ili anufaike na kujivunia maendeleo ya nchi yake. Katika hali halisi ya Tanzania suala la kupatikana ajira inayowapa fursa raia kupata kipato cha kukidhi mahitaji yao ndiyo msingi muhimu wa kupatikana Maendeleo kwa Wote. Katika mikutano hiyo washiriki watatoa maoni na mapendekezo yao ya namna ya kutatua tatizo la ajira. 

Inafahamika kuwa Robo tatu ya Watanzania wanaishi vijijini na kutegemea kilimo. Mapinduzi ya kilimo yatakayoongeza tija na uzalishaji wa sekta ya kilimo na hasa miongoni mwa wakulima wadogo ni hatua ya lazima ili kupatikana maendeleo kwa wananchi wote. Ongezeko la uzalishaji wa chakula litapunguza mfumuko wa bei na gharama za chakula pia Upatikanaji wa lishe bora na ya kutosha utapunguza utapiamlo na kuboresha afya za wananchi. 

Upatikanaji kwa wingi wa nafaka, matunda, maziwa, nyama, pamba na mazao mengine yatachochea uanzishaji wa viwanda vitakavyoongeza ajira. Wakulima wanapoongeza kipato chao wananunua bidhaa nyingi za viwandani na kwa hiyo kuongeza soko la bidhaa na ajira ya wanaotengeneza bidhaa hizo.

Elimu ndiyo ufunguo wa maendeleo. Lengo la elimu ni kuwajengea uwezo watoto waweze kushamiri katika jamii watakapokuwa watu wazima kama wazazi na wahudumiaji wa watoto wao, washiriki katika shughuli za kijamii na kisiasa kama raia wema, na wawe wafanyakazi hodari na wenye tija na wapate kipato kinachokidhi mahitaji katika uchumi wa nchi yao. Je mfumo wetu wa elimu unawaandaa watoto wa Tanzania kuyafikia malengo haya? Kipi kifanyike ili malengo haya yaweze kufikiwa?

Afya njema inamfanya binadamu afurahie maisha yake. Binadamu mwenye afya njema anakuwa na uwezo wa kuchapa kazi na kushiriki katika shughuli za kijamii. Afya njema inajengwa toka mtoto akiwa katika tumbo la mama yake. Mama mjamzito anayepata lishe bora na kinga ya maradhi inasaidia kujifungua mtoto mwenye afya njema. Lishe bora ya mtoto na kinga ya maradhi inamjengea maungo imara, kinga ya mwili na kukuza ubongo wake ipasavyo. Hali ya huduma za msingi za afya ikoje katika nchi yetu? na kipi kifanyike kuziimarisha?

 Nchi yetu ina mali ya asili na raslimali nyingi ambazo hazijatumiwa kwa manufaa ya wananchi wote. Badala ya raslimali hizi kuwa Neema/Rehema zinaweza kuwa balaa. Mambo gani yafanyike ili maliasili za Taifa letu zitumiwe vizuri kuleta neema kwa wananchi wote.

 Baada ya kuzungumza na wadau mbalimbali katika maeneo yao, Waratibu wa Town Hall Meetings wamependekeza mada zifuatazao zitumiwe kuchokozea mijadala katika mikutano ya ndani. Lengo ni kupata mapendekezo ya wananchi wenyewe kuhusu ufumbuzi wa suala la msingi la kuwa na sera zitakazoharakisha Maendeleo kwa Wote na kwa hiyo kupata AGENDA FOR INCLUSIVE DEVELOPMENT.

 Mada zitakazowasilishwa na kujadiliwa ni pamoja na; (Identified Themes for Town Hall Meetings in different Regions);

 Tanga 07 Aprili 2013

  1. Kufufua kilimo cha mkonge katika Mashamba makubwa na kuhamasisha wakulima wadogo wa kilimo cha vyakula, mbogamboga na matunda, na ufugaji wa  n'gombe wamaziwa katika kupambana na  umaskini wa wananchi wa maeneo ya vijijini. (Rehabilitate large scale sisal industry and promote smallholder agriculture in food products, horticulture, and dairy industry to fight poverty in rural areas)
  2. Kutumia bandari ya Tanga kuanzisha eneo maalum la viwanda kuzalisha bidhaa za kuuza nchi za nje ili kuongeza ajira na kukuza uchumi wa Tanga. (Using Tanga port to develop an Export Processing Zone to promote industrialization and generate employment in Tanga Region.)
  3. Rasilimali ya Maendeleo ya Binadamu- elimu ya msingi (elimu ya awali, msingi na sekondari) na  huduma za msingi za Afya (Human Resources Development- Basic Education (pre-school, primary and secondary education) and basic health services

Mtwara 13 Aprili 2013;
  1. Matumizi ya rasilimali ya gesi kwa manufaa ya wakazi wa mikoa ya kusini na taifa kwa ujumla. (Utilization of GAS resource for the benefits of the local population of Southern Regions and the Nation at large)
  2. Maendeleo ya Kilimo cha wakulima wadogo – kuanzisha soko huria la korosho  na bidhaa nyingine za kilimo.(Smallholders' agriculture development -Liberalization of cash nut industry and other agricultural commodities)
  3. Rasilimali ya Maendeleo ya Binadamu- elimu ya msingi (elimu ya awali, msingi na sekondari) na  huduma za msingi za Afya (Human Resources Development- Basic Education (pre-school, primary and secondary education) and basic health services

Dar es Salaam 20 Aprili 2013;
  1. Matatizo ya miundombinu duni, ukosefu wa nishati ya umeme, maji na ufumbuzi wake kwa maendeleo ya Halmashauri  za manispaa za Dar es Salaam  na Taifa kwa ujumla. (The problems of poor infrastructure, lack of reliable energy/electricity, water supply and solutions for the development of Dar es Salaam Municipal Councils and the Nation at large.) 
  2. Tatizo la uwiano wa idadi ya watu (msongamano)na ukosefu wa ajira kwa wakazi wa Halmashauri za Manispaa za Dar es salaam. Namna ya kurasimisha sekta isiyo rasmi na kuendeleza SMEs (The problems of high population density and lack of employment for the residents of Dar es Salaam Municipal Councils. Formalization of informal sector and promotion of small and medium scale enterprises) 
  3. Changamoto zinazoikabili sekta ya elimu na elimu ya stadi za ufundi na ufumbuzi wake (The challenges facing education sector and vocational training and the way forward)
  4. Rasilimali ya Maendeleo ya Binadamu- elimu ya msingi (elimu ya awali, msingi na sekondari) na  huduma za msingi za Afya (Human Resources Development- Basic Education (pre-school, primary and secondary education) and basic health services

Tabora 27 Aprili 2013;
  1. Kilimo endelevu kwa maendeleo ya wakulima wadogo wa kilimo cha Tumbaku, mazao ya chakula, mifugo na ufugaji wa nyuki. Kilimo cha tumbaku na mazingira.  (Sustainable smallholders' agriculture development – Tobacco, food crops, livestock and bee-keeping. Is tobacco production environmentally sustainable?)
  2. Miundombinu duni na maendeleo katika Mkoa wa Tabora. (Poor infrastructure and development in Tabora Region) 
  3. Rasilimali ya Maendeleo ya Binadamu- elimu ya msingi (elimu ya awali, msingi na sekondari) na  huduma za msingi za Afya (Human Resources Development- Basic Education (pre-school, primary and secondary education) and basic health services

Mwanza 04 May 2013;
  1. Sekta ya madini na maendeleo ya wananchi wa mikoa ya ukanda wa ziwa na mchango wake katika maendeleo ya Taifa. (The Minerals sector and its contribution to development of the people of the Lake zone Regions and to the National development.) 
  2. Changamoto zinazowakabili wakulima wadogo wadogo katika sekta ya kilimo cha pamba, mazao ya chakula na sekta ya ufugaji katika Mkoa wa Mwanza. (The challenges facing smallholder cotton, food products and livestock farmers in Mwanza Region)
  3. Matatizo yanayoikabili sekta ya uvuvi na matumizi sahihi ya ziwa Victoria kwa maendeleo ya wananchi wa mikoa ya kanda ya ziwa. (The problems facing fishing industry and utilizations of Lake Victoria for the development of Lake zone Regions)
  4. Rasilimali ya Maendeleo ya Binadamu- elimu ya msingi (elimu ya awali, msingi na sekondari) na  huduma za msingi za Afya (Human Resources Development- Basic Education (pre-school, primary and secondary education) and basic health services

Hata hivyo washiriki watakuwa huru kuchangia juu ya masuala mbalimbali watakayoona yanafaa wakati wa mjadala. Baada ya kumaliza Town Hall Meetings katika mikoa mitano, tutafanya tathmini na kujipanga kukamilisha zoezi hili katika mikoa mingine. Mjadala wa mada hizi utasaidia chama chetu kuchambua Agenda ya Maendeleo kwa wananchi wote  (AGENDA FOR INCLUSIVE DEVELOPMENT) ili kufanya maandalizi ya kuboresha manifesto ya chama chetu cha CUF kwa uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2014 na uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Mwisho:

Chama cha CUF tunaamini katika HAKI SAWA NA MAENDELEO KWA WANANCHI WOTE katika Taifa letu. Kwa mantiki hiyo CUF tunaamini kuwa maendeleo ya Taifa letu yatapatikana kwa ushirikiano wa pamoja wa Watanzania wote, bila ya kujali mipaka ya kiitikadi za kisiasa, eneo analotoka, ukabila, dini ya mtu, na au rangi yake.

HAKI SAWA KWA WOTE

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment