Monday 15 April 2013

[wanabidii] Re: [Mabadiliko] Leo Nimefika Tena Makao Makuu Ya Jeshi La Polisi

Pole sana ndugu Majidy

Wanasheria tuelimishen kama hiv mh Majidy yupo kimakazi Iringa na jalada lipo Dar inakuwaje kuhusu gharama za kuja dar mara kwa mara na malazi?

Je haiwezekan kuomba jalada lihamishiwe mkoan au hata wilayan ambapo ni rahisi kwa mtuhumiwa kufika mara kwa mara

gm

From: Maggid Mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com>
Sender: mabadilikotanzania@googlegroups.com
Date: Mon, 15 Apr 2013 21:01:29 +0100
To: wanabidii<wanabidii@googlegroups.com>; mabadilikotanzania<mabadilikotanzania@googlegroups.com>
ReplyTo: mabadilikotanzania@googlegroups.com
Subject: [Mabadiliko] Leo Nimefika Tena Makao Makuu Ya Jeshi La Polisi

Ndugu zangu,

Leo nilifika tena Makao Makuu ya Jeshi la Polisi. Nilikutana na Kamishna wa Polisi ( Upelelezi) Advocate Nyombi na Afisa mwingine wa Idara hiyo.

Kamishna Nyombi alinijulisha kuwa uchunguzi wa suala la Kibanda ungali ukiendelea. Nami nabaki kwenye kundi la watuhumiwa; tuhuma za kumjeruhi Absalom Kibanda.

Tumekubaliana nifike tena Makao Makuu ya Polisi Aprili 23.

Ahsanteni sana kwa kuendelea kunifariji kwenye kadhia hii iliyonikuta. Na hakika, nawashukuru sana kwa kuendelea kuniamini.

Ni dhahiri, kuwa kweli itakuja kudhihiri, hata kama kweli hiyo itachelewa kutufikia. Na tuwe wenye subira.
Maggid,
Dar es Salaam.

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda; mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
 
TEMBELEA Facebook yetu:
http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
 
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forums" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment